CHUO CHA ESAMI CHAHITIMISHA WASOMI ZAIDI YA 200 KUTOKA NCHI MBALIMBALI BARANI AFRIKA.
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki amewataka wataalamu wanaomaliza fani mbalimbali kujiajiri ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa Ajira nchini.
Pichani ni Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki Peter Mathuki.
Akizungumza katika Mahafali ya 21 ya chuo cha Esami Kilichopo jijini Arusha Katibu mkuu huyo wa jumuiya ya Afrika mashariki Peter Mathuki amesema Kama wataalamu hao wamemaliza elimu za usimamizi , utawala na sera, Biashara,rasilimali watu,uongozi na nyingine lukuki ,wanafursa zakupata nafasi katika mabara mengine kutokana na uhaba wa Ajira.
Alisema kuwa chuo hicho cha Esami ni chuo cha muda mrefu na kilianzishwa wakati jumuiya ya afrika mashariki inaanza na Sasa chuo hicho kimekuwa kwani Kwa sasa hakihusishi wanafunzi kutoka jumuiya ya afrika mashariki pekee Bali Barani afrika.
Alisema kuwa anapongeza chuo hicho na uongozi Kwa ujumla kwa jitihada hizo nzuri,ambapo aliwahusia vijana kutokwenda kuweka vyeti vyao ndani Bali wakaviyumie na kujitahidi kujishughulisha na kazi maeneo mbalimbali hususani katika dunia hii iliyojaa teknolojia.
Kwa upande wake katibu mkuu ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala Bora Juma Mkomi amesema licha ya chuo kutoa wataalamu mbalimbali katika utumishi wa umma , chuo kimeweza kuzifikia nchi za kusini mwa Afrika na hiyo ni kutokana na uwepo wa idadi ya Taasisi zakimataifa zinazohudumu hapa nchini.
Pichani ni katibu mkuu ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala Bora Juma Mkomi.
alisema kuwa chuo hicho kinawapa fursa watumishi wa umma kujengewa uwezo na kujipatia ubora na uwepo wao unaongeza idadi ya Taasis za kimataifa kwani mpaka nchi za kusini mwa afrika wanaofika kujifunza katika chuo hicho.
alisema kuwa chuo hicho kinawapa fursa watumishi wa umma kujengewa uwezo na kujipatia ubora na uwepo wao unaongeza idadi ya Taasis za kimataifa kwani mpaka nchi za kusini mwa afrika wanaofika kujifunza katika chuo hicho.
Alitoa wito Kwa watanzania kufika kujifunza kufuatia kutoa mafunzo mazuri hivyo watazame fursa iliyopo katika chuo hicho cha Essami kwani kinawasaidia kusimamia shughuli zao binafsi
Mkuu wa chuo hicho cha Esami Martin Lwanga amesema jumla ya wahitimu 204 kutoka nchi 28 za Afrika wametunikiwa vyeti vya kufuzu viwango vya taaluma na fani walizosomea zinazotolewa na chuo hicho.
Naye mhitimu wa shahada ya pili ya miradi Sophia Katumbi amesema kama wasimamizi wa miradi itawawezesha kuwaelimisha wananchi na kubuni miradi yenye manufaa kwa jamii..
Comments
Post a Comment