WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI (BRELA) YAWAJENGEA UWEZO WADAU WA UZAAJI MAZAO YA KILIMO NJE YA NCHI.
Na Pendo Mkonyi,Arusha.
Pichani ni kaimu katibu tawala mkoa wa arusha Ramadhani Shabani.Kaimu katibu tawala mkoa wa arusha Ramadhani shabani amefungua Warsha ya takribani siku 3 ya wafanyabiashara wa mazao ya kilimo nje nchi mkoa wa arusha iliyoandaliwa na BRELA.
Akizungumza katika Warsha hiyo jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Golden Rose aliwataka wafanyabiashara kuzingatia mafunzo hayo muhimu ili waweze kufanya biashara zao katika hali nzuri bila ya usumbufu wowote.
BRELA imefanikiwa kuwakutanisha na kuwajengea uwezo Baadhi ya wafanyabiashara wa uzaaji mazao ya kilimo nje nchi mkoani arusha Kwa takribani siku 3Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa kitengo wa usajili wa kampuni Brela Bwana Isdor Paul Nkini katika Warsha ya Wauzaji wa Mazao ya Kilimo nje ya Nchi mkoa wa arusha amesema kuwa amewaku serikali inawataka wafanyabiashara kutekeleza SheriaMkuu wa kitengo wa usajili wa kampuni Brela Bwana Isdor Paul Nkini akizungumza na waandishi wa habari
Aidha BRELA wametekeleza majukumu yao kwa kuwapa elimu wafanyabiashara wa mpakani mara baada ya serikali kuwataka kufuata maelekezo na kuwataka kufuata kanuni,miongozo na taratibu, zilizowekwa.Serikali imeamua kushirikiana Brela ili kuwajengea uwezo zaidi Kwa kuwezesha wafanyabiashara kutekeleza hiyo miongozo hususani Kwa mkoa wa Arusha nini wafanye wakati wa utoaji huduma.BRELA imekuwa na mada maalum Kwa wafanyabiashara kuhusu namna ya kufanya usajili,majina ya Biashara yaweje na huduma zinazotolewa mara baada ya kufanya usajili.Mafunzo hayo yatadumu Kwa takribani siku 3 ambapo siku ya kwanza tutawapa elimu ya kufahamu kanuni za usajili wa kampuni na aina ya biashara na siku ya tatu tutawapa elimu kuhusu leseni ya usafirishaji na kesho kutwa kiliniki maalum ya kufahamu mifumo yao mara baada ya kujisajil ikiwemo kufahamu umuhimu wa kutumia mifumo ya kielektroniki.Aliwataka wafanyabiashara kujitokeza Kwa wingi kuja kujifunza mafunzo hayo kwani muhimu katika kuwaimarisha kibiashara ili waweze kuwa mabalozi waziri na kuepuka kuwa na mkwmo wa biashara.Changamoto kubwa iliyoonekana kwa wafanyabiashara ni kutofahamu sheria za ufanyaji biashara na kutofuata sheria taratibu na miongozo iliyopoBaadhi ya wafanyabiashara walioshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Agnesy Mush amewataka wafanyabiashara kujiwekea utamaduni wa kuhudhuria mafunzo kama hayo ili waweze kupata Mwanga wa namna ya kusajili kampuniAkitaja changamoto kubwa ambazo baadhi ya wafanyabiashara wanazihofia kuwa ni pamoja na uoga ikiwemo wafanyabiashara kutofahamu sheria ipasavyo.Mfanyabishara Mao Chizma amesema kuwa Warsha kama hizo ni muhimu na wafanyabiashara wanapaswa kuondokana na uoga wakati wa ufanyaji biashara na badala yake wasajili Biashara na kampuni zao ili waweze kuzifanya Kwa weledi.Hata hivyo BRELA inamuwezesha mtanzania kupata cheti Cha usajili wa kiwanda kidogo au leseni ya kiwanda Kwa njia ya mtandao na namna ya kuingiza taarifa za kampuni zilizosajiliwa nje ya mfumo wa mtandao katika mfumo wa usajili Kwa njia ya mtandao (ORS)
Comments
Post a Comment