SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI
Na Pendo Mkonyi, Kilimanjaro
Mkuu msaidizi wa shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya Ritaliza iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro Bwana Simon Shayo anawatangazia wazazi na walezi nafasi za masomo kwa watoto wao kwa mwaka 2024.
Akizungumza na vyombo vya habari mkuu msaidizi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi ya Ritaliza amesema kuwa kutokana na umuhimu wa elimu Kwa watoto na ni haki yao kujisomea shule inazo nafasi chache za kuwapokea watoto Kwa madarasa yote.
Nafasi za masomo ni katika madarasa ya chekechea,1,2,3,4,5,na 6 na shule hiyo ni ya kutwa na Bweni kwa jinsia zote,shule inatoa huduma ya usafiri wa uhakika pamoja na upatikanaji wa huduma za kiroho Kwa dini zote.
Aidha shule ya Ritaliza ni shule ya mchepuo ya kiingereza (ENGLISH MEDIUM)iliyopo mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Rombo kata ya holili ambayo ilianzishwa mwaka 2007.
Shule ya Ritaliza inawalea watoto katika maadili mema sambamba na kuandaa jamii Bora ya kitanzania yenye maadili bora na hofu ya Mungu.
Kitaaluma shule ya Ritaliza imekuwa na matokeo mazuri hivyo mwitikio kwa wazazi umekuwa mkubwa na kuzidi kuiamini shule hiyo na kupeleka watoto wao shuleni hapo.
Kadhalika katika matokeo yake ya darasa la 7 mtihani wa Taifa mwaka 2022 waliofanya mtihani walikuwa wanafunzi 47 kati yao wavulana 21 na wasichana 26 walioupata daraja A walikuwa 42 na waliopata daraja B walikuwa 5 tu.
Mwaka 2023 katika mtihani wa Taifa waliofanya mtihani walikuwa wanafunzi 71 kati yao wavulana 28 na wasichana walikuwa 33 waliopata daraja A walikuwa wanafunzi 26 na daraja B walikuwa wanafunzi 44 na mwanafunzi mmoja tu alipata daraja c.
Shuleya Ritaliza inao waalimu wa kutosha kufundishia wenye weledi ,bidii na uzoefu katika kazi.
Ada za shule hiyo ni nafuu na zinalipwa Kwa awamu nne
Shule ina mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunza ambapo Kwa upande wa teknolojia shulehaipo nyuma kwani vipo vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunza mfano vishikwambi kompyuta projector.
Shule ya Ritaliza ina utaratibu wa kuandaa ziara za kimasomo Kwa wanafunzi wote.
Kwa Mawasiliano unaweza kupiga simu zifuatazo 07851 84845,
0782337976,0757897334. Karibu Ritaliza Kwa Elimu Bora.
Comments
Post a Comment