Posts

Showing posts from October, 2023

KAMPUNI YA NEW GREENLEAF SPORT & PROMOTIONS YAFANIKISHA MBIO ZA LAKE MANYARA MARATHONI

Image
  Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu. Mbio za Lake Manyara marathoni zimewakutanisha wadau mbalimbali wa michezo lengo likiwa ni kutangaza vivutio vya utalii Mto wa Mbu mkoa wa Arusha. Pichani ni Bwana Morris Okinda mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya New Green Leaf Sports & Promotions. Akizungumza na waandishi wa habari mwandaaji wa mbio za lake Manyara marathoni Bwana Moriss Okinda amesema kuwa Mbio za Lake Manyara marathoni ni mara ya kwanza kufanyika mto wa mbu mkoani  Arusha. Alisema kuwa licha ya hali ya hewa ya mto wa mbu kuwa ya joto wakimbiaji walifanikiwa na hii inaonesha kuwa endapo mwanamichezo akifanya mchezo eneo hilo atakuwa na uwezo wa kucheza mahali popote Duniani. Mikakati New Greenleaf Sport &Promotions ni kuibua vipaji  na kukuza vipaji vya  watoto wa kitanzania  na kuzalisha vipaji vingi. Alisema kuwa watu awali hakuna kama Mbio hizo zitafanyika Kwa kiwango Cha juu hivyo jambo ambalo qnawashukuru wahisani kutoka kampuni mbalimbali ikiwemo kampuni ya Mawasiliano  ya

WATANZANIA WAASWA KUTEMBELEA TWIGA CAMP SITE MTOAMBU

Image
  Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu. Watanzania wameshauriwa kujijengea utamaduni wa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kujifunza na kujionea. Pichani ni  Kevin Mushi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya  Twiga camp site  Hayo yamesemwa na Kevin Mushi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya  Twiga camp site wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizikuhusiana na huduma za kijamii zinazotolewa na kampuni hiyo. Alisema kuwa Huduma za hema  zinatolewa na camp site endapo ukihitaji uwanja utalipia shilingi 14,000 za kitanzania ukija na hema lako na ikiwa ukikodisha hema utalipia 15,000 na utachajiwa 14,000 Kwa mtu mmoja ambapo utahuduma vyoo maji moto na Maji baridi Mushi Alisema kuwa filamu ya mheshimiwa Rais aliyozindua imeletaa manufaa makubwa sana katika sekta ya utalii kufuatia kuwepo Kwa wageni siyo kama miaka 2 iliyopita wakati wa gonjwa la korona  Akizungumzia moja ya huduma anayoitoa maeneo hayo ya mahema amesema kuwa ni msaada mkubwa Kwa wadau wa utalii kufuatia kufurahia mfum

WAKIMBIAJI WA MBIO ZA LAKE MANYARA MARATHONI KWENDA KUTALII HIFADHI YA ZIWA MANYARA BURE

Image
Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu. Mkuu wa Hifadhi ya  Taifa ya ziwa Manyara na Kamishina msaidizi  Bi Evaline Mallya amesema kuwa wakimbiaji  wote walioshiriki katika Mbio za lake Manyara marathoni watapata nafasi ya kwenda kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali. Pichani ni Mkuu wa Hifadhi ya  Taifa ya Ziwa Manyara na Kamishina msaidizi  Bi Evaline Mallya Akizungumza na waandishi wa habari Kamishina msaidizi wa hifadhi hiyo ya lake Manyara marathoni  amesema kuwa amefurahishwa na Mbio hizo ambazo zimefanyika Kwa mara ya kwanza na kuhamasisha utalii katika mkoa wa Arusha eneo la mto wa mbu . Alisema kuwa kila mwaka watafanya Mbio hizo na kutoa taarifa zaidi Kwa jamii na  wadau wote wa utalii namna ya kushiriki Mbio hizo Akizungumza vivutio vilivyopo katika hifadhi ya ziwa Manyara mkuu huyo wa Hifadhi alisema kuwa ni pamoja na uwepo wa chemichemi za maji moto zenye joto la nyuzi kuanzia 65 mpaka 75 maji ambayo yanasadikika kuwa  ni tiba kulingana na Imani,Kuna daraja la juu lenye kit

RC MONGELLA AMUELEZEA MAREHEMU ZELOTHE ; ALIKUWA KIONGOZI ALIYENYOOKA.

Image
Na Prisca Libaga Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella amemuelezea Marehemu Zelothe Stephene Zelothe aliyekuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi (mstaafu) wa Jeshi la polisi nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, kuwa alikuwa ni Kiongozi aliyenyooka, muadilifu, mzalendo na mwenye kupenda watu na mwenye bidii katika kazi. Pichani ni  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella  Mhe Mongella ameeleza hayo mara baada ya sala fupi iliyofanyika nje ya jengo la kuhifadhia maiti,  Hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha, muda mfupi baada ya kuwasili mkoani Arusha na kuhifadhi mwili huo hospitalini hapo. Ameanza kwa kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa fursa aliyoitoa kwa maisha ya Mzee Zelothe hapa duniani, na kukiri kwamba kila mwanandamu anayosafari yake na mwisho huwa ni kifo na kusema kuwa marehemu Zelothe alikuwa ni Kiongozi hodari mwenye hekima nyingi na kauli thabiti, aliyenyooka na asiyekurupuka katika kufanya maamuzi. Amethibitisha kuwa, katika kipindi chote ambacho m

KAMPUNI YA UTALII YA AFRICAN GALLERIA YAONDOA ADHA YA MAJI KWA WANANCHI KILIMA MOJA PAMOJA NA KUJENGA MADARASA 7 YA SHULE YA KILIMATEMBO KARATU

Image
 Na Pendo Mkonyi,Karatu. Kampuni ya African Galleria imeendelea kushirikiana na jamii kutatua changamoto za kijamii Kwa kuwachimbia visima vya maji Kwa  wananchi na kujenga madarasa ya shule wilayani Karatu mkoani Arusha. Hayo yamesemwa na Kiliani Mwakulomba  meneja katika kampuni ya African Galleria wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kutatua changamoto kadha wa kadha eneo la Karatu ikiwemo ujenzi wa madarasa kuanzia darasa la 1 mpaka darasa la 7 katika shule Kilimatembo  Kibaoni pamoja na nyumba za waalimu. Pichani ni  Kiliani Mwakulomba  meneja katika kampuni ya African Galleria. African Galleria imefanya misaada hiyo ya kiutu Kwa kujali na kuonyesha upendo na Kwa wakazi wa eneo hilo kama njia mojawapo ya kudumisha ujirani mwema na mahusiano. Aidha kampuni hiyo ya African Galleria imefanikiwa kuchimba visima 3 eneo la Kilima  Moja ili kuondoa Adha ya maji Kwa wananchi wa eneo hilo hii ikiwa ni  alama ya ushirikiano kati ya kampuni hiyo n

MBIO ZA LAKE MANYARA MARATHON ZAFANA MTO WA MBU,WADAU WAKIMBIA WAKITALII,MSHINDI WA KWANZA ALAMBA MILIONI

Image
  Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Joshua Nassari ameshiriki mbio za Lake Manyara Marathon 2023 na kusema kuwa alisema kwa mara ya kwanza mbio zimefanikiwa zikiwa na malengo ya kuhamasisha Utalii. Pichani ni  Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Joshua Nassari    Mhe. Nassari alisema "kwa mara ya kwanza Wilaya ya Monduli imeandaa Marathon hii kwa lengo la kufungua fursa mpya ya utalii katika hifadhi yetu na kuongeza mzunguko wa fedha katika wilaya yetu". Mkuu huyo alisema kuwa hii ni fursa mpya ya utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara, hifadhi inayosifika kwa kuwa na  Simba wengi wanaokwea miti. Kuna Utalii mwingi lakini riadha ni utalii wa michezo na imehamasisha mzunguko wa FEDHA kutokana na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje  waliofika kushiriki una tunaimani mwaka ujao tutafanya vyema zaidi,"alisema Nassari. "Kwakuwa eneo la Mto wa  Mbu liko kimkakati wa kiutalii ndio imekuwa sababu kubwa ya kuvuta watu wengi kiasi hiki. Na tumeona ku