OOLA ACADEMY YA MTO WA MBU YAFAULISHA TENA WANAFUNZI WOTE
Na Pendo Mkonyi Mto wa Mbu.
Mkuu wa shule ya awali na msing Oola Academy Bwana Mkenea Legishe amesema kuwa shule hiyo imefanikiwa tena kufuatia kufaulisha wanafunzi wote wa darasa la 7 na ijulikane kuwa shule hiyo imeendelea kufaulisha Kwa miaka 6 mfulilizo na kuwashangaza wakazi wa mto wa mbu.Pichani ni mkuu wa shule ya awali na msingi Oola Academy.
Alisema kuwa mnamo mwaka 2018 darasa la 7 walishika nafasi ya 3 kiwilaya na mwaka 2019 walishika nafasi ya 2 na kadiri miaka ilivyozidi kusonga ufaulu wa shule uliendelea kuwashangaza wananchi kutokana na ufaulu wa hali ya juu.
Alisema kuwa mwaka huu 2023 wanafunzi wamefaulu Kwa alama A ambapo wanamshukuru Mungu na timu ya Oola Academy Kwa kufanikisha zoezi Hilo kwani wanafunzi wamefanya vizuri na kama ilivyo ada
Somo la kiingereza wanafunzi wamepata Alama A ya 49 kiswahili wamepata A ya 46 somo la sayansi wamepata A ya 42 na hesabu wamepata A ya 42 ambapo Kwa tahimini hizo inaonesha wanafunzi wanaofaulu vizuri Kwa viwango vya serikali.
Mwanafunzi Sinyati Emanuel qmeibuka kidedea Kwa kushika nafasi ya kwanza Kwa kupata alama A akufuatiwa na Jackiline Kwa kupata alama A akufuatiwa na Ather junior na Elisha hivyo wanafunzi hao ni Bora kufuatia kuingia kwenye kinyanganyiro Cha alama za serikali.
Alisema kuwa kulingana na alama za serikali inaonesha shule ya msingi na awali Oola imeingia kwenye Madaraja yanayohutajika.
Akizungumzia somo la sayansi na hisabati amesema kuwa waalimu wamekuwa walitumia mbinu mbalimbali ikiwemo mbinu ya upendo ambapo mwanafunzi anavutiwa ba kuweka juhudi kwenye nasomo hayo.
Kadhalika wanafunzi hukaa n waalimu kama marafiki hawatumii kiboko kufundishia Bali upendo Kwa wanafunzi zaidi na waalimu hujitoa Kwa kuwasaidia wanafunzi na kutokubali kushuka Kwa wanafunzi.
Akizungumzia upande wa somo la sayansi wanafunzi wote wanafundishwa Kwa vitendo ndio maana somo Hilo hufaulu Kwa kiwango Cha serikali kinachohitajika.
Alisema kuwa wanafunzi wanaoteuliwa kujiunga na elimu ya serikali hupangwa shule husika na Oola hawajawahi kuteuliwa Kwa mara ya pili hivyo wazazi waingie mtandaoni kujionea matokeo na wafanye maamuzi ya kuwaandikisha wanafunzi kwenye shule hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shule huyo Bwana Duncan Samweli alitumia nafasi hiyo kuwashukuru waalimu na warenda kazi wote wa shule Kwa kufanikisha zoezi Hilo ambapo Muda siyo mrefu wataanda ghafla ya kupongeza shule nzima Kwa kufanya kazi kubwa
Alisema kuwa hata dereva na mpishi shuleni wamechangia mafanikio ya shule ya wanafunzi hivyo pongezi zinawahusu .
Alisema kuwa wanashukuru wazazi Kwa kushirikiana vema pindi wanapohitajika shuleni ambapo anewaonba kuendelea na moyo huo huo wa usikivu.
Comments
Post a Comment