SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA YA MSINGI TUMAIN JUNIOR YA KARATU YAFAULISHA KWA DARAJA A .

 Na Pendo Mkonyi, Karatu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi ya Tumaini Junior Modest Bayo amesema kuwa wanafunzi wote waliofanya mtihani wa Darasa la 7. Wamefaulu Kwa kiwango Cha juu yaani Daraja A.Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasis za elimu Tumaini Bwana Modest Bayo.


Modest amesema kuwa ufaulu umefanyika Kwa asilimia 100 kufuatia kuwa na waalimu mahiri shuleni hapo na wanafunzi wenye utii na nidhamu njema.ambapo shukrani Zina muendea mkuu wa shule na timu yake.

Alisema kuwa matokeo hayo si ya kushangaza kwani Kila mwaka shule ya Tumaini imekuwa ikifanya vizuri tangu shule hiyo kuanza kutoa elimu ya Darasa la 7

Kadhalika mkurugenzi huyo amesema kuwa shule ya Tumaini Junior ni sehemu sahihi ya kuwaandikisha watoto  ili kupata elimu Bora.
Akizungumzia mpango wa kufungua shule mpya ya Tumain Tx pre & primary  school iliyopo njia panda kilometa 8 kutoka Karatu mjini itafunguliwa hivi karibuni lengo ni kuendelea kutoa elimu na kukomboa watoto wa kitanzania.

Sanjari na hayo uongozi wa shule za Tumaini tayari umeanzisha shule ya sekondari ya mchepuo  wa sayansi  na Biashara eneo la Makuyuni mkoani Arusha.

Alisema kuwa  shule ya Tumaini ni shule Bweni  na shule ambayo inafanya vizuri sana na inafundisha masomo ya kawaida na masomo ya ziada ambapo aliwakaribisha wazazi kuwaandikisha kidato Cha 5 Kwa wingi.
Alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wazazi kuwaandikisha kwa wingi katika shule hiyo kwani ina mazingira Mazuri lakini pia shule za Tumaini zinajali afya za watoto Kwa kuwapa lishe kamili ambapo pia shule inawajali wanafunzi Kwa kupewa usafiri kufuatia shule kuwa na magari ya kutosha.

Alisema maisha ya kiroho yanapewa kipaumbele kwani upo uhuru wa kuabudu Kwa mwanafunzi kulingana na Imani yake japokuwa upo wakati hufundishwa mambo ya kiroho Kwa pamoja wakiamini Mungu ni mmoja anayeabudiwa.



Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.