LAKE MANYARA HALF MARATHON KUFANYA MBIO ZA KM 21,KM 10 NA KM 3.5 TAREHE 29/10/2023.

Na Pendo Mkonyi Mto wa Mbu.

Taasis ya Greenleaf Sports Promotion,imeandaa mashindano ya  Mbio yatakayofanyika eneo la mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha mnamo tarehe 29/10/2023

Akizungumza na vyombo vya habari mwandaaji wa Mbio hizo za lake Manyara Half  Marathon Morris Okinda  amesema kuwa Mbio hizo zitafanyika  kuanzia lango la kuingiliwa hifadhi ya ziwa Manyara na kumalizika  katika  uwanja wa Barafu.

Okinda alisema kuwa lengo la Mbio hizo ni kupata wachezaji wa kuliwakilisha taifa  kwa kuinua vipaji na kutangaza utalii katika mto wa Mbu kufuatia kuwa na vivutio vingi vya utalii hususani eneo la mto wa Mbu lenye sehemu zuri la kupumzika.

Aidha  katika mashindano hayo kitakuwa na mashindano ya Mbio aina 3
Aina ya kwanza ni 21km Half Marathon aina ya pili ni 10km Excutive Run na aina ya tatu ni 3.5km fun Run.

Mbio hizo za za Lake Manyara half Marathon zitakuwa ni Mbio za barabarani ambazo zitaanzia  lango la hifadhi ya ziwa  Manyara, kuelekea barabara ya Mto wa Mbu Makuyuni na  kumalizikia uwanja wa Barafu mto wa Mbu

Kutakuwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma  za Asili,wasanii,michezo ya watoto na  katika maandalizi hayo ya lake  Manyara half marathon ipo kamati ya maandalizi Kwa kushirikiana  na baadhi ya taasis ili kufanikisha Mbio hizo na taasis hizo ni kama ifuatavyo Lake Manyara National Park,Tanzania Cultural Tourism programe(CTP) Jungle Pearl Resort,King Scorpion Safari,Teast Poa Cafe,Bonite Bottlers,na Tigo Tanzania

Lake Manyara half Marathon ina kifurushi ambacho kitakuwa na namba ya kukimbilia ,T shirt rasmi ya mashindano pamoja na Medal.

Zawadi zitakazotolewa zitakuwa na viwango tofauti kulingana na Mbio 21km-Half Marathon -Wanaume
1.1000,000/=
2.500,000/=
3.400,000/=
4.250,000/=
5.200,000/=
6.100,000/=
7.100,000/=
8.100,000/=

10km-EXCUTIVE   RUN -WANAUME NA WANAWAKE
1.500,000/=
2.350,000/=
3.200,000/=
4.150,000/=
5.100,000/=
6.50,000/=
7.50,000/=
8.50,000/=

NA 5KM-FUN RUN  Washiriki wote watapewa medali tu.

Usajili utakuwa kama ifuatavyo ili kushiriki Mbio za lake  Manyara Half Marathon utaweza kujisajil Kwa Njia  ya Twhema (online) kwenye website ni http:reg.lakemanyaramarathon.com na kufanya malipo ya Tsh 35000/=tu kupitia Tigo ambapo lipa no ni5639852-Lake Manyara Marathon 23.

Kwa upande wake meneja mauzo  Kampuni ya Tigo Tanzania Karatu Bwana Mwema Machange  alisema kuwa wameshirikiana ili kuhakikisha zoezi Hilo linaenda vizuri kuliko walivyotarajia kwani kampuni  ya mawasiliano ya Tigo  Tanzania imekuwa ikisapoti michezo kwani michezo Sasa ni  ajira kubwa sana duniani hivyo hawataki kuona watanzania wenye vipaji wakibakia nyuma ili Kila mtanzania aweze kufurahia ,wanafanya hivyo kuhakikisha watanzania wanafahamu kuwa Tigo ipo kila mahali.

Kampuni ya Tigo imeahidi kufikisha  habari hizo Kanda ya Kaskazini na hata nje ili watanzania waweze kujumuika na  ili  vijana waweze kutimiza ndoto zao na kuweza kujiongezea kiajira na kipato Kwa pamoja na vilevile Tigo ina kampeni ya  mchezo wa Tigo Cha wote ambayo lengo ni kuwafikia watumiaji  wa tigo kuweza kujishindia zawadi ikiwemo sms,dakika mbs na pesa tasilimu ambapo kutakuwa na ticket utakayoweza kununua kupitia lipa namba.

Meneja wa kampuni ya  Test Poa Coffee Kenned  Mwangosi wa mkoani arusha wilaya ya Monduli amesema kuwa wao wamejipanga kudhamini huo mchezo wa kukimbia kwani kukimbia ni moja ya mazoezi katika afya ya mwanadamu na Mbio Bora ni pamoja na afya njema hivyo ijulikane kuwa Test Poa Coffee ni miongoni mwa wadau wa wakubwa wa utalii nchini ambao  ni  wanatoa huduma na  wapo sehemu ya pekee maeneo ya mto wa Mbu chini ya TANAPA  kwa kuwapokea wageni mbalimbali.hivyo  watakuwa karibu na wageni wote Kwa kuwaandalia vyakula vyenye ladha Halisi na vinywaji siku hiyo.

Hata hivyo kauli Mbiu ya Mbio hizo  za lake Manyara Half Marathon ni Tukimbie  Tukitalii.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.