MAHAFALI YA 3 YA SHULE YA GILISTEN YAFANYIKA WAZAZI WASHEHEREKEA UFAULU WA WATOTO WAO KUFUATIA SHULE KUWA YA KWANZA TANZANIA
Na Pendo Mkonyi, Simanjiro.
Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Simanjiro Bwana Kiria Laizer amekiri kufurahishwa matokeo ya Darasa la 7 katika shule ya Gilisten kufuatia kushika namba moja Tanzania
Ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 3 ya darasa la 7 ya shule ya mchepuo wa kiingereza ya Gilisten iliyopo wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara na kusema kuwa jambo lililofanywa na Mhasisi wa shule ya Gilisten bwana Justin Nyari kuwekeza shule katika wilaya hiyo ni jambo la kukumbuka milele kwani ni sadaka kubwa iliyotolewa mbele za Mungu na kukubaliwa.
Aliwapongeza wazazi wa mji wa mererani kwa kutambua uwepo wa shule hiyo katika jamii kwani shule imelenga kuzalisha elimu na kutoa elimu Bora.
Kadhalika aliwapongeza waalimu kwa kufanya kazi yao Kwa ufanisi mkubwa kwani kazi yao imefanyika Kwa kiwango Kikubwa na mtu ambaye alistahili kulipa mshahara mkubwa kuliko mtu awaye yote.
Alisema kuwa utajiri bila vitendo ni kazi Bure hivyo jambo alilofanya Nyari kujenga shule mererani ni jambo la kuigwa katika jamii ambalo kila mwekezaji katika mji wa mererani anapaswa kulifanya pasipokushurutishwa..
Aliwataka wawekezaji kuhakikisha mji wa mererani unakuwa na kuongezeka isiwe tu watu wanakuja wanachukua madini wanaacha mji huo kimasikini kwani Mungu aluweka madini hayo Kwa makusudi.
Pia aliwapongeza wanafunzi wote waliofanya vizuri kutoka shule ya Gilisten kwani wameheshimisha mji wa mererani ambapo aliwasihi wazazi kuendelea kuwasomesha watoto hapa mirerani hakuna ya sababu ya wazazi kuwapeleka watoto nje ya mji huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya Gilisiten Bwana Justin Nyari wakati akizungumza katika Mahafali hayo ya 3 amesema uwekezaji uliofanyika ni Kwa ajili ya Mungu na wananchi.
Alisema kuwa mradi wa shule amabao umefanywa na Taasis hii ya elimu ya Gilisten ni Kwa ajili ya kuwainua watoto wa kitanzania kuweza kunufaika na mpango wa elimu.
Alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Awamu ya Sita Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwezesha elimu bure Kwa watoto wa kitanzania kwani mradi huo wa elimu umeleta manufaa makubwa sana.
Akizungumzia shule ya Glisten alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kufuatia kuzidi kufanya vizuri idadi ya awali ikiwa ni 15 na baadaye 21 na kisha kuongezeka zaidi na hii imechangiwa na uwepo wa waalimu mahiri kutoka shule ya Glisten.
Alisema kuwa shule hiyo kama ingetangazwa Tena kufanya mitihani ya darasa la 7 ingeshika namba moja kwani imefaulisha Kwa kiwango Cha alama 292.
Mkurugenzi wa shule alisema kuwa watoto wanaelimishwa siyo kukaririshwa hivyo badao amewekeza nguvu kubwa sana kuhakikisha watoto wanapata elimu Bora.
Aidha mhasisi huyo wa shule ya Glisten alisema kuwa tayari wameshawekeza eneo lingine la shule na januari watoto wataingia darasani kujisomea.
Aliwakemea baadhi ya wananchi wasiokuwa na maneno ya hekima kufuatia kutoa maneno ya uongo juu ya mitihani ya shule hiyo kuvujishwa jambo ambao siyo kweli
Bilionea Saninu Laizer wakati akizungumza katika Mahafali hayo ya 3 ya shule ya mchepuo wa kiingereza ya Gilisten Amesema kuwa amefurahishwa na mwenendo wa shule hiyo kufuatia wanafunzi kuonyesha maadili mema.
Alisema kuwa endapo watu wasomi kama hao watapatikana maendeleo yatakuwa makubwa mererani na Tanzania Kwa ujumla.
Aliwapongeza watoto Kwa kufanya vizuri ambapo aliwakumbusha kuwa bado wanahitajika kusoma kwani elimu waliyoipata bado ni ndogo sana haitoshelezi waendelee kujipanga na masomo yao.
Mkuu wa shule ya Glesten wakati akiitoa historia ya shule hiyo Alisema kuwa alama za matokeo mwaka huu 2023 281.mpaka.292.0 ambapo shule ya Gilisten imefanikiwa kuongoza na kufaulisha kiwango cha juu
Alisema kuwa wanatarajia makubwa kuliko hayo na malengo ya kufikia 300 shule hii inaongoza kitaaluma na kimatokeo shule hii inafanya vizuri hakuna shule nyingine inayowafikia
Shule ya Glisten imekuwa ikifaulisha Kwa kiwango Kikubwa kufuatia watoto kupangwa shule za Ilboru na nyingine kama hizo.
Alisema kuwa shule Yao imekuwa ikisemwa Kwa Mengi ijapokuwa hawana Muda wa kusikiliza yasemwayo zaidi ya kuendelea kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufanya vizuri kitaaluma
Glory Abas Akizungumza Kwa niaba ya wanafunzi wenzake alisema kuwa walivyo Leo wanafunzi waliofanya vizuri ni kwasababu ya waalimu mahiri.
Pia amewapongeza wazazi Kwa kufanya uwekezaji mkubwa wa elimu katika maisha yao kwani maarifa waliyoyapata kamwe hayawezi kuharibika .
Dina Mbise mratibu elimu kata ya mererani wakati akizungumza katika Mahafali hayo amewataka Wahitimu kwenda kupambana zaidi kwani bado mnahitajika kujisomea kama ambavyo mlukuwa mkisoma hapa Glesten.
Aliwapongeza waalimu Kwa kujitoa kuwasaidia watoto hao kufanya vizuri katika mitihani yao ya Darasa la 7 ambapo aliwashukuru wazazi Kwa kuwatendea haki watoto kwa kuwajali na kuwapa mahitaji yao ya msingi kwa wakati.
Kadhalika aliwataka wazazi kwenda kuwalea watoto katika maadili mema ya kumhofu Mungu ambapo katika mahafali hayo zaidi ya milioni 3 zilikusanywa Kwa ajili ya kuwapa waalimu kama motisha ambapo zoezi Hilo liliongozwa na mhasisi wa shule hiyo ya Gilisten.
Hata hivyo jumla ya Wahitimu 42 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi ya darasa la 7.
Comments
Post a Comment