KAMPUNI YA ZARA TOURS YASHEREKEA SIKU YA UTALII DUNIANI ,YATAJA MAFANIKIO MAKUBWA KWA KIPINDI CHA ZAIDI YA MIAKA 30 CHA UTOAJI HUDUMA YAKE KWA JAMII.
Na Pendo Mkonyi, Kilimanjaro
Katika kuadhimisha siku ya utalii duniani kampuni ya Zara tour yaipongeza serikali ya Tanzania hususani pongezi kubwa Kwa mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuitangaza nchi ya Tanzania kupitia filamu ya The Royal Tour kwani matokeo makubwa yametokea katika kusukuma sekta ya utalii.
Hayo yamesemwa na Zainab Ansell mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Zara Tanzania Adventures wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa filamu ya Royal Tour imeleta mchango mkubwa kwani imesukuma sekta ya utalii ipasavyo kwani ulimwengu mzima sasa unaijua nchi ya Tanzania.
Aidha alisema kuwa mwaka huu umekuwa mwaka wa Baraka sana kwa watalii na mambo yameenda vizuri na ipo Imani kubwa mpaka kufikia 2024 Hadi 2025 katika nchi Tanzania itakuwa mbali katika sekta ya utalii.
wakati huo amesema kuwa pindi mgeni mmoja anapowasili nchini ni furaha Kwa mama wa sokoni kwani ni lazima watanufaika,vijana watapata ajira,mama wa dukani watafanya mauzo mpaka wafanyakazi waliopo mahotelini.
Pamoja na hayo alisema kuwa siku ya Leo ya utalii duniani ni siku ya kujivunia sana kwani pia kampuni ya Zara Tanzania Adventures limefanikiwa kwani imefanikiwa kutoa huduma kwa zaidi ya miaka 37 kwenye jamii ikiwemo utoaji elimu ambapo wamefanikiwa kufungua shule ya Zara charity kuanzia 2019,pia ipo Moshi kids center kwani elimu ni ufunguo wa maisha,ajira Kwa vijana zimetolewa,akina mama,akina dada na wengine wengi kupitia utalii,
Hata hivyo amewakaribisha watanzania kufika Zara kwenda kupanda mlima Kilimanjaro Kwa bei nafuu kipindi Cha kusherehekea miaka 62 ya uhuru
Baadhi ya wanufaika katika kampuni ya Zara Tanzania Adventures wakiwemo madereva na waongoza utalii wamekiri mafanikio makubwa katika maisha yao na familia zao Kwa kuziwezesha ipasavyo kikipato.
Joseph Marandu ni muongoza utalii katika kampuni ya Zara tours kwa.
miaka 20 Sasa amesema kuwa kampuni ya Zara imemsaidia sana katika maisha yake na amrjipayia uzoefu mkubwa kutokana na kuwepo kwenye kampuni hiyo miaka hiyo.
Raphael Mwambora ni dereva katika kampuni ya Zara Tanzania Adventures ambapo pia ameiomba Shirika la hifadhi Taifa kuboresha miundo mbinu ya barabara iliyopo mbugani ili magari yaweze kupita vizuri kwani ubovu wa barabara unachangiwa magari kuharibika haribika ovyo.
Comments
Post a Comment