KAMPUNI YA MAWASILIANO VODACOM YAGAWA ZAWADI NONO KWA WATEJA WAKE MSIMU HUU WA SIKUKUU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA
Na Pendo Mkonyi, Arusha
Kampeni ya Samabaza Shangwe gusa maisha nchini imeleta matokeo makubwa kufuatia washindi zaidi ya 5 kujipatia zawadi mbalimbali ikiwemo kitita cha pesa milioni 10,simu janja,Tv flat screen, Bodaboda mara baada ya wateja wa Vodacom kufanya miamala mbalimbali kupitia mtandao wa Vodacom.
Pichani ni mfanyabiashara wa vinyago Prisikila Gabriel mkazi wa Ilboru jijini Arusha aliyejishindia zawadi ya milioni 10. Kutoka kampuni ya Mawasiliano Vodacom
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali Kwa wateja meneja msaidizi wa kampuni ya Mawasiliano Vodacom Kanda ya kaskazin Hendry Temu amesema kampeni hiyo ilianza rasmi mwezi wa 11 mwaka 2023 nchi nzima ya Tanzania na hii ni mara ya 8 ambayo imefanyika kilombero jijini Arusha ikiwa kampeni hii imeshapita kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Alisema kuwa wateja ili waweze kushiriki kwenye kampeni hiyo lazima wawe wanatumia miamala ya vodacom kulipa kwa simu kutuma fedha,kujinunulia muda wa hewani au vifurushi ambapo Kwa namna hiyo anaweza kushiriki kwenye shindano au kuweza kusambaziwa shangwe ili kujipatia nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kutoka Vodacom.
Bwana Temu amesema kuwa Leo katika jiji la Arusha wapo wateja waliojishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu Milioni 10,Tv flat screen,bodaboda,simu janja mara baada ya kufanya miamala mbalimbali ya kifedha Kupitia mtandao wa Vodacom.
Alisema kuwa kampuni ya Mawasiliano Vodacom imefanikiwa kulipia bima za afya Kwa watoto 100 na wamama 100 katika hospital ya mkoa ya mount meru Kwa kipindi cha mwaka mzima hii imetokana na wateja wanaofanya miamala ya kununua bando,au kutumia mpesa ambapo tayari wamechangia kugusa maisha ya watu wengine.
Aidha kampuni ya Mawasiliano Vodacom imekuwa msitari wa mbele kugusa maisha ya jamii moja Kwa moja mfano kuchangia mambo ya kijamii kama vile kuchangia vifaa vya elimu vya shule mbalimbali,kutunza mazingira,kuchangia huduma za kiafya na kutunza afya za watu ambapo kampuni hiyo imesema itaendelea kufanya zoezi hiilo Kwa kurudisha Ile sehemu wanayoipata ili kuwapinguzia wananchi mizigo wanayokutana nayo katika maisha.
Pia mwaka Jana kampuni ya Mawasiliano ya vodacom ilikuwa na kampeni ya amsha shangwe, amsha ndoto ambapo kampeni hiyo ilikuwa inahamasisha kugusa maisha ya Mtu mmoja mmoja kwenye ndoto yake alikuwa nayo ambapo yamkini Kuna mtu alikuwa amekwama kwenye ujenzi lakini kampuni ikamsaidia Kwa kugusa maisha yake.
Meneja huyo alisema kuwa, kampuni ya Mawasiliano ya vodacom imekuwa ikibuni aina ya kampeni ya kuja nayo Kwa wananchi lengo likiwa ni kuwainua kiuchumi watanzania kupitia miamala mbalimbali ya kifedha wanayoifanya.
Alitoa wito kwa watanzania kuondokana na utamaduni wa kujiwekea fedha majumbani na badala yake watunze fedha Kwa njia za kidigitali ikiwemo kutunza fedha kwenye Simu kwani pia inawezesha kupata huduma zote kwenye Simu mfano katika huduma za afya,usafiri hotelini na waondokane na kutembelea na fedha nyingi kwani ni vigumu hata wezi kumwibia.
Hata hivyo aliwahimiza watanzania kutumia miamala mbalimbali ya kifedha kujipatia huduma mbalimbali za kijamii pasipokutembea na maburungutu ya fedha mfukoni.
Kwa upande wake Prisikila Gabriel mkazi wa Ilboru mkoani Arusha mfanyabiashara soko la vinyago jijini Arusha mteja aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 10 amesema kuwa amefurahi sana kujishindia zawadi ya fedha kwani itamuwezesha kwenda kufanya ujenzi wa nyumba ambapo amewahimiza watanzania wengine kutumia mtandao wa Vodacom na kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ili iujiweka kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.
Pichani ni Prisikila Gabriel mkazi wa Ilboru mkoani Arusha mfanyabiashara soko la vinyago jijini Arusha
Godfrey Urassa ni mkazi wa Arusha aliyejishindia Tv flat screen amesema kuwa ni mara ya kwanza kujipatia zawadi ya sambaza shangwe kutoka Vodacom kwani amekuwa akinunua bando,umeme, vifurushi na hata kubeti kwenye mpira,na amesema alikuwa hajui ila tarehe 19/12/2023 alishangaa kupigiwa simu kutoka Vodacom alishangaa sana na hakuamini lakini baadaye aliamini .
Hata hivyo amewahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kununua bidhaa mbalimbali kupitia mtandao wa Vodacom kwani unalipa na ni uhakika ikiwemo kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ili wajishindie zawadi nono kama alivyojishindia.
Comments
Post a Comment