MBIO ZA LAKE MANYARA MARATHON ZAFANA MTO WA MBU,WADAU WAKIMBIA WAKITALII,MSHINDI WA KWANZA ALAMBA MILIONI
Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Joshua Nassari ameshiriki mbio za Lake Manyara Marathon 2023 na kusema kuwa alisema kwa mara ya kwanza mbio zimefanikiwa zikiwa na malengo ya kuhamasisha Utalii.
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Joshua Nassari
Mhe. Nassari alisema "kwa mara ya kwanza Wilaya ya Monduli imeandaa Marathon hii kwa lengo la kufungua fursa mpya ya utalii katika hifadhi yetu na kuongeza mzunguko wa fedha katika wilaya yetu".
Mkuu huyo alisema kuwa hii ni fursa mpya ya utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara, hifadhi inayosifika kwa kuwa na Simba wengi wanaokwea miti.
Kuna Utalii mwingi lakini riadha ni utalii wa michezo na imehamasisha mzunguko wa FEDHA kutokana na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje waliofika kushiriki una tunaimani mwaka ujao tutafanya vyema zaidi,"alisema Nassari.
"Kwakuwa eneo la Mto wa Mbu liko kimkakati wa kiutalii ndio imekuwa sababu kubwa ya kuvuta watu wengi kiasi hiki. Na tumeona kuanzia tarehe 27.10.2023 wakimbiaji walianza kuwasili hii yote imeongeza pato kwa taifa na mtu mmoja mmoja", aliongeza Mhe. Nassari.
Mbio hizi ndefu (Marathon) licha ya kuongeza fursa za kifedha kwa jamii pia, huimarisha afya na kuondoa magonjwa nyemelezi na kutoa mwanya kwa makampuni makubwa ikiwemo TANAPA kujitangaza na kupata wateja wanaowahitaji.
Amesema kuwa wanayo furaha sana kufanikisha Mbio hizo zilizoanzia lango la ziwa manyara ambazo Mbio hizo ni za kipekee kufanyika na kuhamasisha utalii na ni Matumaini Kila mwaka Mbio hizo zitakuwa endelevu.
Alisema wakimbiaji wa Mbio hizo watapata fursa ya kwenda kutembelea na kutalii katika hifadhi ya ziwa manyara kwani katika hifadhi hiyo vipo vivutio mbalimbali likiwemo bonde la ufa,ziwa manyara lenyewe lenye ndege wazuri wa kuvutia,wanyama kama kiboko,na chemichemi yenye ziwa maji moto kuanzia nyuzi joto 65-75 au mpaka 80 kulingana na kipindi maji ambapoyo yanasadikika ni tiba kulingana na Imani.
Mmoja wa wadhamuni wa mbio hizo za lake Manyara marathoni kutoka kampuni ya African Galleria Bwana Kilian Mwakulomba wakati akizungumza na vyombo vya habari amesema kuwa ni mara nyingi wamekuwa wakidhamini mashindano ya Mbio kama hizo na pia wao ni wadau wazuri kwani pia wamekuwa wakijitolea sana ili kujiunga mkono serikali
Pichani ni uongozi wa kampuni African Galleria mmoja ya wadhamuni wakubwa katika Mbio za lake Manyara marathoni.
Mbio za Lake Manyara Marathon zimefanyika kwa mara ya kwanza ziliandaliwa na kampuni ya Grean leaf Mohar zilihusisha kilometa 21, Kilometa 10 wanaume na wanawake pamoja na Kilometa 5.
Mwandaaji wa mbio hizo Morris Okinda kutoka kampuni ya Greanleaf Mohar alisema mwitikio umekuwa mzuri kwa wanariadha na wadau mbalimbali.
Pichani ni Morris Okinda kutoka kampuni ya Greanleaf Mohar Mwandaaji wa mbio za Lake Manyara Marathoni
"Nawashukuru wote waliofika akiwemo mkimbiaji mashuhuri Moses Kiptanui na pia wadhamini waliojitokeza katika kufanikisha mbio hizi na tutaendelea kuandaa kwa ubora zaidi,"alisema Okinda.
Alisema kuwa amewapongeza wadau kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania ambapo amesema kuwa Hilo ni tukio la mara ya kwanza na watu wamejitokeza na Mbio kama hizo zitakuwa endelevu huo ni mwanzo tu ambapo alitumia nfasi hiyo kuwapongeza wahisani kumuwezesha kufanikisha Mbio hizo.
Mmoja wa wawekezaji wakubwa katika hifadhi ya ziwa manyara Frank Mbuya meneja wa Manyara Lake view ambaye alifanikiwa kukimbia Mbio za km10 amesema kuwa amefurahia Mbio hizo kwani ni fursa ya kutangaza utalii eneo la mto wa Mbu,
Alisema wageni wengi kutoka ndani ya nchi na nje ya Tanzania wamekaribia Mbio hizo ambapo wao kama wawekezaji wa hotel maeneo hayo wamenufaika ambapo amehimiza Mbio hizo kufanyika mara Kwa mara.
Aliwataka watanzania hususani jamii ya mto wa mbu kuona umuhimu wa kushiriki Mbio hizo ikiwemo kutumia fursa wakati mwingine na kujitokeza Kwa wingi.
Kevin Mushi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga camp site eneo la mto wa Mbu wakati akizungumza katika Mbio hizo za Lake Manyara Marathon alisema kuwa ushiriki umekuwa mzuri na wanataraji Kwa kipindi kijacho watu kujitokeza zaidi.
Akizungumzia moja ya huduma anayoitoa maeneo hayo ya mahema amesema kuwa ni msaada mkubwa Kwa wadau wa utalii kufuatia kufurahia mfumo huo wa kupiga kambi kupitia hema na kufanya shughuli zao za utalii ipasavyo.
Mmoja wa wanachama kutoka kikundi kipya Cha hotel na lodges mtoa wa Mbu Bi Salama Ibrahim
Alisema kuwa Mbio hizo kwake zimemfurahisha sana kwani mwitikio umekuwa mkubwa sanabiwani yeye alifanikiwa kukimbia km 5 ambapo aliwataka watanzania kufika katika kampuni Yao kunufaika
Pichani ni Mmoja wa wanachama kutoka kikundi kipya Cha hotel na lodges mtoa wa Mbu Bi Salama Ibrahim aliyekimbia km 5
Naye Mwanariadha Herman Vitalis amefanikiwa kushinda mbio za kilometa 21 za Lake Manyara Marathon zilizofanyika eneo la mto wa Mbulu wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Vitalis alitumia muda waa saa 1:4:47 akifuatiwa na mshindi wa pili katika mbio hizo kwa wanaume ambaye ni Maiko Kishiba kutoka JKT Arusha kwa muda wa saa 1:05:05 na nafasi ya tatu kwenda kwa Mao Hando kutoka Katesh kea muda wa saa 1:05:28.
Mara baada ya zoezi la Mbio hizo mshindi huyo alijishindia kitita Cha shilingi milioni moja kama kifuta JASHO huku akiwa na malengo makubwa mwakani
Kwa Upande wa wanaume Kilometa 10 mshindi alikuwa ni Emanuel Dinda kutoka Katesh kwa muda wa dakika 29:36:2 huku wa wanawake akiwa ni Elizabeth Boniface kutoka Arusha muda wa dakika 35:59:36.
Comments
Post a Comment