DR KAZOBA AFUNGUA TAWI LA TIBA MBADALA ARUSHA
Na Pendo Mkonyi, Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Bwana Felician Mtahengerwa amewataka watanzania kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kuzipa kipaumbele Kwa kuzinunua Kwa wingi na kuepuka kutukuza bidhaa zinazozalishwa nje
Pichani ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Bwana Felician Mtahengerwa.
Ameyasema hayo wakati akizindua duka la dawa za asilia la Kazoba Herbal International jijini Arusha na kusema kuwa sawa hizi dawa za kiasili zinasaidia sana kuponya magonjwa mbalimbali.
Aidha Mtahengerwa amesema kuwa dawa za kiasili ama miti shamba zipo vizuri kwani hizi ndizo wazungu hufanyia tafiti na kuzalisha dawa za kizungu na kurudi kuziuza huku afrika.
Mtahengerwa amesema kuwa ni vema watanzania wakajenga utamaduni wa kudhamini bidaaa zinazozalishwa hapa nchini kwani hakuna mwingine wa kuziinua zaidi yenu.
Kwa upande wake Dr Kazoba mkurugenzi mtendaji wa Kazoba International Herbal product wakati akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa ni muda mrefu amekuwa akijishughulisha na tafiti mbalimbali za dawa ambapo pia amekuwa akitembelea hospitali mbalimbali nchini na kufanyia tafiti kupitia dawa za Asili.
Kadhalika Dr Kazoba amesema kuwa mara baada ya kufanya tafiti dawa zake hupeleka Kwa mkemia mkuu ili kuthibitisha ubora ambapo mafanikio ni makubwa ikiwemo wizara ya afya amabyo hutoa cheti cha kutambua dawa hizo.
Amesema kuwa uzinduzi huo umeenda sambamba na siku yake ya kuzaliwa ambapo kituo hicho kitatumika zaidi kuwahudumia watanzania katika nyanja mbalimbali na ikiwemo vipimo.
Hata hivyo Dr Kazoba amesema kuwa watumiaji wanapaswa kufahamu dawa zote zilizoandaliwa na Kazoba International Herbal product zimeaminiwa kwani zinakinga na kutibu magonjwa.
Kauli mbiu ya Kazoba International Herbal product ni afya yako ndio mtaji wako wa kwanza
Comments
Post a Comment