KAMPUNI YA SOIL FOR THE FUTURE TANZANIA LTD IME SAINI HATI YA MAKUBALIANO NA VIJIJI ZAIDI YA 2 WILAYANI MONDULI VYAINGIA MAKUBALIANO YA BIASHARA YA CABORN.
Na Pendo Mkonyi,Monduli
Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha Joshua Nassari amesimamia zoezi la utiaji saini hati ya makubaliano kati ya kampuni ya Soil for the Future Tanzania Ltd na baadhi ya vijiji wilayani Monduli Kwa lengo la kuzalisha Kaboni
Pichani ni Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha Joshua Nassari
Akizungumza wilayani Monduli wakati wa makubaliano hayo mhe Nassari amesema kuwa Asilimia kubwa ya wananchi wilayani Monduli ni wafugaji hivyo kama wakiboresha nyanda za malisho watakuwa na uwezo wa kuinua kipatao Cha mtu mmoja mmoja na kuleta maendeleo.
Alisema kuwa kama biashara hiyo ikifanikiwa yapo mpato yatapatikana ambapo fedha zitakazopatikana ni Kwa ajili ya kufanya maendeleo ya wananchi hivyo ieleweke hizo siyo fedha za kuliwa hovyo kwani zitaingizwa kwenye mfumo wa serikali
Alisema Kwa sasa Dunia nzima inahangaika kutokana na majanga ambayo yamefanywa na baadhi ya watu waharibifu wa mazingira hivyo ikiwa uhifadhi utazingatiwa basi manufaa yatakuwa mazuri
Alisema kuwa mkataba huo siyo wa kumpa mtu ardhi Bali ni Kwa ajili ya kuandaa nyanda za malisho na endapo mkataba huo ukikiukwa mkataba huo utavunjwa Muda wowote pamoja hivyo amewatoa wasiwasi wananchi wanaoenda kusaini hati hiyo ya makubaliano kufanya biashara hiyo ya Kaboni pamoja na uhifadhi wa nyanda za malisho.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Bi Happiness Laizer amesema kuwa Kwa kipindi cha Januari mpaka desemba 20223 kampuni ya ya Soil for the Future Tanzania Ltd imefanikiwa kutekeleza shughuli zifuatazo katika halmashauri ya kwanza ni kutambulisha mradi kuanzia ngazi ya vijiji hadi wilaya, pili ni kutoa elimu Kwa vijiji, na kuandaa na kuwasilisha hati ya makubaliano ya utekelezaji wa mradi kati ya kampuni na vivi husika.
Alisema kuwa wakati wa uwasilishwaji wa hati ya makubaliano ya biashara ya kaboni baina ya kampuni na vijiji husika changamoto ilitokea kwani wananchi hawakupata uelewa kwani walidhani wanaporwa ardhi yao jambo ambalo siyo kweli.
Mkurugenzi alisema kuwa kupitia biashara hiyo ya Kaboni wananchi wataweza kununua vifaa vya elimu mfano madawati,kujenga zahanati n a mengine kama hayo.
Alisema fedha zikishaingizwa kwenye akaunti ya serikali ya Kijiji ijulikane wazi fedha hizo ni serikali hivyo amesisitiza zitumiwe Kwa kuzingatia taratibu na kanuni ya matumizi ya fedha za serikali.
Kwa upande wa mkurugenzi wa kampuni ya Soil for the Future Tanzania Ltd Bwana Idd Mfunda amesema kuwa wao wamesajiliwa kufanya biashara ya kaboni na kiujikita kuhifadhi nyanda za malisho na kutekeleza majukumu yao Kwa ubia katika serikali na kampuni zingine sambamba na kutoa elimu Kwa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya Kaboni na uhifadhi wa mazingira.
Alisema kuwa kampuni hiyo tayari imeanza matayarisho ya miradi mikubwa minne ambapo kwa Tanzania ambapo huu ni mradi wa kwanza ambapo hapo baadaye watakuwa na mradi wa pili hifadhi in ya Taifa Serengeti ,mradi wa tatu hifadhi ya Taifa Ruaha mradi wa nne ni pori la akiba Lugala kaskazin mwa Tanzania.
Alisema bado hawajaanza biashara bali ni matayarisho ambapo kazi ya matayarisho na utekelezaji wa mradi husimamiwa na ofisi ya makamu wa Rais na waratibu wakuu ni wizara za kisekta ikiongozwa na ofisi ya ya Rais tawala za mikoa na serikali za mtaa.
Mratibu wa mradi Longido na Monduli Bwana Richard Ndaskoi amesema kuwa lengo kubwa la mradi ni kuboresha nyanda za malisho na kufanya biashara ya kaboni.
Hata hivyo amewaondoa hofu wananchi
Kuwa ardhi yao haitahamishwa Wala mifugo Yao kuhamishwa kwani kampuni hiyo ipo kuwasaidia kurejesha ile hali ya zamani wa kuwezesha mifugo kupata chakula Cha kutosha ikiwemo kuepusha uchungaji wa mifugo wa kuhamahama.
Comments
Post a Comment