ONGEZEKO LA NAULI ZA DALADALA NA MAGARI YA MASAFA MAKUBWA KUPANDA DESEMBA 8
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Mamlaka ya usafiri Ardhini Latra imetangaza ongezeko la nauli viwango vya mabasi na daladala hapa Nchini mara baada ya siku 14 kuisha kuanzia leoPichani ni Mkurugenzi mkuu wa Latra Taifa Habibu Juma Suluo
Akizungumza katika Kikao kizazi hicho Mkurugenzi mkuu wa Latra Taifa Habibu Juma Suluo katika kikao kilichowakutanisha wadau wa sekta ya Usafirishaji Kanda ya kaskazin amesema kuwa lengo la kikao kazi hicho ni kuchochea maendeleo ya usafiri ndani ya mikoa na Taifa kwa ujumla .Aidha kikao hicho kimekuja kufuatia ombi lililotolewa na wadau hao wa Usafirishaji kwa mkurugenzi mkuu ili kusikiliza changamoto zinazowakabili kulingana na gharama za maisha kupanda.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa nauli hizo zimegawanyika katika viwango mbalimbali kulingana na umbali wa kilometa ambazo wananchi wanapaswa kuzingatia.
Alisema kuwa serikali imejaribu kuangalia nauli Kwa upya kufuatia gharama za maisha kupanda ikiwemo vipuri vya magari ili wamiliki nao waweze kupata kidogo hata kufanyia marekebisho magari Yao ikiwemo serikali kujipatia mapato lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais.
Katibu mkuu wa usafirishaji kanda ya kaskazin Arusha , Kilimanjaro na Manyara (Akiboa) Lokeni Adolfu Masawe, wameridhia kiwango hicho kilichowekwa na Latra na kueleza kuwa itasaidia kupunguza gharama za uwekezaji.
Alisema kuwa wamefurahia maamuzi yaliyotolewa na Latra ambapo ameunga mkono zoezi Hilo na kutoa maagizo Kwa wasafirishaji wote kuwaangalia wanafunzi kwani nauli wanayopaswa kuchukua ni 200 tu wasijaribu kuleta matatizo.
Lokeni alisema kuwa awali walikabiliwa na Tozo mbalimbali za serikali zaidi ya 20 ikiwemo Kodi ya mapato, matairi ila Sasa imeonekana imepatikana angalau sehemu katika sekta hii ya usafirishaji ili kufanya uendelezaji.
Naye mwenyekiti wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma usafiri ardhini mkoa wa manyara John Mathew amesema kama watetezi wa Abiria wamelipokea kwa mikono miwili kwani wadau wote wa Usafirishaji wamehusishwa katika kikao hicho.
Hata hivyo baadhi ya kampuni 28 za Usafirishaji wa mabasi ya masafa marefu zimeshiriki katika kaikao hicho
Comments
Post a Comment