SHULE YA NAZERENE PROGRESSIVE YAWATUNUKU VYETI WAHITIMU 175 WA DARASA LA 7

 Na Pendo Mkonyi, Kilimanjaro.

Mdhibiti mkuu ubora wa shule wa Kanda ya kaskazin Mashariki amekemea vikali vitendo vya ulawiti ushoga na vingine vinavyofanana na hivyo mkoani Kilimanjaro awataka wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya watoto wao ili kuwanusuru na janga hilo ili watoto waweze kufikia ndoto zao.

Akizungumza  Aveline Shirima  kwa niaba ya mdhibiti mkuu ubora wa shule wa Kanda ya kaskazin Akwila Sakaya  katika Mahafali ya 15 Darasa la 7 ya  shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi ya  Nazerene amesema kuwa ni jukumu la mzazi ama mlezi kuhakikisha mtoto/watoto wanakuwa salama.
Aliwataka wazazi kufahamu kuwa lipo wimbo kubwa la uharibifu wa kimaadili ambapo wazazi wameombwa kuwa karibu na watoto  wao kwa kuwaelimisha na kuwasemesha waziwazi ili kuwasaidia kuondokana na machafuko yaliyopo duniani.

Bwana Shirima alisema kuwa shule ya Nazerene ni miongoni mwa shule Bora kwani serikali imeridhishwa na viwango Bora vinavyotolewa na taasisi hiyo ya elimu na pia serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi  nchini 
Aliupongeza uongozi na waalimu Kwa kuwa kinara katika ufundishaji kwani shule imeonekana kuendelea kufanya vizuri kulingana na matokeo mbalimbali ya mitihani mbalimbali ya Taifa ikiwemo kuinua vipawa vya watoto ipasavyo.

Mdhibiti ubora huyo aliwapongeza wazazi wenye watoto waliohitimu Kwa kuwawezesha vijana wao kupata elimu kwani ndani yao watapatikana wataalamu na viongozi mbalimbali  japokuwa aluwakumbusha wazazi kuendelea kuwatunza watoto.

Aidha mdhibiti ubora huyo ameupongeza uongozi wa  taasis za Elimu Nazarene Kwa kusogeza huduma karibu na jamii ilipo kwani shule hiyo ni miongoni mwa shule zinazozingatia ubora na serikali inaitambua taasis hiyo
Pia uongozi wa shule ya Nazerene progressive hivi karibu unataraji kuanzisha elimu ya juu yaani kidato Cha 5 na 6 lengo likiwa ni kurahisha huduma ya elimu katika eneo hilo na pia Kwa wanafunzi wanaohitimu  kuendelea na masomo shuleni hapo.

Kwa upande wake meneja wa shule hiyo Bwana  Wilson Shayo wakati akizungumza katika ghafla hiyo Aliwaahidi kuwakaribisha wazazi na  kukutana  nao ni kwa pamoja mpaka kufikia  mwezi wa 10   kule Township ilipo shule mpya  ya Nazerene iyoanza tangu Januari.

Mkuu wa shule ya Nazarene progressive Bwana Edson Mtaita  wakati akisoma taarifa fupi  ya maendeleo shule  na Matarajio ya  watahiniwa  ya mwaka 2023  alisema kuwa shule ina jumla ya watahiniwa 176 wakiwemo wavulana 91 na wasichana 85 ambapo idadi hiyo imeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo walikuwa na wanafunzi 170.

Aidha Kwa kipindi Cha mwaka jana Wanafunzi 75 walipata daraja A,wanafunzi 46 walipata  daraja B na wanafunzi 18 waliopata daraja c ambapo matokeo ya mwaka Jana hayakuwa mazuri  na lengo halikufikiwa ila upo mkakati uliowekwa na ofisi ya taaluma ambapo Sasa wamejipanga   kuwapa wanafunzi majaribio Kila mwisho wa mwezi,kuwapa kazi za nyumbani, kuhakikisha waalimu wanamaliza mada Kwa wakati

Hata hivyo wanafunzi waliohitimu  Darasa la 7  na kutunukiwa vyeti idadi yao ni 175 ambapo mkuu wa shule hiyo alimtumia  nafasi hiyo kuwapongeza wazazi kuwa kipaumbele kufuatilia maendeleo ya watoto wao Kwa kina  pindi walipokuwa shuleni  ambapo aliwahusia wazazi kuwatafutia watoto wao vituo Kwa ajili ya masomo ya baadaye.

Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.