SHULE ST CATHERINE YAFAULISHA WANAFUNZI WOTE 20 KWA ALAMA A
Na Pendo Mkonyi,Karatu
Shule binafsi ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi ya st Catherine yakiri kufaulisha wanafunzi wote 20.
Hayo yamesemwa na mtaaluma mwandamizi wa shule ya st Catherine Bwana Ezekiel Kalalu na kusema kutokana na matokeo yaliyotangazwa na Baraza la mitihani yamechangiwa na waalimu ambao wamekuwa wakijitoa Kwa moyo wa dhati.
Pichani ni Ezekiel Kalalu mtaaluma mwandamizi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi st Catherine
Alisema kuwa Kila mwanafunzi amekuwa na utamaduni wa kuwafanya wanafunzi wao kujipatia alama A.
Alisema kuwa Siri ya kufika hapo ni mkakati waliojiwekea ikiwemo kufanya maandalizi Kwa kuwaandaa wanafunzi ipasavyo ikiwemo kushiriki mitihani ya ujirani mwema, na waalimu kupewa mazingira mazuri ya kufundishia.
Alisema kuwa shule ya st Catherine siyo mara ya kwanza kufanya vizuri ni kawaida Yao na utamaduni wao kwani Kwa mwaka Jana walishika nafasi ya 3 kiwilaya na darasa la 4 walishika nafasi ya 1 kiwilaya.
Kutokana juhudi hizo shule ilipatiwa vikombe vya pongezi kwani shule hiyo imethibitidha kuwa na utendaji mkubwa wa kazi kwani waalimu wamekuwa marafiki wazuri Kwa watoto na kuwaonesha upendo huo ndio kiwango Cha elimu kinazidi kupanda.
Hata hivyo shule hiyo tayari imetangaza Dawati la udahili Kwa wanafunzi wa elimu ya awali na nafasi za kuhamia ziko wazi Sasa ili kumuwezesha mwanafunzi wa kitanzania kujiunga na shule hiyo kwani mazingira ya shule ni rafiki na yanamuwezesha mtoto kujipatia elimu Bora.
Comments
Post a Comment