WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI INNOCENT BASHUNGWA AFUNGUA KONGAMANO LA 32 LA WAHANDISI JIJIJINI ARUSHA AMBAPO WAHANDISI 57

 Na Pendo Mkonyi,Arusha.

Waziri wa ujenzi na uchukuzi Innocent Bashungwa  wakati akizungumza katika kongamo Hilo amewataka wahandisi kutumia fursa ya kongamano Hilo  kujitathimini.

Baadhi ya wahandisi waliopatiwa kiapo katika kongamano la 32 la wahandisi 

Alisema kuwa serikali inatambua taasis ya wahandisi Tanzania katika kuendeleza mezania ya serikali ambapo aliitaka taasis kuhakikisha inajitangaza ili wahusika waone umuhimu wa kujiunga na taasis yao.

Alisema kuwa( IET)kuwa na umri wa miaka 48 bado idadi ya wanachama ni ndogo kwani mpaka Sasa wanachama wamekaribia zaidi ya wahandisi elfu 4.

Bashungwa alisema kuwa Taasisi hiyo inapaswa kutatua changamoto zinazoikabili taasis hiyo ikiwemo kuwa msitari wa mbele kuishauri nchi zaidi ya Taasis ya kitaaluma.

Aidha wahandisi wametakiwa kutumia nafasi zao ipasavyo Kwa kuwa Suluhisho Kwa maendeleo endelea kufuatia kuwepo Kwa teknolojia mbalimbali kwani serikali unatumika Tehama katika ufanisi wa mambo mbalimbali  ili kuleta majawabu ya hayo.

Alitoa wito Kwa Washiriki kushiriki katika maeneo mbalimbali be ya ujenzi na kuangalia namna ya kutatua changamoto zitokanazo na sekta ya ujenzi .

Mikakati inayopaswa kuangalia ni pamoja na kuwatumia wazee  ili kuwasaidia wahandisi wachanga waliokula viapo siku ya Leo.

Bashungwa alisema kuwa wizara ya ujenzi inavyo viapaumbele vingi ikiwemo  kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo nyakati za ujenzi wa barabara na Madaraja mbalimbali.
Aliwapa changamoto ya kujitathimini na kuhakikisha wanakuza taaluma hiyo ya uhandisi wasikubali kuwa kizuizi Kwa hali yeyote katika utendaji.

Aliwataka kukemea RUSHWA maeneo yao ya kazi ili kuondokana na changamoto maeneo ya kazi na badala yake wawe wazalendo katika nchi yao na ikiwezekana waripotiwe wahandisi ambao siyo waaminifu ili waweze kuwajibishwa na kuwa mfano Kwa wengine.

Naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi na uchukuzi Bwana  Ludovick Nduhiye  Kwa niaba ya katibu mkuu wizara ya ujenzi amesema kuwa kongamano hili ni jeshi kubwa katika nchi ya Tanzania ambapo wanajivunia kuwa na Jeshi la wahandisi.

Alisema kuwa Taasisi his za kitaaluma ndiu chanzo muhimu Cha matokeo ya utafiti hivyo vyama vya usajili na uhandishi na vyama vya ushirikiano vizidi kumshirikianan.

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amepongeza kongamano Hilo kufanyika jijini Arusha ambapo amewahakikishia usalama wanashiriki wote waliohudhuria katika kongamano Hilo.

Alitumia nafasi hiyo kuwaalika wananndisi kutembelea vivutio mbalimbali vya Kanda ya Kaskazini lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais za kuutangaza nichi ya Tanzania na vivutio vyake vya utalii duniani.

Wahandisi Wana wajibu wa kujenga ustawi wa jamii wa wanadamu ili kuleta maendeleo katika Taasis ya uhandisi.

Aliwataka kutumia Muda wao kumtafakari taaluma ya uhamdisi nchini Tanzania ambapo mpaka Sasa  ni zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa Kwa sekta hiyo.

Alisema tangu mwaka 1973 Tanzania imepiga hatua kubwa  sambamba na mafunzo ya miaka 59 ya yahusuyo teknolojia.

Kwa upande wake Rais wa Taasis ya wahandisi  Tanzania Dr Gemma Modu
Amesema kuwa uhandisi una mchango mkubwa katika nchi ambapo alisema kuwa pia hii nifursa kubwa Kwa ajili ya maendeleo
Pichani ni Raisi wa wa Taasis ya wahandisi  Tanzania Dr Gemma Modu

Aliwataka wahandisi kushukuru na kutoa pongezi Kwa ajili ya sererikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani fursa mbalimbali za kazi zinafunguka 

Alisema taasis ya uhandisi ipo bega Kwa bega katika kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini kwani Serena nyingi itaendelea pato la Taifa.

Alisema lengo la  taasis ya uhandisi Tanzania ni kuchukua jukumu Hilo pamoja na serikali ni katika kukuza Dani ya uhandisi syansi na teknolojia nchini ili kutangaza uhandisi
 
Alisema taasis inaendesha shughuli zake Kwa kufuata kanununi ikiwemo kutoa mafunzo ya Muda mfupi katika mikutano warsha ili kuwajengea uwezo

Taasis ya uhandisi(IET) ina malengo ya kufungua matawi nchini ili kuendeleza taasis ipasavyo ili iweze kushirikiana na Mamlaka zingine 

Kadhalika Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA ) kwa namna inavyotekeleza majukumu yake ya kuzifungua barabara nchini.

“TARURA mnaupiga mwingi kwenye Ujenzi wa madaraja na barabara za mawe,mfikishieni salamu zangu Waziri wa OR-TAMISEMI,Mtendaji Mkuu pamoja na watumishi wote wa TARURA.

Pichani ni waziri wa ujenzi na uchukuzi Innocent Bashungwa akimpa cheti Cha pongezi Mhandisi Mshauri Phares Ngereja kutoka makao makuu dodoma ya Taasis ya Tarura.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo tarehe 30 Novemba, 2023 alipotembelea banda la maonesho la TARURA kwenye Kongamano la Kitaifa la 32 la Taasisi ya Wahandisi 

Akizungumza na waandishi wa habari mhandisi   Mshauri Ngereja kutoka makao makuu dodoma amesema kuwa hivi Sasa wanatumia teknolojia ya ujenzi wa mawe katika ujenzi wa barabara na Madaraja.

Alisema kuwa Tarura Kwa kuanzia mpaka Sasa wamefanikiwa kujenga Madaraja 212 yenye gharama ya shilingi billion 8.2 ambapo kama hayo Madaraja yngejengwa kupitia zege yangetumia 36.

Hata hivyo mwaka huu Tarura imejipanga kujenga madaraja 189 nchi nzima katika mikoa yote 26 ambapo mpaka Sasa mwaka huu fedha yapo madaraja  56 yanaendelea na ujenzi ambapo mawe yote hupimwa mp 25 na zaidi Kwa upande wa matofali ni mpa 8 Kwa ajili ya madaraja


Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.