WAHITUMU 45 KUTOKA SHULE YA KANISA LA MUNGU ALDERSGATE BABATI WATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU DARASA LA 7 MAHAFALI YA 17.

 

Na Pendo Mkonyi,Babati

Afisa elimu elimu maalum shule za sekondari halmashauri ya mji wa Babati Martin Petro Kwa niaba ya afisa elimu shule msingi ameupongeza uongozi wa shule za Aldersgate Kwa kazi nzuri wanaofanya kwani shule hiyo ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika halmashauri ya mji wa Babati.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 17 y shule ya msingi ya mchepuo ya Aldersgate .

Pichani ni Martin Petro  afisa elimu,Elimu maalum shule za sekondari halmashauri ya mji wa Babati.

Aidha katika Mahafali hayo ya 17 Kwa wanafunzi wa darasa la 7 na darasa awali amewataka wazazi kuendelea kufuatilia malezi ya watoto wao kwani Kwa kipindi Chote Cha  miaka 7 shuleni watoto wamekuwa katika hali nzuri.

Serikali imelipongeza kanisa la Mungu Kwa kufanya uwekezaji mkubwa na mzuri Kwa ajili ya masuala ya elimu na kuweka mazingira rafiki ya shule Kwa ajili ya wanafunzi pia pongezi Kwa waalimu Kwa kuwawezesha watoto Kwa kufanya vizuri katika mitaala  iliyo rasmi na isiyo rasmi 

Ni Imani yake kuwa watoto watafaulu Kwa kiwango Cha juu kwani tangu shule hiyo hiyo  imeanzishwa haijawahi kufelisha tangu kuanza Kwa shule mwaka  2007 ni dhahiri kuwa shule itafaulu vizuri kuanzia ngazi ya halmashauri na kimkoa hata kitaifa 

Alitoa rai Kwa taasis za elimu kuwasimamua watoto katika masuala ya taaluma na nidhamu ili halmashauri hiyo iweze kuwa Bora zaidi ndani ya halmashauri yenyewe na Taifa Kwa ujumla 

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule ya Aldersgate Dr Fadhil Mshana amewashukuru wazazi waliowakubali na kuwaandikisha watoto wao katika shule hiyo kwani pia shule hiyo kimatokeo darasa la 4 na la 7 wamekuwa walifaulu na pia wanafunzi wamekuwa wakifanya vizuri na ukizingatia watoto wanavyo vipaji kama walivyovionesha.
Pichani ni  mwenyekiti wa kamati ya shule ya Aldersgate Dr Fadhil Mshana.

Aliwataka wazazi kufahamu kuwa shule ya Aldersgate ni eneo sahihi la kumpeleka mtoto kujisomea hivyo wazazi wajitahidi kulipa ada Kwa wakati ili  wanafunzi wazidi kunufaika na mpango wa elimu isiwe kikwazo Kwa watoto kushindwa kuendelea kujisomea eti kwasababu ya mzazi kushindwa kulipa ada hiyo haipendezi.

Mkuu wa shule ya msingi ya  mchepuo wa kiingereza ya Aldersgate Ester Mathias amesema kuwa takribani Wanafunzi 45 wametunukiwa vyeti na wameandaliwa vizuri na watafaulu kwani watoto wazuri wenye maadili mema na Kila mara wamesisitizwa kufuata maadili ya kitanzania na kuondokana maisha ya mfumo wa magharibi yanayoharibu sura na taswira nzuri ya maadili ya Tanzania.
Pichani ni mkuu wa shule ya  msingi ya mchepuo wa kiingereza ya Aldersgate.

Aliwataka wazazi kwenda kuwaandikisha watoto kwenye nafasi za elimu ya chekechea, awali kwani Aldersgate ni eneo la mikono salama Kwa maisha ya watoto.

Mchungaji Paul Fisoo na mtumishi katika shule ya Aldersgate amesema kuwa shule ya Aldersgate imekuwa ya  mfano wa kuigwa kwani ni sehemu salama na shule hiyo ina miundo mbinu rafiki usafiri Kwa ajili ya watoto,pia shule ina uzio  Kwa lengo la kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira salama.
Pichani ni mchungaji Paul Fisoo washule ya Aldersgate.


Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.