KAMPUNI YA UTALII YA KILL FAIR KUKUTANISHA WADAU WA UTALII ZAIDI YA 600 JUNE 7 HADI JUNE 9 JIJINI ARUSHA

Na Pendo Mkonyi,Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Angela  Kairuki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair 2024  yanayotarajiwa kufanyika Juni  7 hadi 9 mwaka huu mkoani Arusha .

Aidha katika maonyesho hayo wanunuzi zaidi ya 600 wa Utalii kutoka nchi  40 duniani na waonyeshaji pamoja na wadau 468 wa utalii kutoka nchi 37, wamethibitisha kushiriki maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair  yanayotarajia kuanza Juni 7 hadi 9 mwaka huu jijini Arusha.
Vile vile wadau hao na wanunuzi  wa  utalii  watatembelea vivutio vya utalii, ili wakawe mabalozi wazuri kwenye nchi zao.


Mkurugenzi wa Kili fair Ltd Dominic Shoo  ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo,amesema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza vivutio vilivyopo nchini pamoja na kuonesha tamaduni mbalimbali za kiafrika. 
Pichani ni mkurugenzi  wa Kampuni ya Kill fair 
Bw Dominic Shoo 

Alisema kuwa Kwa takribani siku tatu tunatarajia kuwa na kiwango kikubwa cha biashra kwa sababu lengo letu kubwa  kukutanisha wadau toka mataifa mbalimbali duniani, kuja kujua vivutio vyetu hapa Tanzania, wavitembelee na kuweza kuwa mabalozi wazuri, kwa ajili ya kuuza vivutio vya Tanzania.   

Mwaka huu onyesho hilo ni kubwa kuliko la mwaka jana, sababu  wamekuwa na waonyeshaji zaidi na mwamko wa  wanunuzi ni mkubwa kuliko mwaka jana na wamekua na kiwango cha juu, kuliko mwaka jana kutokana na vitu ambavyo wameweza kuvinunua, ili kuhakikisha onyesho hilo linalingana na hadhi ya viwango vya kimataifa.

Naye Mkuu wa kitengo cha masoko na mauzo kutoka kampuni ya Media works Noel Petro ,amesema asiilimia 70 ya wateja wao wanatokana na utalii na ndiyo maonyesho ya kipekee sana huku akiiomba serikali kujengwa kwa mabanda ya maonyesho ya kudumu ili kuwepo kwa mazingira salama nyakati zote.
Pichani ni Mkuu wa kitengo Cha masoko na mauzo Kampuni ya Media Works Bw Noel Petro

"Maonyesho haya ni ya kipekee kwetu sisi kwani yanaleta fursa ya utalii kwani wateja wetu wakubwa wanatokana na utalii,kila mtu atakayekuja kwenye banda lao atapata punguzo kubwa la gharama na wamekuja na fursa ya kupunguza changamoto ya taka ngumu ikiwemo chupa za maji ili kuokoa mazingira"amesema 

Kwa upande wake Daniel Sambai kutoka Serena hotel amesema kuwa, kila mwaka ongezeko la wanunuzi limekuwa likiongezeka kutoka nchi 34-40 na hii ni kutokana na uongozi na usimamizi imara wa waandaji hao ambao umekuwa mkubwa .

"Naupongeza uongozi wa Karibu Kili fair kila mwaka wanunuzi wanaongezeka na cha msingi nisema tuu wakija wanunuzi Wazuri wanachangia kuleta wageni wengi Nchini na nchi zimeendelea kuongezeka."amesema .


Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.