CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Chuo Cha Ufundi Stadi Cha Olokii kilichopo chini ya Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosis ya kaskazin Kati Kinatangaza Dawati la udahili Kwa mwaka 2023/2024.
Pichani ni Baadhi ya Wahitimu wa kozi ya fani ya umeme katika chuo Cha Ufundi Olokii.
Akizungumza na vyombo vya habari mkuu wa chuo cha Olokii Eng.Zelothe Meshevi Mollel amesema kua Dirisha la udahili liko wazazi sasa kwa ajili ya kuwasaidia vijana kukamilisha ndoto zao.
Alisema kuwa ikiwa kijana ana kiu ya kufikia ndoto zake chuo hicho kipo tayari kumsaidia kwani wapo waalimu waliobobea katika masuala ya ufundishaji wa fani mbalimbali za ufundi.
Aidha mpaka sasa chuo hicho kimeshazalisha wataam zaidi ya 900 tangu mwaka 2009 kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Watoto wa kitanzania wengi wao wapo kwenye ajira mbalimbali wakipigania ndoto zao katika sekta mbalimbali kutokana na kufuzu vema katika chuo cha kanisa cha Olokii.
Mkuu wa chuo Eng. Zelothe wakati akizungumza na vyombo vya habari ametaja fani zinazotolewa na chuo cha Olokii kuwa ni pamoja na :
UMEME WA MAJUMBANI (ELECTRICAL INSTALLATION)
UCHOMELEAJI VYUMA (WELDING AND METAL FABRICATION)
USHONAJI (DESIGN, SEWING AND CLOTH TECHNOLOGY)
USEREMALA (CARPENTRY AND JOINERY)
UJENZI (MANSONRY AND BRICKLAYING)
UFUNDI WA MAGARI (MOTOR VEHICLE MECHANICS)
Hata hivyo c onhuo kinatoa ofa ya Punguzo la ada kwa wanafunzi watakaowahi chuoni Ofa hii ni ya mwezi mmoja( 1) wa tano na mafunzo ya Komputer na Ujasiriamali ni bure kwa wanafunzi watakao jiunga.
Kwa Mawasiliano zaidi unaweza kupiga simu zifuatazo: 0752405073 / 0714625936
Comments
Post a Comment