WANANCH WA MONDULI WAISHUKURU MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA(AUWSA) KUFANIKISHA ZOEZI LA UPATIKANAJI WA MAJI MONDULI.
Na Pendo Mkonyi, Arusha
Mbunge wa jimbo la Monduli pamoja na Wananchi wa wilaya ya Monduli wameipongeza serikali Kwa kuwatatulia tatizo la maji kufuatia tatizo hilo kudumu Kwa takribani miezi 3
Pichani ni Mbunge wa jimbo la Monduli Fredick Lowasa.Akizungumza na waandishi wa Habari Mbunge wa jimbo la Monduli Fredick Lowasa amesema kuwa ameishukuru serikali Kwa kutatua tatizo hilo kwani lilikuwa ni kero Kwa wananchi kufuatia wqnanchi kuhangaika kutafuta Maji kwani wanawake walilazimika kutafuta maji Kwa punda hata maeneo ya mjini jambo ambalo lilikuwa halipendezi.
Aidha Mbunge huyo alisema kuwa takribani kata 3 ikiwemo Monduli juu,meserani,Engutoto na Lashaine walikuwa wameathirika Kwa sehemu kubwa ukizingatia ni kata za mjini ila ameipongeza Mamlaka Kwa kipindi hicho ambacho walifanikiwa kusambaza maboza ya maji Kwa wananchi ili kuwasaidia kuondoa adha Kwa akina mama.
Alisema kuwa Monduli Sasa maji yatapatikana kufuatia pampu kubwa kutoka ufaransa yenye uwezo wa kusukuma maji kilometa 40 kufungwa katika kisima Cha Seedfam Ngaramtoni mkoani Arusha Ambapo huo ni mradi wa miaka 20 ambao uliletwa na mzee Lowasa kupitia mkopo wa IDB.
Ameipongeza Mamlaka Kwa kuonyesha jambo kubwa aliloliomba tokea wakati wake wa kwanza wa kampeni enzi za marehemu Dr Magufuli ambapo mchakato huo bado ulikuwa haujaanza hata Kwa Rias wa Sasa haikuwa ahadi yake kwani mchakato wa upatikanaji wa maji eneo hilo haukuwa kwenye mpango Bali na Hai na maeneo mengine lakini mheshimiwa Rais baadaye alipokea jambo Hilo na kulifanyia kazi.
Mbunge huyo amesema kuwa Monduli ni eneo ambalo wananchi hawakuwahi kuona maji tangu enzi za uhuru ila Sasa mradi huu unaenda vizuri kwani mradi mkubwa billion 16 unaotaraji kutokea ambapo utawanufaisha Wana Monduli hivi karibuni.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli Isack Joseph ametumia fursa hiyo kumshukuru waziri wa maji Juma Aweso Kwa kufanikisha jambo Hilo pamoja na mkuu wa wilaya ya Monduli Joshua Nasari Kwa kuwezesha jambo Hilo kupitia serikali ya awamu ya 6 kwani Kila wakati wamekuwa wakiangalia namna ya kutatua tatizo hilo la maji.
Naye mkuu wa wilaya ya Monduli Joshua Nasari amesema kuwa kama kiongozi mkuu wa kiserkali ametoa pole Kwa wananchi kwani hakuna aliyependa tatizo Hilo liwepo kwani halikupangwa ila Monduli sasa tayari tatizo hilo limefika mwisho kufuatia kujengwa kisima chenye uwezo wa kubeba Lita milioni 10 ambacho kimeshakamilika ambapo vijiji 13 vitanufaika na mradi huo.
Na Ijulikane kuwa wilaya ya moduli hakuna mradi wowote wa maji umewahi kufanyika hivyo kutokana na mradi mkubwa wa mkoa wa Arusha wa zaidi Bilioni 520 serikali iliona kilio cha wananchi wa Monduli ikaamua kufanya mradi mdogo ndani yake wa billion 16 ambapo tangu miaka 20 ipite haukuwahi kutokea hivyo mapinduzi makubwa yanakwenda kwenye vijiji 13 mpaka nanja.
Mathalani mradi huo wa maji unaenda kuongeza kiwango Cha maji eneo la Monduli Mjini kwani mkandarasi ameshapatikana ambaye ni Jandu kwani anaaminika na siyo kampuni ya ubabaihaji hivi karibuni mkataba huo utakwenda kusainiwa.
Bwana Nasari alitoa angalizo Kwa Mamlaka na wananchi kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kudumu Kwani pampu hiyo imegharimu kiasi Kikubwa Cha fedha ambapo aliwataka kutunza hicho kidogo walichopata wakati wakisubiri mradi mkubwa ujazo ambapo amewakumbusha pia wananchi kujitahidi kutatua changamoto za wananchi na siyo kupiga Kelele Bali kuonyesha njia.
Meneja wa mkoa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (AUWSA) Bwana Justin Rujomba amesema kuwa anaushukuru uongozi wa wilaya ya Monduli Kwa kumpa ushirikiano mkubwa Kwa kipindi Chote ambacho pampu ilivyokuwa imeuungua ambapo amesema kuwa huo ni mfano wa kuigwa na ya kuwa kunapotokea jambo viongozi wanapaswa kutatua changamoto na siyo kulalamika.
Sanjari na hayo Bwana Rujomba amesema kuwa wao kama Mamlaka pamoja na Ruwasa wamejipanga kutatua changamoto ya ukosefu wa maji mji wa Monduli ambapo wamefunga pampu mpya ili maji yaweze kupatikana licha ya mradi mkubwa ujao wa bilio16 ambao umeidhinishwa na mheshimiwa Rais na wao kama watendaji na Ruwasa mkoa Sasa wataweka Muda ni lini mradi huo ukamilike pindi Jandu watakaposaini mkataba huo.
Comments
Post a Comment