WAFANYA BIASHARA WA MKOA WA ARUSHA WAPATA MTANDAO WA MASOKO WA NDANI NA NJE YA NCHI KUPITIA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA TECHNOSERVE
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Afisa biashara mkoa wa Arusha amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi Kwa wafanyabiashara ambapo amewasisitiza wafanyabiashara kufuata kanununi na sheria ili waweze kufanya biashara hata nje nchi.
Pichani ni Afisa biashara mkoa wa arusha Bwana Njivaine MollelAkizungumza na waandishi wa habari Njivaine Mollel katika semina iliyowakutanisha wadau wa biashara na wataalam jijiji Arusha amewasihi wafanyabiashara kuhakikisha wanakuwa ba vielelezo vyote muhimu vya ufanyaji biashara ili kuepuka usumbufu usiokuwa na lazima na pia ili waweze kushindana ipasavyo sokoni wazingatie ubora wa bidhaa.
Kwa upande wake Getrude Kawam msimamizi wa mradi wa wasindikaji wa chakula jumuishi lishe unaofadhiliwa na Shirika la maendeleo yakimarekani USAID kupitia FEED THE FUTURE wakati akizungumza katika semina hiyo amesema kuwa wamewakuranisha wafanyabiashara na Shirika liso la kiserkali la Tekno serve ili usambazaji wa bidhaa zao zinawafikia walaji wa ndani na nje ya nchi hivyo mara baada ya semina hiyo watapata matokeo mazuri.
Lengo ni kuhakikisha bidhaa hizo zinapatikana Kwa wakati na bidhaa zinaenda Kwa walengwa hususani Kwa wafanyabiashara wa chini wa kati na WA juu anbapo wafanyabiashara hao watapata kusaini makubaliano ambayo hayamfungi mtu.
Aidha mradi huo tayari umeshafanya kazi katika mikoa 8 nchini Tanzania na watu zaidi ya 500 nchini wamefikiwa na mkoa wa Arusha ni mara ya 2 kufanyika vilevile Kwa mkoa wa Arusha na Moshi zaidi ya watu 30 wamefikiwa
Mwitikio umekuwa mzuri sana kufuatia wafanyabiashara wengi kuona umuhimu wa kujitokeza na kujifunza zaidi kwenye makongamano.na semina kama hizo
Meneja wa Benki ya kiislam Tanzania ya Amana tawi la Arusha Bwana Francis Mizambwa amesema kuwa taasis hiyo ya kufedha imekuwa ikiwasaidia wakulima wadogo wakiwemo wa vikundi,wa kati na wakubwa kupata pembejeo,dawa,na vifaa vinavyowawezesha kulima.
Francis Mizambwa
Aidha benki hiyo ya kipekee nchini imekuwa bega Kwa bega kuwasaidia wakulima na wafugaji na mnyororo wake wote ikiwemo kununua vifaa vya kufanikisha kulima mfano trekta,vifaa vya umwagilijiaji na maghala.
Pamoja na hayo benki ya Amana pia inawasaidia wafanyabiashara ambao ni wanunuzi wa bidhaa kama vile kuku,mahindi na wanahitaji kusafirisha nje wanapewa ushauri na kusaidiwa kujitambua kukaa anapostahili ili aweze kufanya biashara zake ipasavyo.
Mkurugenzi wa kiwanda Cha maisha millers kinachozalisha unga sembe mkoani arusha bwana Imran amefurahishwa na semina hiyo ambayo amesema mafunzo hayo yamemwimarisha zaidi ambapo kibiashara kiwanda Cha maisha millers kimefanikiwa kusambaza bidhaa hiyo nchini na kidogo kenya
Aliwataka wakulima Kwa wingi zao la mahindi na kuyahifadhi katika hali nzuri ili yafae katika soko kufuatia baadhi ya wafanyabiashara wa zao hilo kushindwa kutunza ipasavyo ili kufikia viwango vya kimataifa sokoni
Kampuni ya usindikaji maziwa na uuzaji bidhaa mbalimbali za maziwa ya Asil Dairy mkoani Arusha imeishukuru Technoserve Kwa kuwapa nafasi ya kukutana na wataam mbalimbali katika kukuza wigo kibiashara
Jackline Ngasa amesema kuwa Asili Dairy wamejipanga ipasavyo kufikia masoko mengine ya ndani na nje Kwa kuzingatia zaidi ubora na vigezo zaidi.
Absalom Mwaipaja afisa biashara tecno saver amewataka wafanyabiashara kwenda kuzingatia Yale yote waliojengewa uwezo na wataalam ili waweze kusimama ipasavyo na kufanikiwa
Meneja wa Benki ya Equity jijini Arusha Francis Muro amesema kuwa beki hiyo inamuwezesha mfanyabishara kunufaika na mikopo mbalimbali ili kuwasaidia
Pia benki hiyo imekuwa ikiwasaidia wakulima na hata mtu mmoja mmoja katika ufanyaji biashara.
Pia kabla ya kumsaidia mteja kwanza huwekeana makubaliano hususani katika matumizi ya fedha ziweze kwenda eneo husika licha ya kuwepo Kwa changamoto.
Meneja wa kiwanda Cha maziwa Cha The Grande demams Nenyuata Fadhil amesema kuwa mafunzo kama hayo ni mazuri kwani yanawasaidia kuimarisha sekta ya uzalishaji na wafanyabiashara kujitambua,pia katika biashara kiwanda Cha the Grande demams mkoani arusha kimesema kuwa kinaendelea kutoa huduma afrika Mashariki na zaidi amewaalika wananchi kunywa maziwa Kwa wingi.
Comments
Post a Comment