SHULE YA MSINGI YA MCHEPUO WA KIINGEREZA YA MIALE YA JIJINI ARUSHA IMESEMA KUWA INAONA FAHARI KUWAKUZA WATOTO KIMAADILI ZAIDI
Na Pendo Mkonyi Arusha
Shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi Miale iliyopo Kata ya Ilboru imeendelea kushika nafasi kwa kuongoza kitaaluma pamoja na kuwainua watoto kimalezi kutokana na elimu bora inayotolewa hapo.
Akizungumza meneja wa taasis hiyo ya elimu ya Miale Stanley Keneth amesema kuwa kama shule wamejitahidi kuwasaidia watoto kujitambua kwa kujua kusoma na kuandika ipasavyo.
Pichani ni Meneja wa shule ya Miale Stanley Kenneth
Aidha shule hiyo tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikifanya vizuri na kuwa na matokeo mazuri na wanafunzi wengi wamefanikiwa kufaulu na kujiunga na elimu ya sekondari maeneo mbalimbali
Shule ya mchepuo wa kiingereza Miale imesema kuwa michezo kwao ni kipaumbele kwani wamefanikiwa kuwatoa watoto wengi kimichezo walioshiriki katika michezo ngazi ya mkoa.
Mikakati mikubwa ya Miale ni kufanya vizuri kitaaluma,ikiwemo mwanafunzi kujiamini,sambamba na kumuwezesha mwanafunzi kuzungumza lugha ya kiingereza vizuri na kuiandika ipasavyo.
Miale ni miongoni mwa shule zinazotoa elimu ya awali na msingi na uwepo wa waalimu wasomi wenye maadili bora pamoja na viwango vya juu vya elimu
Ikiwemo ufundishaji kwa njia ya vitendo na nadharia.
Shule ina maktaba nzuri kwa ajili ya wanafunzi kujisomea ambayo humsaidia mwanafunzi kuyaelewa masomo vizuri kutokana na uwepo wa vitabu mbalimbali.
Shule ya Miale Kipaumbele chake kikuu kwa mwanafunzi ni malezi bora kwani watoto hupewa semina kila wiki kupitia wataalam na kamati ya ufuatiliaji maadili ili kupinga ukatili kwa watoto ili waweze kuwa salama.
Elimu inayotelewa hapo humfanya mwanafunzi kuwa na uwezo wa kimasomo hivyo Miale ni eneo salama Kwa watoto kuweza kujipatia elimu bora na malezi ili kumuwezesha mtoto kufikia ndoto zake.
Mkuu wa shule ya Miale Obadiah Likimbashe
Amesema kuwa kitaaluma shule ya hiyo imekuwa ikifikia wastani uliowekwa na serikali na kila mwaka wanapotoa darasa la 7 hufanya vizuri na watahiniwa wote kufaulu Kwa kiwango Cha alama A na B.
Pichani ni mkuu wa sule Obadiah Likimbashe
Shule ya Miale ilianza mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 87 na mpaka Sasa 2023 ina wanafunzi 324 na tokea shule kupata usajili serkalini mwaka 2017 na mwaka 2018 darasa la 7 walifanya mtihani na kufaulu Kwa alama A na B.
Mwaka huu 2023 shule hiyo imeendelea kuwahidi wazazi wanafunzi wao kufaulu kwani mwaka jana 2022 wanafunzi wote 33 waliofanya mtihani wa darasa la 7 walifaulu na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza sekondari.
Vilevile shule hiyo imekuwa ikifanya mitihani ya ujirani mwema na shule zingine na lengo ni kuinua taaluma licha ya kuogepewa shule hizo kwani wao Miale hawapo kiushindani bali kuwasaidia wanafunzi Kwa kuwajengea uwezo kimasomo.
Miale inamdhamini mtoto kwanza kwani ni taifa la Leo na siyo la kesho kwani wapo Marais wanasheria hivyo wazazi wanakaribishwa kuwekeza Kwa watoto ambapo pia wameaswa kuwafunza watoto na kuwalea iwapasavyo wasiwe bize na kazi na kuwasahau watoto wao ili kuzidi kuwa na kizazi chenye maadili na kinachompendeza Mungu.
Alitoa rai kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao na kuwaonesha upendo ikiwemo ili mtoto anapopatwa na tatizo iwe rahisi kumshirikisha na kuweza kuondokana na changamoto ambayo ingemkabili.
Hata hivyo serikali imeombwa kupunguza kodi katika taasis za elimu binafsi ili ziweze kujiendesha kufuatia baadhi ya wazazi kutokuwa na uwezo wa kulipia watoto wao karo za shule.
Comments
Post a Comment