WAFANYA BIASHARA WA MKOA WA ARUSHA WAPATA MTANDAO WA MASOKO WA NDANI NA NJE YA NCHI KUPITIA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA TECHNOSERVE
Na Pendo Mkonyi, Arusha. Afisa biashara mkoa wa Arusha amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi Kwa wafanyabiashara ambapo amewasisitiza wafanyabiashara kufuata kanununi na sheria ili waweze kufanya biashara hata nje nchi. Pichani ni Afisa biashara mkoa wa arusha Bwana Njivaine Mollel Akizungumza na waandishi wa habari Njivaine Mollel katika semina iliyowakutanisha wadau wa biashara na wataalam jijiji Arusha amewasihi wafanyabiashara kuhakikisha wanakuwa ba vielelezo vyote muhimu vya ufanyaji biashara ili kuepuka usumbufu usiokuwa na lazima na pia ili waweze kushindana ipasavyo sokoni wazingatie ubora wa bidhaa. Kwa upande wake Getrude Kawam msimamizi wa mradi wa wasindikaji wa chakula jumuishi lishe unaofadhiliwa na Shirika la maendeleo yakimarekani USAID kupitia FEED THE FUTURE wakati akizungumza katika semina hiyo amesema kuwa wamewakuranisha wafanyabiashara na Shirika liso la kiserkali la Tekno serve ili usambazaji wa bidhaa zao zinawafikia walaji wa ndani na nje