Posts

Showing posts from November, 2023

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI INNOCENT BASHUNGWA AFUNGUA KONGAMANO LA 32 LA WAHANDISI JIJIJINI ARUSHA AMBAPO WAHANDISI 57

Image
 Na Pendo Mkonyi,Arusha. Waziri wa ujenzi na uchukuzi Innocent Bashungwa  wakati akizungumza katika kongamo Hilo amewataka wahandisi kutumia fursa ya kongamano Hilo  kujitathimini. Baadhi ya wahandisi waliopatiwa kiapo katika kongamano la 32 la wahandisi  Alisema kuwa serikali inatambua taasis ya wahandisi Tanzania katika kuendeleza mezania ya serikali ambapo aliitaka taasis kuhakikisha inajitangaza ili wahusika waone umuhimu wa kujiunga na taasis yao. Alisema kuwa( IET)kuwa na umri wa miaka 48 bado idadi ya wanachama ni ndogo kwani mpaka Sasa wanachama wamekaribia zaidi ya wahandisi elfu 4. Bashungwa alisema kuwa Taasisi hiyo inapaswa kutatua changamoto zinazoikabili taasis hiyo ikiwemo kuwa msitari wa mbele kuishauri nchi zaidi ya Taasis ya kitaaluma. Aidha wahandisi wametakiwa kutumia nafasi zao ipasavyo Kwa kuwa Suluhisho Kwa maendeleo endelea kufuatia kuwepo Kwa teknolojia mbalimbali kwani serikali unatumika Tehama katika ufanisi wa mambo mbalimbali  ili kuleta majawabu ya hayo. A

CHUO KIKUU CHA ARUSHA CHAKARIBISHA WAGENI KUTOKA NCHI ZA MBALI KUFANYA UTALII NA UTAFITI NCHINI TANZANIA.

Image
 Na Pendo Mkonyi, Arusha. Taasis ya kanisa la Waadventista wasabato ulimwenguni itwayo Geo science research institute inayojishughulisha na kufanya utafiti unaotoa ujuzi  jinsi ya Dunia ilivyotokea imetembelea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini lengo likiwa ni kufanya utafiti. Akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya ziara hiyo naibu makamu mkuu wa chuo kikuu Cha Arusha Profesa Pearson Mnkeni Kwa niaba ya  makamu mkuu wa chuo kikuu cha arusha Profesa Patrick  Manu alisema kuwa wamekuwa na wageni kutoka katika taasis ya wasabato ambapo wamefanikiwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii na kujifunza kwa mambo mengi yahusuyo  jiolojia. Pichani ni   naibu makamu mkuu wa chuo kikuu Cha Arusha Profesa Pearson Mnkeni Aidha Wadventista wasabato duniani wanaamini duniani imeumbwa na Mungu  Kwa kipindi Cha siku 6 na siku ya 7 Mungu  akapumzuka ikawa ni sabato ambapo zipo nadharia nyingi zinasema kuwa mwanadamu alibuka tu kutoka kwenye  chembechembe vidogo ambapo taasis ni kufa

ONGEZEKO LA NAULI ZA DALADALA NA MAGARI YA MASAFA MAKUBWA KUPANDA DESEMBA 8

Image
Na Pendo Mkonyi, Arusha. Mamlaka ya usafiri Ardhini Latra imetangaza ongezeko la nauli  viwango vya mabasi na daladala hapa Nchini mara baada ya siku 14 kuisha kuanzia leo Pichani ni  Mkurugenzi  mkuu wa Latra Taifa Habibu Juma Suluo  Akizungumza katika Kikao kizazi hicho  Mkurugenzi  mkuu wa Latra Taifa Habibu Juma Suluo katika kikao kilichowakutanisha wadau wa sekta ya Usafirishaji Kanda ya kaskazin  amesema kuwa lengo la kikao kazi hicho ni   kuchochea maendeleo ya usafiri ndani ya mikoa na Taifa kwa ujumla . Aidha  kikao hicho kimekuja  kufuatia  ombi lililotolewa na wadau hao wa Usafirishaji kwa mkurugenzi mkuu ili kusikiliza changamoto zinazowakabili kulingana na gharama za maisha kupanda. Mkurugenzi huyo alisema kuwa nauli hizo zimegawanyika katika viwango mbalimbali kulingana na umbali wa kilometa ambazo wananchi wanapaswa kuzingatia. Alisema kuwa serikali imejaribu kuangalia nauli Kwa upya kufuatia gharama za maisha kupanda ikiwemo vipuri vya magari  ili wamiliki nao waweze ku

CHUO CHA ESAMI CHAHITIMISHA WASOMI ZAIDI YA 200 KUTOKA NCHI MBALIMBALI BARANI AFRIKA.

Image
 Na Pendo Mkonyi, Arusha. Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki amewataka  wataalamu wanaomaliza fani mbalimbali kujiajiri ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa   Ajira nchini. Pichani ni Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki Peter Mathuki. Akizungumza katika Mahafali ya 21 ya chuo cha Esami Kilichopo jijini Arusha  Katibu mkuu  huyo wa jumuiya ya Afrika mashariki Peter Mathuki amesema Kama wataalamu hao wamemaliza elimu za usimamizi , utawala na sera, Biashara,rasilimali watu,uongozi na nyingine lukuki ,wanafursa zakupata nafasi katika mabara mengine kutokana na uhaba wa Ajira. Alisema kuwa chuo hicho cha Esami ni chuo cha  muda mrefu na kilianzishwa wakati jumuiya ya afrika mashariki inaanza na Sasa chuo hicho kimekuwa  kwani Kwa sasa  hakihusishi  wanafunzi kutoka jumuiya ya afrika mashariki  pekee  Bali Barani  afrika. Alisema kuwa anapongeza chuo hicho na uongozi Kwa ujumla kwa jitihada hizo nzuri,ambapo aliwahusia vijana kutokwenda kuweka vyeti vyao ndani Bali wak

AFISA ELIMU MKOA WA ARUSHA BWANA ABEL NTUPWA AWATAKA WAZAZI KUJIPANGA KUWAPELEKA WATOTO ELIMU YA SEKONDARI KUTOKANA NA MKOA WA ARUSHA KUFAULISHA KWA WINGI

Image
Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Bwana Abel Ntupwa amesema  kuwa mkoa wa Arusha umepokea matokeo  ya wanafunzi Takribani 54,357 waliokuwa  wamesajiliwa ambapo wanafunzi waliofanya mitihani ni wanafunzi wapatao 53,341 sawa na asilimia 98% Pichani ni Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Bwana Abel Ntupwa. Kutokana na sababu mbalimbali wapo  wanafunzi wengine ambao  hawakuweza kufanya mtihani ambao ni sawa na  asilimia 2% lakini niseme  hapa Kuna maboresho makubwa sana kwani huko nyuma wanafunzi mpaka asilimia 12%walikuwa hawafanyi mtihani. Alisema kuwa kati ya wanafunzi 53341 wanafunzi waliofaulu na wenye sifa ya kuingia kidato Cha kwanza ni 45685 Ufaulu huo ni sawa na asilimia 85.64 ambapo kama mkoa wamepiga hatua moja kwenda mbele kwani ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 1.66  ukilinganisha na matokeo ya mwaka Jana ya asilimia 83.3. Ntupwa alisema kuwa halmashauri zimendelea kufanya vizuri sana kwani halmashauri ya jiji la Arusha imefaulisha Kwa asilimia 98.99 ambao ni ufaulu mkubwa sana ambapo ingedh

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA YA MSINGI TUMAIN JUNIOR YA KARATU YAFAULISHA KWA DARAJA A .

Image
 Na Pendo Mkonyi, Karatu. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi ya Tumaini Junior Modest Bayo amesema kuwa wanafunzi wote waliofanya mtihani wa Darasa la 7. Wamefaulu Kwa kiwango Cha juu yaani Daraja A. Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasis za elimu Tumaini Bwana Modest Bayo. Modest amesema kuwa ufaulu umefanyika Kwa asilimia 100 kufuatia kuwa na waalimu mahiri shuleni hapo na wanafunzi wenye utii na nidhamu njema.ambapo shukrani Zina muendea mkuu wa shule na timu yake. Alisema kuwa matokeo hayo si ya kushangaza kwani Kila mwaka shule ya Tumaini imekuwa ikifanya vizuri tangu shule hiyo kuanza kutoa elimu ya Darasa la 7 Kadhalika mkurugenzi huyo amesema kuwa shule ya Tumaini Junior ni sehemu sahihi ya kuwaandikisha watoto  ili kupata elimu Bora. Akizungumzia mpango wa kufungua shule mpya ya Tumain Tx pre & primary  school iliyopo njia panda kilometa 8 kutoka Karatu mjini itafunguliwa hivi karibuni lengo ni kuen

SHULE ST CATHERINE YAFAULISHA WANAFUNZI WOTE 20 KWA ALAMA A

Image
  Na Pendo Mkonyi,Karatu Shule binafsi ya mchepuo wa kiingereza ya awali na  msingi ya st Catherine yakiri kufaulisha wanafunzi wote 20. Hayo yamesemwa na mtaaluma mwandamizi wa shule ya  st Catherine Bwana  Ezekiel Kalalu  na kusema kutokana na matokeo yaliyotangazwa na Baraza la mitihani yamechangiwa na waalimu ambao wamekuwa wakijitoa Kwa moyo wa dhati. Pichani ni Ezekiel Kalalu mtaaluma mwandamizi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi st Catherine  Alisema kuwa Kila mwanafunzi amekuwa na utamaduni wa kuwafanya wanafunzi wao kujipatia alama A. Alisema kuwa Siri ya kufika hapo ni mkakati waliojiwekea  ikiwemo kufanya maandalizi Kwa kuwaandaa wanafunzi  ipasavyo ikiwemo kushiriki mitihani ya ujirani mwema, na waalimu kupewa mazingira mazuri ya kufundishia. Alisema kuwa shule ya st Catherine siyo mara ya kwanza kufanya vizuri ni kawaida Yao na utamaduni wao kwani Kwa  mwaka Jana walishika nafasi ya 3 kiwilaya na darasa la 4 walishika nafasi ya 1 kiwilaya. Kutokana juhudi

OOLA ACADEMY YA MTO WA MBU YAFAULISHA TENA WANAFUNZI WOTE

Image
 Na Pendo Mkonyi Mto wa Mbu. Mkuu wa shule ya awali na  msing Oola Academy Bwana Mkenea Legishe amesema kuwa shule hiyo imefanikiwa tena  kufuatia kufaulisha wanafunzi wote wa darasa la 7 na ijulikane kuwa shule hiyo imeendelea kufaulisha Kwa miaka 6 mfulilizo  na kuwashangaza wakazi wa mto wa mbu. Pichani ni mkuu wa shule ya awali na msingi Oola Academy. Alisema kuwa mnamo mwaka 2018 darasa la 7 walishika nafasi ya 3 kiwilaya na mwaka 2019 walishika nafasi ya 2 na kadiri miaka ilivyozidi kusonga ufaulu wa shule uliendelea kuwashangaza wananchi kutokana na ufaulu wa hali ya juu. Alisema kuwa mwaka huu 2023 wanafunzi wamefaulu Kwa alama A ambapo wanamshukuru Mungu na timu ya Oola Academy Kwa kufanikisha zoezi Hilo kwani wanafunzi wamefanya vizuri na kama ilivyo ada Somo la kiingereza wanafunzi wamepata Alama A ya 49 kiswahili wamepata A ya 46 somo la sayansi wamepata A ya 42 na hesabu wamepata A ya 42 ambapo Kwa tahimini hizo inaonesha wanafunzi wanaofaulu vizuri Kwa  viwango vya serika

SHULE YA THE VOICE YATAJWA KUWA KINARA WA MAADILI KUFUATIA WANAFUNZI WAKE KUWA KIELELEZO MKOANI ARUSHA

Image
 Na Pendo Mkonyi, Arusha Afisa elimu  mkoa wa Arusha Abel Ntupwa akiri kufurahishwa na utendaji kazi wa mmiliki wa shule ya The Voice kufuatia kupenda kuwafundisha wanafunzi ipasavyo na kuwainua wanafunzi kimaadili ya kumhofu Mungu. Pichani ni Afisa Elimu Mkoa Bwana Abeli Ntupwa wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 10 ya shule ya sekondari ya The voice. Ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 10 ya kidato Cha 4 ya shule ya sekondari ya The Voice iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha. Afisa elimu huyo amesema kuwa Maadili mema Kwa mwanafunzi ni Nyenzo kubwa katika maisha ya mwanafunzi ambapo amesisitiza zaidi shule hiyo pia kuzidi  kuboresha maendeleo kitaaluma. Aidha amesema kuwa kutokana na taarifa iliyosomwa na Wahitimu shule ijitahidi kufuta   daraja la tatu kwani kamwe halijamfurahisha na kiwango Cha ufaulu   hivyo mwakani waongeze juhudi ili kufuata daraja la tatu ili wazidi kuwa kinara. Kwani shule hiyo ni shule yenye upako namna  haistahili kur

SHULE YA MSINGI YA MCHEPUO WA KIINGEREZA YA SOCRATES JIJINI ARUSHA YAZIDI KUNOA VIPAJI VYA WATOTO

Image
  Na Pendo Mkonyi,Arusha. Shule ya  msingi ya mchepuo wa kiingereza ya Socrates imekiri kuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 4 kufuatia kufanya vizuri kitaaluma katika jiji la Arusha  Pichani ni Wahitimu wa darasa la 7 shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi ya Socrates ya jijini Arusha  Hayo yamesemwa na Wycliffe Rioba mkuu wa shule hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Mahafali ya kwanza yaliyofanyika shuleni hapo. Pichani ni mkuu wa shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi ya Socrates Bwana  Wycliffe Rioba. Alisema kuwa shule hiyo imefanikiwa kuinua vipaji vya wanafunzi ipasavyo kwani katika shule hiyo Kuna wanafunzi waimbaji,wachezaji wa muziki,wachoraji, na wengine wengi ambapo wanazidi kujengewa uwezo na waalimu mahiri shuleni hapo  Kwa kukuza vipaji vyao. Alisema kuwa vipaji vya watoto ni ajira ikiwa wazazi na walezi watavitambua na kuendeleza Kwa kuwasaidia watoto wao kuwapeleka katika shule za vipaji na mahiri kama i

WAZAZI NCHINI WAASWA KUWA MAKINI NA SIMU JANJA NA TV KWANI NI CHANZO KIKUBWA CHA UHARIBIFU WA MAADILI KWA WATOTO

Image
 Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu. Akizungumza katika Mahafali ya 16  Ya shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi  ya Mwalimu Anna Afisa Kilimo mstaafu Bwana John  Huba amewataka wazazi kuchukua tahadhari kwani kupitia Mitandao hiyo ya kijamii maisha ya watoto yapo hatarini kuangamizwa. Pichani Afisa Kilimo mstaafu Bwana John Huba mgeni rasmi katika Mahafali ya 16 ya shule ya awali ya shule ya Awali na Msingi  Mwalimu Anna. Aidha Mstaafu huyo alisema kuwa  kama wazazi hawatakuwa  karibu na watoto wao Kwa kuwalea ipasavyo  ipo hatari ya kuwapoteza Kwa kutokana na kuiga mambo yasiyofaa katika Mitandao na televisheni ikiwemo mienendo isiyopendeza kwani vipo vitu ambavyo haviendani na umri wao. Alisema kuwa  usalama wa watoto upo mikononi mwa wazazi wao kwani  wao ndio  wenye jukumu la kuwalinda watoto Kwa kusaidiana na waalimu shuleni Kwa kufuatilia maendeleo  ya watoto wao ipasavyo Alisema kuwa wako maadui wakuu 2 katika maisha ya mtoto kwa sasa Adui wa kwanza ni teknolojia  na Adui w