KAMPUNI YA NEW GREENLEAF SPORT & PROMOTIONS YAFANIKISHA MBIO ZA LAKE MANYARA MARATHONI
Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu.
Mbio za Lake Manyara marathoni zimewakutanisha wadau mbalimbali wa michezo lengo likiwa ni kutangaza vivutio vya utalii Mto wa Mbu mkoa wa Arusha.
Pichani ni Bwana Morris Okinda mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya New Green Leaf Sports & Promotions.
Akizungumza na waandishi wa habari mwandaaji wa mbio za lake Manyara marathoni Bwana Moriss Okinda amesema kuwa Mbio za Lake Manyara marathoni ni mara ya kwanza kufanyika mto wa mbu mkoani Arusha.
Alisema kuwa licha ya hali ya hewa ya mto wa mbu kuwa ya joto wakimbiaji walifanikiwa na hii inaonesha kuwa endapo mwanamichezo akifanya mchezo eneo hilo atakuwa na uwezo wa kucheza mahali popote Duniani.
Mikakati New Greenleaf Sport &Promotions ni kuibua vipaji na kukuza vipaji vya watoto wa kitanzania na kuzalisha vipaji vingi.
Alisema kuwa watu awali hakuna kama Mbio hizo zitafanyika Kwa kiwango Cha juu hivyo jambo ambalo qnawashukuru wahisani kutoka kampuni mbalimbali ikiwemo kampuni ya Mawasiliano ya Tigo,kampuni ya African Galleria,Hoteli ya Serena,Hoteli ya Kirumo Lodge, Manyara National Park, Fig Tree Camp na Bonite Bottle's .
Hata hivyo kampuni hiyo imesema kuwa itaendelea kumuunga mkono mheshimiwa Rais wa Awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kutangaza utalii na kuwezesha vijana katika sekta ya michezo ambapo kampuni hiyo imesema itaendelea kuandaa mashindano kama hayo lengo likiwa ni kuibua vipaji na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii mkoani Arusha.
Comments
Post a Comment