KAMPUNI YA UTALII YA AFRICAN GALLERIA YAONDOA ADHA YA MAJI KWA WANANCHI KILIMA MOJA PAMOJA NA KUJENGA MADARASA 7 YA SHULE YA KILIMATEMBO KARATU
Na Pendo Mkonyi,Karatu.
Kampuni ya African Galleria imeendelea kushirikiana na jamii kutatua changamoto za kijamii Kwa kuwachimbia visima vya maji Kwa wananchi na kujenga madarasa ya shule wilayani Karatu mkoani Arusha.
Hayo yamesemwa na Kiliani Mwakulomba meneja katika kampuni ya African Galleria wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kutatua changamoto kadha wa kadha eneo la Karatu ikiwemo ujenzi wa madarasa kuanzia darasa la 1 mpaka darasa la 7 katika shule Kilimatembo Kibaoni pamoja na nyumba za waalimu.
African Galleria imefanya misaada hiyo ya kiutu Kwa kujali na kuonyesha upendo na Kwa wakazi wa eneo hilo kama njia mojawapo ya kudumisha ujirani mwema na mahusiano.
Aidha kampuni hiyo ya African Galleria imefanikiwa kuchimba visima 3 eneo la Kilima Moja ili kuondoa Adha ya maji Kwa wananchi wa eneo hilo hii ikiwa ni alama ya ushirikiano kati ya kampuni hiyo na wananchi waliozunguka eneo hilo.
Kampuni ya African Galleria wanahusika zaidi na utalii ikiwemo huduma Kwa wateja ukiwemo utalii wa ndani na wa nje Biashara ya madini pamoja na utengenezaji wa vinyago wakiwemo mafundi wanaotengeneza hereni bangili na uwepo wa wapishi wabobezi katika vyakula mbalimbali.
Aidha Meneja huyo amesema kuwa kampuni hiyo imewezesha watanzania kunufaika na soko la ajira Kwa kuzalisha na kutengeneza bidhaa mbalimbali za mikono ikiwemo kutengeneza vinyago,hereni,bangili,Shanga na bidhaa zinginezo lengo likiwa kutangaza biashara ya utalii Tanzania.
Akizungumzia mabadiliko ya utalii eneo hilo meneja huyo amesema kuwa mara baada Rais kutangaza vivutio vya utalii kupitia filamu ya The Royal Tour African Galleria wamekuwa wakipata watalii wa wageni kuanzia 100 Kwa siku ambao siyo rasmi Kwa biashara.
Alisema kuwa mheshimiwa Rais amesaidia pakubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma kwani uwepo wa wagaeni ni mkubwa sana na Kila mmoja ananufaika
Kadhalika meneja huyo ameiomba serikali kupunguza kodi katika kazi za mikono za Sanaa zinazozalishwa na watanAnia kufuatia kutokuwa na faida kubwa ili kuendelea kuwavugia wageni zaidi watanzania waweze kunufaika.
Comments
Post a Comment