SHULE YA THE VOICE YATAJWA KUWA KINARA WA MAADILI KUFUATIA WANAFUNZI WAKE KUWA KIELELEZO MKOANI ARUSHA
Na Pendo Mkonyi, Arusha
Afisa elimu mkoa wa Arusha Abel Ntupwa akiri kufurahishwa na utendaji kazi wa mmiliki wa shule ya The Voice kufuatia kupenda kuwafundisha wanafunzi ipasavyo na kuwainua wanafunzi kimaadili ya kumhofu Mungu.
Pichani ni Afisa Elimu Mkoa Bwana Abeli Ntupwa wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 10 ya shule ya sekondari ya The voice.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 10 ya kidato Cha 4 ya shule ya sekondari ya The Voice iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Afisa elimu huyo amesema kuwa Maadili mema Kwa mwanafunzi ni Nyenzo kubwa katika maisha ya mwanafunzi ambapo amesisitiza zaidi shule hiyo pia kuzidi kuboresha maendeleo kitaaluma.
Aidha amesema kuwa kutokana na taarifa iliyosomwa na Wahitimu shule ijitahidi kufuta daraja la tatu kwani kamwe halijamfurahisha na kiwango Cha ufaulu hivyo mwakani waongeze juhudi ili kufuata daraja la tatu ili wazidi kuwa kinara.
Kwani shule hiyo ni shule yenye upako namna haistahili kurudi nyuma kufuatia wanafunzi kuwa shuleni kipindi chote kwani wanafunzi Wana wasaa mzuri wa kujifunza tofauti na wanafunzi ambao wanaotoka umbali mrefu.
Alimtaka mkuu wa shule kupokea maagizo na kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kwa kiwango Cha Gpa1.7 kwani shule hii ni matawi ya juu kuliko shule zingine.
Aidha Afisa elimu huyo amewapongeza waalimu Kwa kuwalea watoto tangu wakiwa na umri wa miaka 4 Kwa juhudi hizo hususani katika kutoa elimu Kwa watoto.
Aliwapongeza waalimu Kwa namna ambavyo wanawaandaa wanafunzi kimaadili na kimalezi kwa ujumla kufuatia kuwasaidia watoto na ni Matarajio Yao kuwa wanafunzi watafaulu Kwa daraja la kwanza.
Alisema kuwa elimu ni safari ya maisha na tayari wanafunzi wamepata ufunguo na pasipoti ya kusafiria kwenye maisha yao ambapo aliwaasa Wahitimu wa darasa la 7 na wanafunzi wote Kwa ujumla kujitambua kuwa ninyi ni vijana na mna uwezo ikiwemo kuenenda sawa na maadili ya familia zenu na nchi ya Tanzania Kwa ujumla.
Alisema kuwa Taifa kuwa na vijana siyo suala la idadi tu Bali ubora Kwa vijana ndio unazingitiwa ukiwemo umahiri,ustahimilivu na udhubutu katika Kutenda jambo.
Kadhalika aliwataka wahitimu hao kuwa ni vijana wenye maamuzi sahihi ambayo hayatawaletea majutu pindi mtakapokuwa huko mitaani msikubali kurubuniwa na fedha za matajiri au watu muwakatae na kuwasikiliza wazazi wenu ili mzidi kufanikiwa.
Pia aliwataka kufikiria kabla ya Kutenda jambo lolote kwani hicho ndio kipimo cha akili Aliwataka kutumia changamoto kama fursa katika jamii iliyowazunguka
Na kuepuka matumizi mabaya ya mtandao ikiwemo kukesha Kwa Muda mrefu kwenye Mitandao kama vile Instagram, Facebook, Twitter na mingineyo Kwani huo unaweza kuwa uraibu.
Aliwahusia wazazi kuwa makini na watoto wao hususani kipindi hichi cha ongezeko kubwa la teknolojia Kwa kufuatilia mienendo Yao Kwa ukaribu ili kuwaponya.
Sanjari na hayo aliwaonya wanafunzi kuepuka uvivvu Bali washughulushwe katika majukumu mbalimbali ikiwemo kuwajibishwa pindi wanapokosea wasinyimwe kiboko ambapo aliwaonya Wahitimu kwenda kujihusisha na michezo mbalimbali kwani ipo michezo mingine yenye madhara katika maisha yao ukiwemo ushabiki uliopitiliza na usiokuwa na maana.
Aliwataka vijana kuwa watu wa kujenga hoja siyo viroja na endapo usipokubalika kaa Kwa kutulia na kujikubali na kuwa mzalendo Kwa kuepuka uhuni,udangaji,umalaya,na matumizi mabaya ya mtandao na kuwataka kujilinda na kujikinga na mambo mbalimbali ikiwemo kujitambua na kula vyakula vya asili wasizidishe chipsi yai na kiepe Kwa wingi.
Alisema kuwa magonjwa yapo kama vile ukimwi hivyo wajihadhari keaninugonjwa huo ni dhambi ya kupooza kwani utateseka na kujiondolea heshima maisha mwenu.
Eleweni wazazi wenu wamewasomesha Kwa gharama kubwa na uwekezaji mkubwa ndio waliofanywa hivyo msiende kuuharibu Kwa namna yeyote Ile Aliwataka kuthibitisha usomi wao katika jamii na familia Kwa kufanya mambo Kwa uharaka na usahihi wasikubali kuwa mzigo.
Pamoja na hayo aliwataka kujitolea maeneo mbalimbali na kufanya kazi pasipo kuchagua kama vile ufugaji,kilimo na kazi zinginezo ili kujipatia kipato ambapo Aliwataka wazazi kuendelea kuwajengea maarifa na ujuzi ikiwemo kuwafunza neno samahani pindi wanapokosea
Pia wazazi wawakumbushwa watoto kuwa Mungu yupo, serikali ipo na jamii ipo na wazazi mjitahidi kuwasimamia watoto wafanye kazi.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shule ya sekondari ya The voice Daniel Mpanduzi alisema kazi kubwa ni kuwapa wanafunzi sauti ya kujitegemea na kujiamini na kuwapa uwezo wa kujikubali ukiwemo uwezo darasani na maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa wanafunzi wengi hutiwa moyo na kuwawezesha na kuepuka kuwabagua wanafunzi licha yawengine kukataliwa maeneo ya shule kulingana na kiwango Cha elimu kuwa chini lakini wakiwa katika shule ya The voice hupewa kipaumbele zaidi .
Akizungumzia ongezeko la teknolojia Duniani mkurugenzi huyo alisema kwao ni fursa kwani wanafunzi wengi wameongezeka kimaarifa kufuatia kuwafundisha wanafunzi namna ya kutumia Mitandao Kwa faida katika kilimo na maeneo mengine.
Alisema kuwa wamekuwa wakisaidiwa wazazi kuwaelewa watoto wao zaidi pindi watoto wao wawapo shuleni pindi wanafunzi wanapofikia kufanya maamuzi wawe wakina nani hapo baadaye
Shule hiyo imekuwa msaada pia Kwa kusaidia watoto wanaotoka mazingira magumu ambapo wakati mwingine hujitoa kuwasaidia kuwapa elimu bure kama sehemu ya kuwatia moyo na kuwaonesha wanaweza na kuithibitishia jamii kuwa jamii ya walemavi nao wakisaidiwa wanaweza.
Hata hivyo Wahitimu wapatao 53 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya kidato Cha 4 katika Mahafali ya 10
Comments
Post a Comment