NCHI ZAIDI YA 20 ZA SHIRIKISHO LA MIFUKO YA UHIFADHI WA MAZINGIRA BARANI AFRIKA WAKUTANA ARUSHA KATIKA MKUTANO WA 13 WA CAFE
Na Pendo Mkonyi,Arusha.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mary Masanja amefungua Mkutano wa 13 wa Shirikisho la Mifuko ya Uhifadhi wa Mazingira Barani Afrika jijini Arusha.
Pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mary MasanjaMkutano huo unajumuisha Mifuko 17 kutoka Nchi 20 za Afrika pamoja na Mifuko rafiki 4 toka Nchi za Bara la Amerika ya Kusini na Karibeni unaanza leo tarehe 28/08/2023 na kumalizika tarehe 01/09/2023.
Sambamba na hilo Naibu Waziri Masanja amesema kuwa Wageni hao mara baada ya kumalizika kwa Mkutano watapata fursa ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini hususan Mkoani Arusha kwa lengo la kuendelea kutangaza Utalii Duniani kupitia Filamu ya - The Royal Tour iliyoasisiwa na Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Naibu waziri amesema kuwa Nchi ya Tanzania ni nchi ya kwanza Barani Afrika na ya 12 duniani Kwa ubora wa vivutio vya utalii vya Asili ambavyo vivutio hivyo vimewezesha Tanzania kutambuliwa na taasisi mbalimbali duniani kama sehemu muhimu Kwa shughuli za utalii.
Tanzania ina eneo la misitu linalofikia hekta 48.1 ambayo huchangia katika uhifadhi wa bionwani, makazi ya wantama na uhavushaji wa mazao mbalimbali,sehemu kubwa ya misitu hiyo takribani hekta milioni 25 ni misitu ya matajawazi ambayohuwezesha shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji nyuki,utalii wa kiikolojia na uwindaji wa kitalii.
Lengo la la mkutano wa 13 WA CAFE una lengo Pana la kuhakikisha upatikanaji endelevu wa fedha ili kukidhi matakwa ya uhifadhi wa maliasili na mazingira,amewahamasisha wadau wa utalii kuutangaza Tanzania nchi isifikayo kama kisiwa Cha amani na yenye wananchi walio na upendo na iliyobarikiwa kuwa na hazina kubwa ya utajiri wa vivutio vya maliasili ba utalii vya kipekee vitakavyokuacha na kumbukumbu nzuri isiyosahaulika.
Kwa upande wake Deusdedit Bwoyo Mwazilishi wa Katibu mkuu ,wizara ya maliasili na utalii amesema mkutano huu ni wanachama kutoka mifuko 19 iliyoko katika nchi 20 za afrika wakishirikiana na mifuko 5 Rafiki kutoka Amerika ya kusini na visiwa vya Caribeani.
Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) Na mfuko wa Hifadhi ya milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF) ni wanachama wa CAFE na ni wenyeji wa mkutano huu ambapo kama ya uongozi wa cafe imeshirikiana na mifuko ya TaFF na EAMCEF katika kufanikisha mkutano huu.
Kaimu katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Bw Ramadhani Madeleka amesema kuwa aliwatumia nafasi hiyo kuwakaribisha Na kuwaalika kutembelea hifadhi ya eneo la ngorongoro na meno mengine yenye vivutio vya utalii ndani ya mkoa wa Arusha na Kwa kutembelea maeneo hayo mkoa na kuwa mabalozi waziri wa kutangaza vivutio vyeti katika nchi mnazotoka na pia mnaweza kuona fursa za kuendelea kusaidia juhudi za uendelezaji wa uhifadhi na rasilimali zilizopo Kwa kipindi Chote mtakachokuwa Arusha jiji.
Comments
Post a Comment