MASISTA WA MTAKATIFU BENEDICTINE WAWEKA NADHIRI ZA KWANAZA WAFUNGA NDOA NAYESU

 Na Pendo Mkonyi,Same.

Masisita  watatu wanofisi au waandaliwa wa hatua katika utawa wamekubali kuweka Nadhiri katika kanisa la Benedict lengo likiwa ni kujitoa maisha yao yote kumtumikia Mungu.

Akizungumza na waandishi wa habari Padre Joseph Andrea Mlacha ambaye ni Wakili paroko wa kanisa kuu Kristo mchungaji  mwema jimbo Katoliki la same.
Padre Mlacha amesema sherehe hiyo imefanyika mara baada ya masisita hao kuweka Nadhiri za kwanza. 
Pichani ni Padre Joseph Andrea Mlacha ambaye ni Wakili paroko wa kanisa kuu Kristo mchungaji  mwema jimbo Katoliki la same.

Aidha padre alisema kuwa ili uweze kuwa mtawa ni lazima uombe na utume maombi kwenye Shirika ili uweze kujiunga ambapo Shirika huwakubalia ambapo Shirika Hilo makao yake makuu ya jimbo la Songea ambapo lilianzishwa nyumba yake same ambayo ni Benedictine ambao wanajiita  mtakatifu Maria Goreth same lenye matawi mkoani Singida na mkoani mwanza.

Alisema kuwa zipo hatua mbalimbali za kuwa mtawa ikiwemo hatua ya  kwanza ya  kuomba inyoitwa asipiranti mtakaji mwombaji ikifuata hatua ya unofisi na hatimaye hatua ya ukandidati na mwisho unafikia hatua ya kuweka Nadhiri za kudumu na hatimaye unaweza kuwa sister

Kadhalika Padre Mlacha alisema kuwa unaweza kutumia maombi pengine ukiwa hata umehitimu kidato Cha nne kwa wale waliosoma Kwa sasa

Alitoa wito Kwa watu wanaotaka kuwa watawa  kudumu katika maombi wakimuomba Mungu awangazie ili waweze kujua wito walioitiwa na Mungu ili waweze kuyapata makuu ya Mungu wakisaidiwa na wazazi wao na walezi kama mapadre ili mwisho waweze kufikia hatua waliokusudia ikiwa ni Baraka ya Mungu.

Hata hivyo Wahitimu waliohitimu wako watatu kutoka majimbo matatu tofauti likiwemo jimbo la Sumbawanga,mwingine jimbo la Kokayanga na mwingine jimbo la Rurengengala kwasababu wito ni popote kama neno linavyosema enenendeni ulimwengu mkatangaze injili kwa Kila kiumbe hivyo wanaenda popote Mungu alipowaita hivyo kama hao waliotoka mbali ni mfano mzuri kama ilivyokuwa Kwa Ibrahim alivyotoka katika nchi yake aende alipooneshwa na  alivyopewa maagizo na Mungu katika utumishi wake

Alitoa wito Kwa watawa hao kwenda kutoa huduma ya injili ipasavyo na kuwajali watu wa Mungu yaani watu wote bila kubagua rangi,kabila na Imani ili waweze kuokolewa.

Kwa upande  wao masisita wlioweka Nadhiri akiwemo  maria Katarina Seleman kutoka jimbo la  Sumbawanga alisema kuwa amefurahi sana kutembelewa na mwenyezi Mungu ili amtumikie ambapo alitoa rai Kwa wengine Wanataka kuwa mtawa wasikate tamaa Bali wajitoe, amesema katika malezi ana miaka 7 na amejongea na kupata ekari takatifu ya Bwana ambapo ametambua kuishi maisha ya uprofesi na pia ataendelea miaka 6 na kuingia Nadhiri za daima zitakazohusisha kuvaa Pete na taji kichwani.
Pichani ni Maria Katarina Seleman kutoka jimbo la  Sumbawanga


Naye sister Maria Galucian alisema kuwa Kwa mapenzi yake Mungu amepokelewa katika daraja la uprofesa ambalo linaitwa kufungwa Nadhiri ambapo ameweka ahadi Kwa Mungu ambazo Nadhiri zipo tatu ukiwemo ufukara, uthabiti uogofya wa mwenendo wa kitawa na utii ambazo ataziishi katika maisha yake Kwa kumtumikia Mungu yaani alisema amefanikiwa kufunga ndoa na Yesu.
Pichani ni Maria Galucian 

Aliwaalika  watu ambao Wanataka kumtumikia Mungu  na kuwa watawa kujitoa sadaka na kujikana katika maisha yao ili waweze kumtumikia Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.