SERIKALI YATAKIWA KUNGATA PANAPOSTAHILI BILA YA HURUMA ILI KUFIKIA MALENGO
Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Kanisa Katoliki Moyo safi wa Bikira Maria ungalimited linalomilikiwa na jimbo Kuu Katoliki Arusha laitaka serikali kuhakikisha linasimamia fedha za wananchi ipasavyo katika ujenzi mbalimbali wa barabara kwani maafa mengine yametokea kwa uzembe wa wakandarasi kujenga barabara chini ya kiwango.
Pichani ni padre Festus Mwangangwi wa kanisa la Katoliki Moyo safi wa Bikira Maria ungalimited linalomilikiwa na jimbo Kuu Katoliki Arusha.
Hayo yamesemwa na padre Festus Mwangangwi wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea mwaka mpya hayo yakiwa ni maoni na ushauri.
Alisema kuwa zipo changamoto nyingi nchi imepita kisiasa,kiuchumi,kidini na ni yapi ya kujifunza ili Neema na Baraka tele zopate kuwepo.
Padre Mangwangwi akigusia maafa yaliyosababishwa na ujenzi duni wakati mafuriko katika barabara mbalimbali mifereji na Madaraja mbalimbali ni chanzo Cha wakandarasi waliokosa uaminifu na kusababisha athari kubwa katika jamii.
Aidha padre Mangwangwi alisema kuwa kabla ya ujenzi kufanyika elimu itolewe kawnza ili kuepusha uharibifu wa fedha za serikali ambazo baadhi ya fedha hizo ni kodi za wananchi na za michango kutoka nchi za wenzetu.
Alihoji Kwa kuuliza kuwa je wakandarasi wanaokuwa wanafanya uzembe je Wana alama sahihi za utendaji kazi au wanafanya kazi Kwa kubahatisha kana kwamba wanaweza kujenga Leo na kesho wakabomoa tena.
Padre Mangwangi alisema kuwa wakati kiongozi anaposimamia nchi au kanisa,wilaya,mkoa anapaswa kuwa na msimamo na kuepuka huruma panapostahili kwani ukicheza na kima utavuna mabua mfano hao wananchi waliojenga katika mkondo wa maji wanapaswa kuondoka eneo hilo na siyo kuwatangazia tangazia waondoke maana ipo siku yanaweza kuja mafuriko makubwa wakaangamia wakati serikali ilikuwa na uwezo wa kuwataka kuhama maeneo hayo kwani maafa yakija serikali itagharamika na kupoteza Muda.
Kadhalika padre Mangwangwi hakusita kuzungumzia changamoto ya umeme nchini namna ambavyo unatesa watu kwani katika parokia ya Ungalimited vitu vyenye thamani ya zaidi milioni 3 zikiwemo friji,jiko na vingine vimeharibiwa na umeme kufuatia umeme kupiga shoti.
Alisema kuwa swala la kukatikakatika kwa umeme limekuwa ni kero kubwa sana kwanza ahadi ni nyingi sana ambazo hazina mashiko yeyote kutoka serikalini kwani wakati ule serikali ilisema mgao upo kutokana na ukame lakini hivi karibuni mvua kubwa zikinyesha kwana hata Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ilitangaza mvua kubwa na kweli zikinyesha na mabwawa mengi yalijaa maji.
"Sasa hilo bwawa la mtela halikuwa na maji kwani"kwanini fedheha hii nasema hii ni aibu kubwa hii ikoje kwani mbona hizo ahadi hazitelekezi kwani hii ikoje eti mitambo imekataa kuzunguka kwasababu mabwawa yamejaa maji mengi hili jambo nasema ni aibu kubwa sana hebu serikali itazame Hilo jambo kwani maendeleo yanletwa na mzunguko mzuri wa umeme .
Kadhalika alizungumzia swala la ushoga ambalo limekuwa ni changamoto duniani na kusema kuwa Kwa wale wanaojihusisha na vitendo hivyo wanawadhalilisha mpaka watoto wao kwani ni jambo ambalo halina kibali mbele za Mungu na wanada.
Aliwasihi viongozi wa serikali na dini,Sasa na vyama kuhakikisha Kwa namna yeyote jambo hilo linakomeshwa kwani maadili ni jambo jema sana katika maisha ya mwanadamu na serikali ili iweze kujiendesha ni lazima kuwa na watu wenye nidhamu njema.
Hata hivyo hakusita kutoa shukrani zake za dhati kwa viongozi wa serikali kwa kipindi cha msimu wa sikukuu namna ambavyo utulivu mkubwa umetawala hususani Kwa mkoa wa Arusha kwani hili limekuwa jambo la ajabu kidogo kufuatia amani kubwa kutawala kwani vijana almaarufu vibaka hawajafanikiwa kuleta madharau Kwa jamii pongezi Kwa jeshi la polisi,mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya Kwa kufanikisha amani hiyo.
Comments
Post a Comment