MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema Serikali inatambua umuhimu wa mtanzania bila kujali dini,kabila Haiba katika maendeleo ya Nchi.
Picha ya mwisho ya Nic Geor Davie(NISHER)Akizungumza katika ibada maalum ya maziko ya kifo Cha Nisher Geor Davie kilichotokea mnamo Tarehe 12 mwezi wa 12 ,prof Kitila alisema kuwa Geor Davie ni mtu wa Mungu na amekuwa akiliombea Taifa lakini kibinadamu yeye ni binadamu kama watu wengine ana nyama na Damu hivyo anastahili kutiwa moyo kama walivyo binadamu wengine.
Alisema kuwa Umri wa Nisher ni mdogo ukilinganisha na ahadi ya Mungu ,ya mwanadamu kuishi miaka 70 kulingana na vitabu vya Mungu,miaka 66 Kwa mtanzania, japokuwa kuhusu kufa ni mpango wa Mungu kwani hakuna ajuaye anapaswa kuishi Kwa Muda Gani.
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza katika sherehe za Kumuaga Nisher amesema kuwa huwezi kutaja mkoa wa Arusha usitaje huduma ya kitaifa ya Ngurumo ya Upako.
Alisema kuwa kutokana na utaratibu wa serikali kuwa msingi wake ni watu basi mahali Ambapo panasisitiza amani kama tiba mfano huduma ya Ngurumo ya Upako ni mahali pa kuheshimiwa
Amemtia Moyo Nabii Mkuu Geor Davie na kuahidi serikali kumuunga mkona juhudi zinazofanya na huduma ya Ngurumo ya upakoo kwani pia Mungu yupo upande wako kufuatia wewe kuwa mtu imara sana.
Mlezi wa chuo cha Manabii Askofu Dunstan Maboya wakati akihubiri katika ibada ya mazishi alisema kuwa Kuna vitu vingi sana vinavyotokea katika familia kunakuwepo na kigugumizi sana hususani familia maarufu kama vile familia za watumishi wa Mungu ambapo alitumia nafasi hiyo kumtia moyo Nabii Mkuu Geor Davie kuwa wakubali kijana wao amekubali kwani watakapokubali msiba utakuwa mwepesi ndipo wataweza kusherehekea
Alisema kuwa Nisher siyo wa kwanza kufariki kutoka katika nyumba za watumishi wa Mungu mfano Ayubu katika maandiko matakatifu alizika watoto wake wote 7,mfalme Daudi naye pia alipoteza mwanae licha ya ufalme na umaarufu alipokuwa nao
Alisema kuwa hii ni Baadhi ya mifano ya watu wa Mungu waliofikwa na misiba na pia stephano alivyokufa Kwa kupigwa mawe mpaka akafa hii inaonesha watu wataondoka.
Maboya alisema kuwa Mungu anapendezwa na watu wenye moyo wa kishujaa na subirai na ijulikane kuwa mfariji wa kweli ni roho mtakatifu na mateso ya mwenye haki ni mengi lakini Mungu huwaokoa na yote.
Kutoka 35:30-32
[30]Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, BWANA amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;
[31]naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;
[32]na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba,
Alisema kuwa kijana Nic Davie(Nisher ) alikuwa mkarimu na kijana mchapa kazi hivyo alivyosikia habari za kufa Kwa kijana Mungu akampa Hilo neno.
Dkt Maboya alisema kuwa alihuzinishww na kifo hicho Kwa kurudi Kwa kufikiria jinsi mzazi alivyowekeza katika mahitaji na malezi japokuwa Mungu amesisitiza mtu kufanya kazi Kwa bidii ili msiwalemee wengine.
Kuzaliwa:Nic Davie alizaliwa mjini Arusha Tanzania mnamno Julai8,1989 akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya Nabii Mkuu Deor Davie na mchungaji kiongozi Mama Anna Davie,mtoto wa pili akiwa ni Monica Davie na WA mwisho akiwa niKen Davie.
Nic Davie alikuwa kijana mkarimu mcheshi na mwenye moyo wa upendo Kwa Kila mtu bila ubaguzi.
Elimu:Nic Davie akisoma Tanzania na kuziendeleza zaidi nchini Marekani katika maswala ya audio na video industry .
Kazi:Nic Davie alikuwa kijana mchapa kazi sana na mwenye ubunifu mkubwa katika kazi zake na kuwa mfano wa kuigwa na vijana wengi ndani na nje ya Tanzania.
Nic Davie alikuwa mtayarishaji na miongozaji wa video za muziki na filamu,sound engineer,recording engineer,mtaalam wa information Technology (IT),Mtangazaji wa redio na Televisheni,piaalikuwa msanii wa Muziki,muigizaji pamoja na mtayarishaji wa sauti(voice over artist).
Nic Davie alipata umaarufu mkubwa kutokana na kazi zake za uzalishaji na uongozaji wa video za muziki wa bongoflava na nyinginezo aliweza kufanya kazi kama wasanii wakubwa kama vile,Kundi la Weusi,Joh Makini,Fid Q,Benpol ,Shilole,Belle9,Baraka de Prince n.k.
NicDavie alisafiri kwenda nchi mbalimbali na baba yake mzazi Kwa kazi za huduma kama vile nchi ya Marekani,Israel,Misri,Afrika Kusini,Kenya na Falme za Kiarabu(Dubai)
Pia akizungumza mikoa mbalimbali nchini Tanzania akirekodi matukio yote ya kihistoria na kutunza katika mfumo wa video na sauti ambapo baadhi ya kazi zake ni kama mkutano uliofanyika viwanja vya BIAFRA jijini Dar es salaam mwaka 2008, mkutano uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza mwaka 2007 mkutano mkubwa uliofanyika kwenye viwanja vya magereza jijini Arusha mwaka 2006,mkutano mkubwa uliofanyika viwanja vya stadium jijini Arusha mwaka 2010 kongamano kubwa lililofanyika ukumbi wa mikutano ya kimataifa Arusha(AICC)mwaka 2016 pamoja na ziara ya soko la Samunge ilyofanyika januari mwakahiu 2023.
Kifo:Nic Davie(NISHER) amefariki katika umri mdogo wa miaka 34 .Marehemu alianza kuugua mwanzoni mwa mwezi Novemba aliwahishwa hospital, madaktari walijitahifi Kwa kadri ya uwezo wao kurejesha afya ya mpendwa wao mpaka umauti ulipomfika Tarehe 12 mwezi wa 12 mwaka 2023 saa nane na dakika tisa usiku
Kwa upande wao Benpol msemaji wa wasanii wa ametoa pole Kwa familia na wasanii Kwa kumpoteza mtu mhimi lakini amesema kuwa kupitia Nisher wamezaliwa watayahirishaji wengi,ajira nyingi wamesema asante
Nabii Mkuu Geor Davie wakati msanii Benpol alipomaliza kutoa salamu za pole Alivunja ratiba na kusimam na kuahidi kuwasaidia vijana wakati wote iwe ni Kwa pesa hata ushauri.
Alisema kuwa watu ni hazina endapo mkiwekeza Kwa bidii katika miyoyo Yao kwani watakukumbuka daima.
Mrisho Mashaka Gambo Mbunge wa jimbo la Arusha mjini wakati akizungumza katika ibada hiyo maalum aliweza kutoa salamu za pole na kumtia moyo Mkuu Nabii Geor Davie kuwa huwezi kuwa mtu mkubwa usipate mitihani hivyo pole sana.
Kauli mbiu ya msiba huo Kwa kijana Nisher ni pumzika Kwa Amani mbunifu mwenye fikra za nje ya box.
Comments
Post a Comment