WATANZANIA WAASWA KUTEMBELEA TWIGA CAMP SITE MTOAMBU

 Na Pendo Mkonyi,Mto wa Mbu.

Watanzania wameshauriwa kujijengea utamaduni wa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kujifunza na kujionea.

Pichani ni Kevin Mushi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya  Twiga camp site 

Hayo yamesemwa na Kevin Mushi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya  Twiga camp site wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizikuhusiana na huduma za kijamii zinazotolewa na kampuni hiyo.

Alisema kuwa Huduma za hema  zinatolewa na camp site endapo ukihitaji uwanja utalipia shilingi 14,000 za kitanzania ukija na hema lako na ikiwa ukikodisha hema utalipia 15,000 na utachajiwa 14,000 Kwa mtu mmoja ambapo utahuduma vyoo maji moto na Maji baridi

Mushi Alisema kuwa filamu ya mheshimiwa Rais aliyozindua imeletaa manufaa makubwa sana katika sekta ya utalii kufuatia kuwepo Kwa wageni siyo kama miaka 2 iliyopita wakati wa gonjwa la korona 

Akizungumzia moja ya huduma anayoitoa maeneo hayo ya mahema amesema kuwa ni msaada mkubwa Kwa wadau wa utalii kufuatia kufurahia mfumo huo wa kupiga kambi kupitia hema na kufanya shughuli zao za utalii ipasavyo.

 Ametoa ombi kwa serikali kutazama Kwa upya tozo  upande wa mto wa Mbu siyo game contolin Area  kitu ambacho kimewanyima wageni kwao na pia kumtoza mgeni Dola  29.5 na bado anatozwa Dola 10anakuwa ni mgumu kulala mto wa Mbu anaona ni  Heri aende Karatu

Hata hivyo wadau wa utalii wamehimizwa kutumia fursa iliyopo sass kufanya kazi Kwa bidii,na kutangaza nchi ya Tanzania KUPIKA shughuli za mikono  na Sanaa.

Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.