Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Taasis ya kanisa la Waadventista wasabato ulimwenguni itwayo Geo science research institute inayojishughulisha na kufanya utafiti unaotoa ujuzi jinsi ya Dunia ilivyotokea imetembelea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini lengo likiwa ni kufanya utafiti.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo naibu makamu mkuu wa chuo kikuu Cha Arusha Profesa Pearson Mnkeni Kwa niaba ya makamu mkuu wa chuo kikuu cha arusha Profesa Patrick Manu alisema kuwa wamekuwa na wageni kutoka katika taasis ya wasabato ambapo wamefanikiwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii na kujifunza kwa mambo mengi yahusuyo jiolojia.Pichani ni naibu makamu mkuu wa chuo kikuu Cha Arusha Profesa Pearson Mnkeni
Aidha Wadventista wasabato duniani wanaamini duniani imeumbwa na Mungu Kwa kipindi Cha siku 6 na siku ya 7 Mungu akapumzuka ikawa ni sabato ambapo zipo nadharia nyingi zinasema kuwa mwanadamu alibuka tu kutoka kwenye chembechembe vidogo ambapo taasis ni kufanya utafiti ambao unatoa ushahidi kwamba Dunia iliumbwa na Mungu.
Maeneo waliyotembelea wageni hao ni pamoja na ziwa Victoria huko mwanza, kuona miamba iliyopo ambapo walipata nafasi ya kujifunza wakiwemo waalimu wa shule za sekondari ambao wamejionee ili watakapokuwa na wanafunzi shuleni waweze kuwapa elimu sahihi kuhusu umbaji
Kadhalika Wageni hao walifanikiwa kutembelea hifadhi ya Taifa ya ngorongoro,ziwa manyara ambapo walifika Hadi bonde la ufa, Serengeti,na kujionea mambo mbalimbali ambapo waliopatiwa maelezo na wataalam kulingana na maeneo husika.
Alisema kuwa Taasis hiyo ni taasis pekee katika kanisa la wasabato duniani ambayo hufanya tafiti kulingana na mtazamo uliofanywa na Mungu ambapo hakuna kituo Cha Kikiristo duniani ambayo ina kituo kama hicho kinachofanya kazi kama hiyo.
Hata hivyo ziara hiyo ni mara ya kwanza kufanyika barani afrika ambapo wengi wa wahudhuriaji wa wageni katika maeneo hayo ni walimu wa sekondari kutoka kanda ya mashariki , sambamba na wageni kutoka nchi zingine kama vile Kenya ,Uganda Ethiopia, Sudani ya kusini, Burundi, Rwanda na Congo.
Comments
Post a Comment