Posts

Showing posts from December, 2023

KAMPUNI YA MAWASILIANO VODACOM YAGAWA ZAWADI NONO KWA WATEJA WAKE MSIMU HUU WA SIKUKUU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA

Image
 Na Pendo Mkonyi, Arusha  Kampeni ya Samabaza Shangwe gusa maisha nchini imeleta matokeo makubwa kufuatia washindi zaidi ya 5 kujipatia zawadi mbalimbali ikiwemo kitita cha pesa milioni 10,simu janja,Tv flat screen, Bodaboda  mara baada ya wateja wa Vodacom kufanya miamala mbalimbali kupitia mtandao wa Vodacom. Pichani ni mfanyabiashara wa vinyago  Prisikila Gabriel mkazi wa Ilboru jijini Arusha aliyejishindia zawadi ya milioni 10. Kutoka kampuni ya Mawasiliano Vodacom  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali Kwa wateja meneja msaidizi wa kampuni ya Mawasiliano Vodacom Kanda ya kaskazin Hendry Temu amesema  kampeni hiyo ilianza rasmi mwezi wa 11 mwaka 2023  nchi nzima ya Tanzania na hii ni mara ya 8 ambayo imefanyika kilombero jijini Arusha ikiwa kampeni hii imeshapita kwenye mikoa mbalimbali nchini. Pichani ni  meneja msaidizi wa kampuni ya Mawasiliano Vodacom Kanda ya kaskazin Hendry Temu  Alisema kuwa wateja ili waweze kushiriki kwenye kampeni hi

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.

Image
  Na Pendo Mkonyi, Arusha. Chuo Cha  Ufundi Stadi Cha Olokii kilichopo chini ya Kanisa la Kiinjili Kilutheri  Tanzania(KKKT)Dayosis ya kaskazin Kati Kinatangaza Dawati la udahili Kwa mwaka 2023/2024. Pichani ni Baadhi ya Wahitimu wa kozi  ya fani ya umeme katika chuo Cha Ufundi Olokii. Akizungumza na vyombo vya habari mkuu wa chuo cha Olokii Eng.Zelothe  Meshevi Mollel amesema kua Dirisha la udahili liko wazazi sasa kwa ajili ya kuwasaidia vijana kukamilisha ndoto zao. Alisema kuwa ikiwa kijana ana kiu ya kufikia ndoto zake chuo hicho  kipo tayari kumsaidia kwani wapo waalimu waliobobea katika masuala ya ufundishaji wa fani mbalimbali za ufundi. Aidha mpaka sasa chuo hicho kimeshazalisha wataam zaidi ya 900  tangu mwaka 2009 kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania. Watoto wa kitanzania wengi wao wapo kwenye ajira  mbalimbali  wakipigania ndoto zao katika sekta mbalimbali kutokana na kufuzu vema katika chuo cha kanisa cha Olokii. Mkuu wa chuo Eng. Zelothe wakati akizungumza na vyombo v

BENKI YA CRDB YATOA ZAWADI YA GARI KWA MTEJA

Image
Na Pendo Mkonyi Arusha  Wateja zaidi ya 500 wamefanikiwa kujishindia zawadi mbali mbali ikiwemo fedha thasilimu ,Magari,Laptop,Simu Janja kupitia benki ya crdb  Pichani ni  Mkuu wa Kitengo cha wateja na biashara ,Steven Adil alisema benki ya CRDB Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi gari hilo ,iliyofanyika katika benki hiyo tawi la Usariver wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha. Mkuu wa Kitengo cha wateja na biashara ,Steven Adil alisema benki ya CRDB ilitenga kiasi cha sh,milioni 350 kwa ajili ya kampeni hiyo iliyozinduliwa februali 14 mwaka huu,Mbagala jijini Dar-Es-salaam. Benki ya CRDB imekabidhi gari jipya aina ya Vanguard lenye thamani ya Milioni 30 kwa mshindi wa jumla Dkt Bakati Zuberi akitokea Mkoani Arusha,aliyeshinda kupitia kampeni maalumu ya Benki ni SimBanking kupitia simu za mkononi. "Kampeni hiyo imekuwa na manufaa makubwa sana kwa watanzania wenye kufahamu huduma zetu za kidigitali zinazopatikana benki ikiwemo mikopo na akaunti" Alisema kupitia kampeni hiyo benki

KAMPUNI YA SOIL FOR THE FUTURE TANZANIA LTD IME SAINI HATI YA MAKUBALIANO NA VIJIJI ZAIDI YA 2 WILAYANI MONDULI VYAINGIA MAKUBALIANO YA BIASHARA YA CABORN.

Image
 Na Pendo Mkonyi,Monduli Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha Joshua Nassari amesimamia zoezi la utiaji saini hati ya  makubaliano  kati ya kampuni ya Soil for the Future Tanzania Ltd na baadhi ya vijiji  wilayani Monduli Kwa lengo la kuzalisha Kaboni Pichani ni  Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha Joshua Nassari  Akizungumza wilayani Monduli wakati wa makubaliano hayo mhe Nassari amesema kuwa Asilimia kubwa ya wananchi wilayani Monduli ni wafugaji hivyo kama wakiboresha nyanda za  malisho watakuwa na uwezo wa kuinua kipatao Cha mtu mmoja mmoja na kuleta maendeleo. Alisema  kuwa kama biashara  hiyo ikifanikiwa yapo mpato yatapatikana ambapo fedha  zitakazopatikana ni Kwa ajili ya kufanya maendeleo ya wananchi hivyo ieleweke hizo siyo fedha za kuliwa hovyo kwani zitaingizwa  kwenye mfumo wa serikali  Alisema Kwa sasa Dunia nzima inahangaika kutokana na majanga ambayo yamefanywa na baadhi ya watu waharibifu wa mazingira hivyo ikiwa uhifadhi utazingatiwa basi manufaa yatakuwa mazur

MAHAFALI YA 3 YA SHULE YA GILISTEN YAFANYIKA WAZAZI WASHEHEREKEA UFAULU WA WATOTO WAO KUFUATIA SHULE KUWA YA KWANZA TANZANIA

Image
 Na Pendo Mkonyi, Simanjiro. Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Simanjiro Bwana Kiria Laizer amekiri kufurahishwa matokeo ya Darasa  la 7 katika shule ya Gilisten kufuatia kushika namba moja Tanzania  Pichani ni  Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Simanjiro Bwana Kiria Laizer Ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 3 ya darasa la 7 ya shule ya mchepuo wa kiingereza ya Gilisten iliyopo wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara na kusema kuwa jambo lililofanywa na Mhasisi wa shule ya Gilisten bwana Justin Nyari kuwekeza  shule katika wilaya hiyo ni jambo la kukumbuka milele kwani ni sadaka kubwa iliyotolewa mbele  za Mungu na kukubaliwa. Aliwapongeza wazazi wa mji  wa mererani kwa kutambua uwepo wa shule hiyo katika jamii kwani shule imelenga kuzalisha elimu na kutoa elimu Bora. Kadhalika aliwapongeza waalimu kwa kufanya kazi yao Kwa ufanisi mkubwa kwani kazi yao imefanyika Kwa kiwango Kikubwa na mtu ambaye alistahili kulipa mshahara mkubwa kuliko mtu awaye yote. Alisema kuwa utajiri b

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

Image
  Na Pendo Mkonyi, Arusha. Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mipango na  Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema Serikali inatambua umuhimu wa mtanzania bila kujali dini,kabila Haiba katika maendeleo ya Nchi. Picha ya mwisho ya Nic Geor Davie(NISHER) Akizungumza katika ibada  maalum ya maziko ya  kifo Cha Nisher Geor Davie kilichotokea mnamo  Tarehe 12 mwezi wa 12 ,prof Kitila alisema kuwa  Geor Davie ni mtu wa Mungu na amekuwa akiliombea Taifa lakini kibinadamu yeye ni binadamu kama watu wengine ana nyama na Damu hivyo anastahili kutiwa moyo kama walivyo binadamu wengine. Alisema kuwa Umri wa Nisher ni mdogo ukilinganisha na ahadi ya Mungu ,ya  mwanadamu kuishi miaka 70 kulingana na vitabu vya Mungu,miaka 66 Kwa mtanzania, japokuwa kuhusu kufa ni mpango wa Mungu kwani hakuna ajuaye anapaswa kuishi Kwa Muda Gani. Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza katika sherehe za Kumuaga Nisher amesema kuwa huwezi kutaja mkoa wa Arusha usitaje huduma ya kitaifa ya Ngurumo ya Upako. Alisema ku

WAZIRI WA FEDHA MWIGULU NCHEMBA AFUNGUA RASMI KONGAMANO LA 14 LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI MKOANI ARUSHA.

Image
 Na Pendo Mkonyi, Arusha. Waziri wa Fedha, dkt. Mwigulu Lameck Nchemba   ameipongeza PSPTB kwa kuendelea kusimamia maadili na mienendo ya Wataalam kwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa wataalam wanaokiuka miiko ya taaluma yao, likiwamo suala la kufanya kazi chini ya kiwango kama ilivyobainishwa kupitia taarifa ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (GAG). Pichani ni waziri wa fedha Dkt MWIGULU Nchemba.            Dkt. Nchemba ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linalofanyika katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha. Waziri wa Fedha, dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , akiziagiza sekta zote nchini kuhakikisha zinawatumia wataalam wa Ununuzi na Ugavi wenye sifa kwenye shughuli zao. Dkt. Nchemba alisema kuwa anasikitishwa na kuwepo kwa baadhi ya Wataalam wanaofanya kazi pasipo kuwa na sifa stahiki na bila kusajiliwa na Bodi kama ilivyo takwa la kifungu cha 11 cha Sheria ya PSPTB. “Changamoto ya kuwapo kwa wataalam ambao wanafanyakazi p

IFAHAMU AKAUNTI YA ELIMU JUNIOR INAVYOWANUFAISHA WATOTO WACHANGA NA WANAFUNZI NCHINI.

Image
 Na Pendo Mkonyi, Arusha. Meneja wa tawi la benki ya uchumi commercial  ya mkoani Kilimanjaro Bw James Kileo amewatoa hofu  wazazi na walezi wenye kipato Cha kati kutokuhangaika  wapi watapata fursa,kwani banki hiyo imekuja na Suluhisho la  elimu kupitia akaunti ya Elimu Junior itakayomrahisishia mtanzania yoyote kuhudumiwa. Akizungumza na waandishi wa habari Meneja huyo wa tawi Bwana Kileo amesema kuwa akaunti hiyo inamsaidia mtoto kuwekewa akiba na mzazi ama mlezi inayomuwezesha kupata mahitaji yake Kwa wakati ikiwemo kumfundisha mtoto umuhimu wa kuweka akiba na kuwa na nidhamu ya Fedha. Pichani ni  Meneja wa tawi la benki ya uchumi commercial  ya mkoani Kilimanjaro Bw James Kileo Amebainisha   mtoto wa siku moja anaweza kufunguliwa akaunti yake kupitia mzazi  Kwa  kuanzio Cha shilingi 5000 na cheti Cha kuzaliwa na akaunti hiyo Haina gharama zozote za uendeshaji ama makato. Amesema licha ya uwepo wa manufaa hayo wazazi wanapaswa kujua  akaunti hiyo inamsaidia mtoto Kwa kumpa kutambua

MAKUNDI MBALIMBALI YA JAMII YAMEJENGEWA UWEZO JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA MATOKEO YA SENSA YA WATU MA MAKAZI YA MWAKA 2022

Image
 Na Pendo Mkonyi, Arusha. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mhe. Zaituni Swai amesema kuwa, Takwimu za matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022, yatawawezesha viongozi na watalamu wa mkoa huo, kupanga mipango thabiti ya utekelzaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 iliyozinduliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa wiki iliyopita. Pichani ni Mbunge wa viti maalum mhe Zaituni Swai Mhe. Zaituni ameyasema hayo, kwenye mkutano wa Mafunzo ya Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 kwa viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa AIM MALL Jijini Arusha leo tarehe 11 Desemba, 2023. Amesema kuwa, matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yalikuwa ni ya Kisayansi zaidi livha ya kuonesha I bdadi ya watanzania ni milioni 61 huku Idadi ya watu katika mkoa wa Arusha wamefikia 2, 356, 255, ameongeza kuwa takwimu hizo zimeenda mbali zaidi yakionyesha idadi

HOSPITALI YA GEMSA ARUSHA YASISITIZA MATUMIZI YA BIMA ZA AFYA

Image
  Na Pendo Mkonyi, Arusha. Katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za Afya Hospitali binafsi ya  Gemsa  wameunga  mkono juhudi za serikali za  utoaji wa    matibabu Bora ya kibingwa  kupitia bima za Afya . Akizungumza na waandishi wa habari juu ya utoaji wa huduma za madaktari bingwa , magonjwa ya wanawake,mifupa,meno,masikio, pua na ngozi , mdhibiti ubora kutoka    Gemsa  Jijini Arusha ,Dkt Jimmy  Wilfred amesema  kila mtanzania  anapswa kupata huduma ya matibabu Bora kama adhma ya serikali inavyosisitiza kua na bima za Afya, hivyo wanaungana na serikali katika kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma Bora. Pichani ni M dhibiti ubora kutoka  hospital ya Gemsa  Jijini Arusha ,Dkt Jimmy  Wilfred Dr Jimmy Amewaasa wananchi ambao Bado hawajajiunga na huduma za afya za bima,kujiunga kutokana na kuokoa gharama na kumrahisishia mwananchi  matibabu ya uhakika kwani magonjwa  hayatoi taarifa. Kwa  upande wa wakazi wa jiji la  Arusha na watumiaji wa  huduma za bima ya afya wakati w

KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA CHA ARUSHA (AICC)CHAKABIDHI MISAADA YA KIUTU KWA WAHANGA KATESH

Image
 Na Prisca Libaga. Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeshiriki kwenye zoezi la kutoa msaada kwa wahanga waliokumbwa na changamoto ya mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyoisababishwa na mvua kubwa kwenye kijiji cha Katesh, Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara. AICC ilikabidhi msaada wa mablanketi 200 na kiasi cha shilingi milioni 12 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga aliyeambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt Jim James Yonazi na Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Karoline Mthapula mapema leo tarehe 07 Disemba 2023 kwenye Kijiji cha Katesh. Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa AICC, Afisa Uhusiano Mwandamizi  Fredrick Maro alisema AICC imeguswa na maafa hayo na inatambua wajibu wake wa kuisaidia jamii inayoizunguka. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa, Mhe. Queen Sendiga ameishukuru AICC kwa msaada wake uliofika kwa wakati