IFAHAMU SHULE YA ST TIMOTHY NEWLAND KILIMANJARO KINARA WA MAADILI YENYE WANAFUNZI WAISHIO MAISHA YA UTAKATIFU YA KUONGOZWA NA MUNGU
Na Pendo Mkonyi, Kilimanjaro.
Shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya StTimothy iliyopo katika kata ya mabogini Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro imejikita katika utoaji wa elimu Bora yenye kumkomboa mtoto wa kitanzania kielimu na kuyafikia malengo yake.
Mkurugenzi wa shule hiyo ya Timothy Askofu James Bukulu amesema ni miaka 19 Sasa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo yenye misingi ya elimu Bora na maadili katika sekta hiyo
Amesema kwa miaka kadhaa shule imekua ikifanya vizuri Kitaaluma huku wakidumisha ujirani mwema kwa kusaidia wanafunzi wanaotoka Katika mazingira magumu kwa kuwapatia elimu.
Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi ya St Timothy Bwana James Bukulu.
Alisema kuwa wanafunzi wamefanikiwa kutokana na utii wa Mungu ndani yao kwani wamekuwa wakitenga Muda wa kumwabudu Mungu na kumpa kipaumbele katika maisha yao kwanza.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa shule imefanikiwa kuzalisha wanafunzi wataalamu shuleni hapo ambapo wapo ambao walishahitimu elimu ya vyuo vikuu na baadhi wamerudi kufundisha wanafunzi katika shule hiyo baada ya kupata ajira.
Alisema kuwa wanafunzi wote shuleni wamekuwa wakifaulu Kwa jitihada zao wenyewe hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye amekuwa akifaulu Kwa njia za udanganyifu
Kwa upande wake meshack Christian ambaye aliwahi kusoma shule hiyo miaka ya Nyuma na sasa ni Mwalimu wa Tehama shuleni hapo ,amesema Dunia ya sasa inabadilika katika ulimwengu wa kidigitali hivyo masomo ya Tehama ni muhimu kwa vijana na wanafunzi ili kuendana na ukuaji wa teknolojia.
Aliwataka wanafunzi kuhakikisha wanatoa kipaumbele katika masomo hayo ikiwemo wazazi wao kuwaruhusu watoto wao kujifunza Tehama kwani inalipa kwani kwasasa Dunia imejawa na teknolojia nyingi.
Baadhi ya wanafunzi wanaonufaika na mpango wa elimu akiwemo Precious Herman alisema kuwa shule ya st Timothy imewabadilisha kwa kiasi kikubwa kwani wameweza kujitambua na wameahidi kufika mbali kutokana na kiu ya ndoto zao.
Hata hivyo shule hiyo inaunga mkono wizara ya elimu kupitia mabadiliko makubwa ya mitaala mipya nakuhakikisha inateekeleza kwa kutoa elimu Bora.
Ni shule nzuri Sana!!! Ipo kwenye mazingira safi na ni rafki Kwa kujisomea, ufaulu uko juu, maadili safi na usafiri wa kutisha🙏🤝
ReplyDelete