KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA CHA ARUSHA (AICC)CHAKABIDHI MISAADA YA KIUTU KWA WAHANGA KATESH

 Na Prisca Libaga.

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeshiriki kwenye zoezi la kutoa msaada kwa wahanga waliokumbwa na changamoto ya mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyoisababishwa na mvua kubwa kwenye kijiji cha Katesh, Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara.


AICC ilikabidhi msaada wa mablanketi 200 na kiasi cha shilingi milioni 12 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga aliyeambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt Jim James Yonazi na Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Karoline Mthapula mapema leo tarehe 07 Disemba 2023 kwenye Kijiji cha Katesh.Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa AICC, Afisa Uhusiano Mwandamizi  Fredrick Maro alisema AICC imeguswa na maafa hayo na inatambua wajibu wake wa kuisaidia jamii inayoizunguka.



Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa, Mhe. Queen Sendiga ameishukuru AICC kwa msaada wake uliofika kwa wakati

Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.