IFAHAMU AKAUNTI YA ELIMU JUNIOR INAVYOWANUFAISHA WATOTO WACHANGA NA WANAFUNZI NCHINI.
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Meneja wa tawi la benki ya uchumi commercial ya mkoani Kilimanjaro Bw James Kileo amewatoa hofu wazazi na walezi wenye kipato Cha kati kutokuhangaika wapi watapata fursa,kwani banki hiyo imekuja na Suluhisho la elimu kupitia akaunti ya Elimu Junior itakayomrahisishia mtanzania yoyote kuhudumiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja huyo wa tawi Bwana Kileo amesema kuwa akaunti hiyo inamsaidia mtoto kuwekewa akiba na mzazi ama mlezi inayomuwezesha kupata mahitaji yake Kwa wakati ikiwemo kumfundisha mtoto umuhimu wa kuweka akiba na kuwa na nidhamu ya Fedha.
Amebainisha mtoto wa siku moja anaweza kufunguliwa akaunti yake kupitia mzazi Kwa kuanzio Cha shilingi 5000 na cheti Cha kuzaliwa na akaunti hiyo Haina gharama zozote za uendeshaji ama makato.
Amesema licha ya uwepo wa manufaa hayo wazazi wanapaswa kujua akaunti hiyo inamsaidia mtoto Kwa kumpa kutambua uwepo wa taasis za kifedha , umuhimu wake ikiwemo thamani ya fedha,akiba ,utunzaji,na itamsaidia hata atakapokuwa mtu mzima katika ulimwengu wa Sasa
Kadhalika benki ya uchumi kupitia akaunti ya Elimu Junior inahudumiaa kundi la wanafunzi, watoto wachanga, zaidi ya 1000 ambao wamefunguliwa akaunti,na itamsaidia mwanafunzi kukamilisha mahitaji yakielelimu na pindi anapopata changamoto za kiafya hupata matibabu.
Mbali na hayo amesema zipo akaunti za vijana ambazo ni maalumu kwajili ya vijana wenye umri wa miaka 18 na kuendelea,na kumuwezesha kijana kufanya miamala nyakati zote, kuunganishwa na mifumo mingine wezeshi ikiwemo yakibenki.
Ipo akaunti ya mavuno ambayo inawezesha mtu yoyote kuweka fedha zake nakupata faida ya asilimia 9 Kila mwisho wa mwaka ambayo ni nzuri kama jamii yakitanzania ikaitumia kwajili ya matumizi mazuri ya fedha zao.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara na Masoko wa bank hiyo,Israel lyatuu amesema bank hiyo ya wananchi ilianzishwa mwaka 2005 na wanamatawi 4 ,matatu yakiwepo Mkoani Kilimanjaro na moja wilaya ya Karatu Arusha na imekuwa ikitoa huduma zake Kwa Miaka 18 Sasa Kwa kutoa huduma zakifedha ikiwemo wafanyabiashara,Taasisi za Kanisa, Mtu mmoja mmoja kubwa nikuwafikia makundi yote ndani yajamii.
Amesema ipo mikopo ya vikundi ambapo Hadi Sasa watu elfu 30 kutoka vikundi zaidi ya 1500 wamefikiwa Kwa kutoa mikopo zaidi ya shilingi billion 38 Kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo,wakati na wakubwa ,na mikopo hiyo Haina gharama zozote.
Amesema ipo mikopo ya kilimo na wafugaji na hii ni ili kurahisha maendeleo endelevu katika sekta hizo Kwa masilahi mapana ya Taifa .
Uchumi bank inatoa bima Kwa wateja wake ikiwemo nyumba dhidi ya moto, majanga,mvua hususani kipindi hiki Cha mvua wa elninyo wananchi wanapaswa kukata ili kukingwa na majanga ama athari zitakanazo na majanga mbalimbali.
Mbali na hayo wanatoa huduma yakuwaunganisha wateja na huduma mtandao(internet bank) mahala popote kupitia mawakala waliopo mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, nakueleza wamepanua wigo wa utoaji wa huduma ikiwemo kuipeleka bank hiyo makao makuu ya nchi ,mkoani Dodoma .
Comments
Post a Comment