SERIKALI KUIMARISHA ULINZI WA MALI NA MAISHA YA WATU DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU.

Na. Anangisye Mwateba-Dodoma

Serikali kupitia Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuimarisha ulinzi wa mali na maisha ya watu dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo yenye changamoto nchini ikiwemo Kiwangwa, Bwilingu, Mkangena na maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Pori la Akiba Wami-Mbiki.Pichani ni Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula

Haya yamebainika wakati Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula akijibu swali la Mhe. Subira Khamis Mgalu(Mb) aliyetaka kujua Je, Serikali imefikia wapi kuzuia Tembo kuharibu mazao na kuwadhuru wananchi wa Kiwangwa, Bwilingu, Mkange na wanaozungukwa na Hifadhi ya Wami-Mbiki.

Mhe. Kitandula alisema  Wizara imechukua hatua ya  Kuweka kambi za muda za Askari na kuwapatia vitendea kazi (magari na pikipiki) kwa ajili ya doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu.

Mhe. Kitandula aliongeza kuwa hatua nyingine ni kufanya doria za udhibiti wa wanyamapori kwenye maeneo yenye changamoto ya tembo ikiwemo eneo la Mkangena ambalo lipo karibu na Hifadhi ya Taifa Saadani.

‘Vilevile wizara inatoa elimu kwa jamii kuhusu namna bora ya kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori wakali na waharibif na Kusambaza kwa wananchi namba maalum katika mikoa yote ambapo kwa Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Morogoro namba ya kupiga simu bure (0800110098) kwa ajili ya kutoa taarifa za matukio ya uvamizi wa wanyamapori akiwemo tembo kwenye makazi ya watu ili kuwezesha Askari kufika haraka na kuwadhibiti’ Alisema Mhe. Kitandula

Mhe. Kitandula pia aliongeza kuwa matukio 47 ya wanyama wakali na waharibifu yanafanyiwa tathmini ili wananchi waliothiriki waweze kupata stahiki zao kutokana na uharibifu uliotokea.

Aidha Mhe. Kitandula alisema kuwa wizara iko teyari kushirikia na vikundi mbalimbali vya ufugaji nyuki ikiwamo kutoa utaalamu wa ugani pamoja na kutoa mizinga ya kufugia nyuki ya kisasa.

Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.