TFS NJOONI NA MKAKATI WA MITI YA MATUNDA-MHE. KITANDULA
Na Pendo Mkonyi,Muheza Tanga Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula ameutaka uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuwa na mikakati ya kusambaza miche ya miti ya matunda katika maeneo ya shule za Sekondari Msingi nchini Pichani ni Naibu Waziri wa wizara ya mali asili na utalii mhe Dunstan Kitandula Mhe. Kitandula ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya Kutembelea shamba la Miti Longuza na Hifadhi ya Msitu wa Asili Amani wilayani Muheza Mkoani Tanga. Mhe. Naibu Waziri pia ameutaka uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kuanzisha vilabu vya malihai kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari ili Watoto na vijana wajifunze umuhimu wa uhifadhi wa malisili za misitu nchini. Pia Mhe. Kitandula ameutaka uongozi wa Shamba la Miti Longuza kuweka mkakati wa kusambaza zao jipya la miti inayozalisha zao la mpira kwa vijiji ambavyo vinazunguka eneo la shamba hilo kwa kuwapa elimu wananchi wajiunge kwenye kilimo cha miti hiyo. Vilevile Mhe. Kitand