WAKIMBIAJI WA MBIO ZA LAKE MANYARA MARATHONI KWENDA KUTALII HIFADHI YA ZIWA MANYARA BURE
Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya ziwa Manyara na Kamishina msaidizi Bi Evaline Mallya amesema kuwa wakimbiaji wote walioshiriki katika Mbio za lake Manyara marathoni watapata nafasi ya kwenda kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali.Pichani ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara na Kamishina msaidizi Bi Evaline Mallya
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishina msaidizi wa hifadhi hiyo ya lake Manyara marathoni amesema kuwa amefurahishwa na Mbio hizo ambazo zimefanyika Kwa mara ya kwanza na kuhamasisha utalii katika mkoa wa Arusha eneo la mto wa mbu.
Alisema kuwa kila mwaka watafanya Mbio hizo na kutoa taarifa zaidi Kwa jamii na wadau wote wa utalii namna ya kushiriki Mbio hizo
Akizungumza vivutio vilivyopo katika hifadhi ya ziwa Manyara mkuu huyo wa Hifadhi alisema kuwa ni pamoja na uwepo wa chemichemi za maji moto zenye joto la nyuzi kuanzia 65 mpaka 75 maji ambayo yanasadikika kuwa ni tiba kulingana na Imani,Kuna daraja la juu lenye kita 28 kutoka aridhini na daraja Hilo lipo karibu na geti la kuingilia ziwa manyara ambalo linakuwezesh kufurahia wanyama waliopo maeneo hayo kama vile kima, Simba kwenye miti
Wanyama kama viboko,
Alisema kuwa ziwa manyara bado limeendelea kujaa vizuri licha ya changamoto za kupungua kipindi Cha mwanzo lakini Sasa hali ni nzuri na wapo watalii wengi wanafanya utalii wa kupiga kasia au kanui.
Hata hivyo alitoa rai kwa wakazi wa mto wa mbu kutunza maeneo ya mtawanyiko wa wanyama maeneo ambayo yana mapitio ya wanyama ili eneo hilo liweze kuwa salama ili kuendelea kuvutia utalii maeneo hayo
Kauli mbiu ya hifadhi hiyo ni utalii uanze na sisi na uhifadhi uanze na sisi.
Comments
Post a Comment