HOSPITALI YA GEMSA ARUSHA YASISITIZA MATUMIZI YA BIMA ZA AFYA
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za Afya Hospitali binafsi ya Gemsa wameunga mkono juhudi za serikali za utoaji wa matibabu Bora ya kibingwa kupitia bima za Afya .
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya utoaji wa huduma za madaktari bingwa , magonjwa ya wanawake,mifupa,meno,masikio, pua na ngozi , mdhibiti ubora kutoka Gemsa Jijini Arusha ,Dkt Jimmy Wilfred amesema kila mtanzania anapswa kupata huduma ya matibabu Bora kama adhma ya serikali inavyosisitiza kua na bima za Afya, hivyo wanaungana na serikali katika kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma Bora.
Dr Jimmy Amewaasa wananchi ambao Bado hawajajiunga na huduma za afya za bima,kujiunga kutokana na kuokoa gharama na kumrahisishia mwananchi matibabu ya uhakika kwani magonjwa hayatoi taarifa.
Kwa upande wa wakazi wa jiji la Arusha na watumiaji wa huduma za bima ya afya wakati wakizungumza na waandishi wa wameelezea umuhimu wa kutumia bima za afya katika kupata matibabu ya afya kupitia bima hizo ambazo Ni NHIF, STRATEGY, MO ASSURANCE Ambapo huduma zote zinatolewa kwa watumiaji wa bima hizo katika hospital ya GEMSA ya jijini Arusha.
Hata hivyo hivi karibuni waziri wa afya mh ummy mwalimu alisisitiza watanzania kuwa na bima ya afya Ili kuwarahisishia kupata matibabu ya uhakika pindi wanapopata changamoto za kiafya.
Comments
Post a Comment