DCEA YAPIGA HODI WILAYANI MWANGA; YATOA ELIMU KINGA KWA WANAFUNZI NA JAMII SOKONI MWANGA

Na Prisca Libaga Maelezo, Mwanga

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya Wilaya ya Mwanga tarehe 19.09.2024 imetoa elimu kinga kwa makundi mbalimbali  juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. 

Jumla ya watu 2,500 walipatiwa elimu kinga ikihusisha wanafunzi wa Shule za Sekondari za Mwanga, Vudoi na Mandaka pamoja na wafanyabiashara/wachuuzi wa  Soko la Mwanga.

DCEA Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha wananchi  wa Wilaya ya Mwanga washirikiane na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya waliopo katika maeneo yao wanayoishi kwa kupiga bure namba ya simu 119.


Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.