ASKARI WANYAMAPORI WA VIJIJI KUTOKA MANYONI WAPATIWA MAFUNZO YA KUPAMBANA NA WANYAMA WAKALI NA WAHARIBIFU
Na. Prisca Libaga,Dodoma Wizara ya Maliasili na Utalii inaendesha mafunzo ya kudhibiti wanyama wakali na waharibifu kwa Askari wanyamapori wa vijiji wapatao 24 kutoka Wilaya ya Manyoni. Mafunzo yanayotarajiwa kukamilishwa Mwishoni mwa mwezi Februari 2024 ambaio yanaendeshwa katika Chuo cha Likuyu Sekamaganga kilichopo mkoani Ruvuma. Pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) Hayo yamebainika leo Bungeni wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) akijibu swali lililoulizwa na Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki ambaye alitaka kujua Je nini mkakati wa serikali wa kudhibiti tembo wanaoathiri wakulima wa korosho wa tarafa ya Nkonko? Aidha Mhe. Kitandula aliongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori nchini, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa na kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kusim