WAZAZI NCHINI WAASWA KUWA MAKINI NA SIMU JANJA NA TV KWANI NI CHANZO KIKUBWA CHA UHARIBIFU WA MAADILI KWA WATOTO

 Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu.

Akizungumza katika Mahafali ya 16 Ya shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi  ya Mwalimu Anna Afisa Kilimo mstaafu Bwana John  Huba amewataka wazazi kuchukua tahadhari kwani kupitia Mitandao hiyo ya kijamii maisha ya watoto yapo hatarini kuangamizwa.

Pichani Afisa Kilimo mstaafu Bwana John Huba mgeni rasmi katika Mahafali ya 16 ya shule ya awali ya shule ya Awali na Msingi  Mwalimu Anna.

Aidha Mstaafu huyo alisema kuwa  kama wazazi hawatakuwa  karibu na watoto wao Kwa kuwalea ipasavyo  ipo hatari ya kuwapoteza Kwa kutokana na kuiga mambo yasiyofaa katika Mitandao na televisheni ikiwemo mienendo isiyopendeza kwani vipo vitu ambavyo haviendani na umri wao.

Alisema kuwa  usalama wa watoto upo mikononi mwa wazazi wao kwani  wao ndio  wenye jukumu la kuwalinda watoto Kwa kusaidiana na waalimu shuleni Kwa kufuatilia maendeleo  ya watoto wao ipasavyo

Alisema kuwa wako maadui wakuu 2 katika maisha ya mtoto kwa sasa Adui wa kwanza ni teknolojia  na Adui wa pili ni ndugu jamaa marafiki wanaofika katika familia kwani baadhi yao wamekosa utu na kugeuka wakatili  Kwa watoto ikiwemo kuwafanyia vitendo vya ubakaji, ulawiti  na ushoga na vingine vinavyofanana na hivyo.
Aidha Mstaafu  huyo amewataka viongozi wa kimila, viongozi wa kidini kuendelea kukemea vitendo viovu vinavyofanywa na jamii na kusisitiza maadili katika jamii zaidi ili kuponya kizazi kilichopo na Cha baadaye 

Akizungumzia Taasis hiyo ya elimu ya Mwalimu Anna  amewataka kujitangaza Kwa watu ili kufahamika zaidi kufuatia elimu nzuri inayotolewa hapo ambapo aliwataka wazazi kutumia fursa iliyopo kuwaandikisha watoto shule wenye umri mdogo kwenda kulelewa na kunufaika na mango wa elimu.
Naye mkuu msaidizi wa shule ya msingi Mwalimu Anna  Bi Sabina Michael wakati akisoma risala yake Kwa mgeni Rasmi alisema kuwa katika Mahafali hayo ya 16 wanafunzi wapatao 56 wamehitimu elimu ya msingi wakiwemo wasichana 31 na wavulana 25.
Pichani ni Mkuu wa shule msaidizi wa shule ya awali na msingi ya Mwalimu Anna Bi Sabina Michael akisoma risala Kwa mgeni rasmi

Alisema kuwa shule ya awali na msingi Mwalimu Anna ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2020 mwezi wa 9 na kufunguliwa tarehe 10/10/2021 na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Monduli Bwana Edward Josam Balele.

Shule ya awali ilianza ikiwa na jumla ya wanafunzi 84 wakiwemo wasichana 38 na wavulana 46,walimu 6 na mtunza mazingira 1 ambapo mpaka Sasa ina jumla ya wanafunzi 175.

Pia alisema kuwa  kutokana.nanusimamizi Bora na bidii kubwa waliyo nayo  viongozi na watumishi wa shule hiyo kipo kitengo kipya Sasa Cha day care ambacho kinapokea watoto wa miaka 2 na hii imekuja mara baada ya wadau wengi wa elimu kuwa na uhitaji.

Taaluma katika shule hiyo imefanikiwa  kufanya vizuri Kwa madarasa ya awali na msingi ambapo shule imefanikiwa kuondoa wastani wa  Alama B kwenda wastani wa  Alama A  Kwa madarasa yote ya awali 
Kutokana na uwepo wa  mtaala mpya watoto wanatumia Muda mwingi kujifunza  Kwa vitendo shuleni ili kuhakikisha hawapotezi kitu chochote katika masomo.

Matarajio makubwa ya shule Mwalimu Anna ni mtoto atakayepitia hapo kwenda kufanikiwa kitaaluma Kwa kufanya vizuri katika kuongea lugha ya kiingereza Kwa ufasaha kuandika vizuri kusoma na kuhesabu ikiwemo ujuzi wa kujisisamia yeye mwenyewe.

Mafanikio katika shule ya Mwalimu Anna ni pamoja na kufanikiwa kununua vifaa vya kutosha Kwa ajili ya michezo mbalimbali ya watoto,ujenzi wa vyumba 2 vikubwa vya madarasa,ofisi moja,vyoo vya wanafunzi hii ni kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi,

Kadhalika Kwa kipindi hiki Cha mwaka 2023 shule imefanikiwa kumalizika ujenzi wa jilo kipya la gesi la kisasa ambalo linasaidia kupika Kwa wakati na kupunguza adha ya uharibifu wa mazingira unaokumba nchi  na Dunia Kwa ujumla

Pichani ni Mkuu wa shule ya Awali(chekechea )ya Mwalimu Anna Bi Mary Moshi.

Mkuu  wa shule ya Awali  Bi Mary Moshi amewakaribisha wazazi kwenda kuwaandikisha watoto Kwa wingi katika shule hiyo kufuatia shule hiyo kusajiliwa na wizara na kufahamika lakini pia ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika mkoa wa Arusha na Tanzania Kwa ujumla

Alisema kuwa nafasi za watoto zipo wazazi hivyo wazazi na walezi wote wanakaribishwa kuwapeleka watoto katika shule hiyo k Ani ni shule inayozingatia maadili bora na kuwalea watoto kiroho 

Mkuu wa shule ya Awali ya  Mwalimu Anna Zenice Albert  kwa niaba ya mkurugenzi wa shule hiyo wakati akitoa shukrani za dhati katika Mahafali hayo 

Amesema  kuwa Kuna changamoto ya mahudhurio  kutoka Kwa wanafunzi ambapo amewaomba wazazi wajitahidi kuwalipia watoto usafiri ili wawahi masomo shuleni  kwa wakati.
Pichani ni Mkuu wa shule ya Msingi ya Mwalimu Anna Bi Zenice Albert.

Sanjari na hilo amewaomba wazazi kulipa ada kwa wakati kwani ndio inawawezesha waalimu kulipwa mishahara ya waalimu na kukarabati miundo mbinu ya shule pindi inapohitajika

Aliwatia moyo wazazi na kusema kuwa kweli wazazi mnaweza Wala msirudi nyuma dhidi ya watoto wenu jitahidini kuendelea kufuatilia maendeleo ya watoto ili waweze kukua vema kimaadili na kuipaisha shule ya Mwalimu Anna kitaaluma.



Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.