TPHPA YAHIMIZA UZALISHAJI WA MAZAO YASIYOTUMIA KEMIKALI ZA SUMU
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Nchini TPHPA imetilia mkazo wa uzalishaji mazao yasiyo na sumu ili kupanua wigo katika soko la dunia kwa lengo LIKIWA ni kulinda afya za walaji.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Wadau wa TPHPA Jijini Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliyetarajiwa kuwa Mgeni Rasmi, ameipongeza mamlaka hiyo kwa jitihada zake kubwa za kuleta mabadiliko na uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo.Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda (katikati kushoto) akipata ufafanuzi wa bidhaa zinazozalishwa na Mamlaka(TPHPA) hiyo kutoka kwa Dkt. Neduvoto Mollel wa kwanza (kulia).
Aidha ameongeza kuwa, Sekta ya Kilimo ni mkombozi kwani inategemewa kuongeza ajira kwa jamii hususani vijana na wanawake, kuimarisha mfumo wa chakula na kuongeza pato la taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
"Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta hii muhimu imeongeza bajeti kutoka Bilioni 970 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kufikia Tirioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, hii yote ni kuhakikisha tunajiimarisha katika soko la dunia na kuzidi kuwa bora katika uzalishaji wa chakula cha kutosha"
Ameongeza kuwa, TPHPA inatambua juhudi za serikali katika utekelezaji wa majukumu yao, ushauri na maelekezo muhimu yenye lengo la kuhakikisha mamlaka hiyo inaimarika na kuendelea kufanya vizuri.
"Tunaendelea na jitihada za kutanua wigo wa kilimo cha umwagiliaji lakini pia kupambana na changamoto mbalimbali zikiwemo usugu wa viuatilifu, kupotea kwa vinasaba katika mimea ya asili, ubunifu na mbinu juu ya viuatilifu sambamba na hayo tunajipanga kwa matumizi ya akili mnemba ili kuendana na Maendeleo ya Teknolojia lakini pia kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi" ameeleza Prof. Temu.
Mkurugenzi wa TPHPA Prof. Joseph Ndunguru ameeleza kuwa, mkutano huu umetoa fursa kwa wadau wa sekta ya kilimo kubadilishana uzoefu, changamoto na ushauri katika kuleta mageuzi kwa sekta hiyo.Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Nchini (TPHPA) Profesa Joseph Ndunguru.
Naishukuru kamati ya kudumu ya Bunge, inayosimamia Wizara ya Kilimo, Viwanda na Biashara kwa kupitisha bajeti ambayo imetupa tumaini la kufikia malengo tuliyojiwekea TPHPA" ameeleza Prof. Ndunguru.
"Nawasisitiza Mamlaka ya TPHPA kuhifadhi mbegu za asili, hii itasaidia kuepuka upotevu wa mbegu bora zinazotegemewa katika ushindani wa soko la dunia" amesisitiza Kaganda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPHPA Prof. Andrew Temu amesema kuna muelekeo wa mamlaka hiyo kutimiza malengo yake ya kuboresha afya za watu kutokana na juhudi na mikakati mbambali inayowekwa.
Comments
Post a Comment