DKT. BITEKO APONGEZA CHUO CHA UTALII
Na Pendo Mkonyi,Dar es salaam
Chuo cha Utalii kimepongezwa kwa kupokea vijana 20 kwa ajili ya kusomea masuala ya Utalii na ukarimu kupitia ufadhili wa Dkt. Samia Suluhu Hassan scholarship.
Pichani ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko(Mb)
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko(Mb) wakati akifungua Kongamano la uwekezaji la Wilaya ya Pangani katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mhe. Biteko aliweka msisitizo kwa vijana hao 20 ambao wanatoka wilaya ya Pangani kuwa wamepata bahati ya ufadhili huo wakasome kwa nguvu na bidii, pia wajiepushe na mambo maovu ambayo yanaweza kuwaharibia safari yao ya Masomo.
Mhe. Biteko emeipongeza Wizara ya Maliasi na Utalii ikishirikiana na Taasisi zake kwa kuendelea kuzalisha fursa na mazao mapya ya Utalii hasa kwenye Wilaya ambazo zina vivutio vya Utalii.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alisema kuwa kongamano la Utalii la Wilaya ya Pangani litaisaidia wizara kutimiza lengo la kufikia watalii Milioni tano na kufikisha mapato ya Dola za Kimarekani Milioni mia sita ifikapo mwaka 2025.
Comments
Post a Comment