KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA KWA KUSIMAMIA VYEMA MIRADI YA REGROW


Na.Prisca Libaga ,Morogoro

Wizara ya Maliasili na Utalii imepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa kutekeleza na kusimamia vyema Miradi ya Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania(REGROW).

Pichani ni Mhe. Timotheo Mnzava(Mb) wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua na kutembelea miundombinu mbalimbali inayotekelezwa na mradi wa REGROW katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Timotheo Mnzava(Mb) wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua na kutembelea miundombinu mbalimbali inayotekelezwa na mradi wa REGROW katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi pamoja na Kujionea shughuli mbalimbali za kujikwamua kiuchumi zinazofanywa na vikundi vya COCOBA katika kijiji cha Mikumi.

Mhe. Mnzava aliongeza kuwa miradi inayotekelezwa kupitia miradi ya REGROW ni mkombozi sahihi katika kusadia kukuza utalii kusini mwa Tanzania kwa kuwa itaongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ambao watatembelea mbuga zinazopatikana kusini mwa Tanzania 

Mhe. Mnzava aliongeza kuwa kuwepo kwa vikundi vya kujikwamua kiuchumi COCOBA ni njia rahisi ya kukomesha vitendo vya ujangili hasa kwa jamii ambazo zinazozunguka hifadhi za wanyama na misitu.

Kupitia vikundi vya  COCOBA jamii inapata  elimu ya uhifadhi na  elimu ya kujikwamua kiuchumi kupitia mazao mbalimbali ya utalii, hivyo kuiepusha jamii kuwa na fikra ovu za kufanya ujangili wa kuharibu hifadhi za wanyama na misitu.

Aidha Mhe. Mnzava aliongeza kuwa ufadhili wa masomo kwa vijana wanaoishi pembezoni mwa hifadhi utaleta tija katika uhifadhi kwa kuwa vijana hao watakuwa walinzi wa kwanza wa kutunza maliasili wanyama na misitu lakini pia watajua faida ya kuwa na biashara ya utali katika maeneo yao.

Kwa niaba ya wizara ya Maliasili na Utalii Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula ameishukuru kamati hiyo kwa kutembelea na kukagua miradi hiyo.

Aidha Mhe. Kitandula alisema kwamba wizara imepokea miongozo, maelekezo na sehemu ambako kulionekana kuna changamoto wizara itafanyia kazi ili kuziondoa changamoto hizo.



Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.