SHULE YA MSINGI YA MCHEPUO WA KIINGEREZA YA MECSON YA JIJINI ARUSHA YAFANYA MAHAFALI YA 12 YAHITIMISHA WANAFUNZI 57 WA DARASA LA 7
Na Pendo Mkonyi, Arusha
Elimu imetajwa kuwa nyenzo kubwa duniani Tena ni mkombozi mkubwa maishani mwanadamu.
Hayo yamesemwa na Dr,Dominic Ringo mkurugenzi wa Recoda wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 12 na kuipongeaa shule ya mchepuo wa kiingereza ya Mecson Kwa kuwaandaa watoto ipasavyo ikiwemo wazazi kukubali kuwekeza Kwa watoto wao.
Dr Dominic amesema kuwa urithi Bora na zawadi nzuri Kwa mtoto ni elimu hivyo amewapongeza wazazi Kwa kuwawezesha watoto kupata elimu ambayo ndio msaada katika maisha yao.
Uwekezaji wa elimu Kwa watoto katika shule za msingi ni muhimu maana ndipo uhitaji ulipo zaidi katika kuwaimarisha pia msingi Imara katika mambo ya tehama ni muhimu ili waweze kuendana na kasi ya teknolojia.
Hata hivyo endapo mtoto hataandaliwa vema siku za usoni anaweza kuwa kibarua kutokana na kushindwa kuandaliwa kukabiliana na changamoto hivyo wazazi na waalimu wanalo jukumu la kufundisha mtoto kufanya bidii isivyo kawaida,wazazi wanatakiwa kuwa na maono ya kuwasaidia watoto wao wenye kujitambua,
ikiwemo wazazi kukubali kuwekeza Kwa watoto wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya ya Mecson iliyopo olasiti jijini la Arusha amewataka wazazi wa watoto waliohitimu Darasa la 7 kuhakikisha wanaenda kuwatunza watoto pindi wanaporejea majumbani kufuatia duania ya Sasa kuharibika na kuvutia zaidi Kwa nje kuliko ndani.
Hayo yamesemwa na Meck shirima mkurugenzi mtendaji wa shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya Awali na msingi ya Mecson wakati akizungumza katika Mahafali ya 12 ya na kusema kuwa watoto waliohitimu wamelelewa katika maadil mema na wamefundishwa katika maisha ya kiroho na kielimu.
Amesema kuwa wazazi wanapaswa kuwalea watoto katika njia iwapasao Kwa kipindi chote watakachokuwa majumbani ili wasisahau kile ambacho walichofundishwa Kwa Muda mrefu hapo shule ya Mecson
Kwa upande wake mtaaluma Mwandamizi katika shule ya Mecson Bwana Moses Ruheba amesema kuwa katika Mahafali wamehitimisha wanafunzi 57 wakiwemo wasichana23 na wavulana34 hivyo wanamshukuru Mungu Kwa tukio Hilo
Ni Matumaini Yao shule hiyo itafaulisha Kwa kiwango Cha juu kwani mara nyingi wanafunzi wote hufaulu na kupangiwa shule kadhaa ndani ya jiji la Arusha na wengine hupangiwa shule za viipaji maalum.
Ametoa wito Kwa wazazi wa watoto waliohitimu kuendelea kujiamini shule yaMecson na wazidi kuwaandikisha watoto Kwa wingi kwani shule hiyo inamtegemea Mungu siku zote.
Baadhi ya Wahitimu katika shule hiyo akiwemo Angela Shirima amewashukuru waalimu katika shule ya Mecson Kwa kumuwezesha mpaka hapo alipofikia ambapo ametaja mbinu na Siri ya yeye kufanikiwa ni kujisomea Kwa bidii ikiwemo ratiba kabambe aliyojiwekwa nyumbani Kwa ajili ya masomo yake ambapo amewasihi wengine kuendelea kujisomea ili waweze kuIfikia ndoto za maisha yao.
Comments
Post a Comment