CHUO CHA BIBILIA PAG CHAHITIMISHA WANACHUO 16 CHAWATAKA KUWA WAADILIFU MAENEO YAO YA KAZI
- Get link
- Other Apps
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Askofu mkuu wa makanisa ya PAG (T) Daniel Awe amewataka Wahitimu waliohitimu mafunzo ya Bibilia Theolojia kuhakikisha wanayafanyia kazi yale yote waliojifunza pamoja na kuwa kielelezo katika jamii.
Ameyasema hayo katika Mahafali ya 18 ya chuo cha Theolojia Cha Regional Bible School (RBS) kilichohitimisha wanachuo 16 njiro jijini Arusha.
Alisema kuwa chuo Cha Bibilia Cha RBS ni chuo kongwe hapa nchini kwani kimehitimisha wasomi wengi katika ngazi mbalimbali na wapo maeneo mbalimbali wakimtumikia Kristo.
Aidha aliwataka Wahitimu kuwa na moto wa uamsho ndani yao na kumtangaza Kristo Kwa mataifa yote ambapo aliwasisitiza kuzingatia maadili mema .
Alinukuu maadili matakatifu kutoka kitabu Cha mathayo 9:1-18 msitari usemao Mathayo 9:1-4
[1]
Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao.
[2]Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
[3]Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.
[4]Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu?.....
Askofu Awe Alisema kuwa chuo hicho kimezalisha wataalamu wengi ambapo ipo mpango mikakati ya kuzalisha wasomi wengi zaidi mpaka ifikapo mwaka 2032 ambapo mambo makubwa makuu matatu yatapewa kipaumbele katika elimu,katika mafunzo,na katika ujuzi wa maisha Kwa njia ya kisasa.
Pamoja na hayo wanachuo wanatarajiwa kufundisha Kwa lugha ya kiingereza ili waweze kuendana Kasi ya teknolojia,lakini pia wataalam zaidi ya 700 wenye cheti wanatarajiwa kuongezeka mpaka ifikapo mwaka
2031 wawe zaidi ya 7000 wenye stashahada.
Kadhalika wenye stashahada kutoka 85 Kwa mwaka 2021 kuwa zaidi ya 300 mpaka mwaka 2032 na wenye shahada ya udhamiri wanatakiwa kufikia 55 na wenye shadya ya uzamivu wa angai wafikie 10 ifikapo mwaka 2032.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho cha Theolojia Cha Regional Bible School (RBS) Mchungaji Mathayo Amsi wakati akizungumza katika ghafla hiyo amewataka Wahitimu kuyafanyia kazi mafundisho waliyoyapata na kuyapima yote yale yasiyofaa na kuyaweka pembeni.
Pia amewataka kutokubali kuiangusha Imani ya kipentekoste Bali waondokane na tamaa zisizo na tija ambapo aliwahusia wanachuo waliobakia kuendelea na masomo na kujitahidi kuwa kielelezo ili waweze kuIfikia kusudi la Mungu.
Mtaaluma mwandamizi katika chuo hicho amesema kuwa wanadhamini kile wanachokifanya pia wanaendana na mpango mkakati ikiwemo elimu kufikia kwani Vipo viwango na mwenendo ambao wasomi wanapaswa kufikia
Alisema kuwa Kituo Cha Arusha ni kituo muhimu sana kwani ndio chimbuko la a vyuo vingine vya PAG nchini
Hiki ni kituo muhimu hakitakufa kwani kinaendelea ambapo amewataka wakufunzi kuendeleza ushirikiano
Umuhimu wa elimu katika kanisa ili
kukabiliana na mafundisho yasiyofaa .
Amesema kama kanisa wanakemea mafundisho yasiyofaa hivyo kupitia mafunzo hayo hawategemei kutokea Kwa mafundisho yasiyofaa kwani wapo baadhi ya watumishi wachache wanaowapotosha watu.
Kuvaa kola kusiwafanye mshindwe kutimiza majukumu yenu ipasavyo
elimu ya kawaida ya ngazi isikupe kiburi bado ina nafasi ya kujiendeleza kwani Kuna diploma na zaidi msijisifu msione mmemaliza Kwani hakuna mafanikio makubwa pasipo mkakati na kuzingatia eneo la elimu.
Kwa upande wake mhitimu katika Mahafali hayo amesema kuwa wamenufaika na fursa mbalimbali katika chuo hicho ikiwemo kufahamiana na wanachuo wengine
Mafanikio katika chuo hicho nii pamoja maboresho ya miundo mbinu katika chuo katika hicho, upatikanaji wa maji Kwa wakati chuo hapo.
Hata hivyo chuo Theolojia Cha Regional Bible School (RBS) kilianza mwaka 1989 na kimekuwa na mafanikio makubwa kufuatia kuzalisha waangalizi wakubwa,wakiwemo maaskofu waangali wa wilaya na wengine wengi.
- Get link
- Other Apps
Comments
Post a Comment